STORI; MAAMUZI YAPI YAFANYIKE? MTUNZI; ALANA JOSEPH. Baada ya mahusiano ya mda mrefu kati ya Celine na James , walifikia muafaka Wa kutaka kuoana. Hatua ya kwanza ilikuwa ni wao kutambulishana kifamilia. Celine alimwambia James, " unajua tumekuwa pamoja kwa muda mrefu pasipo wazazi wetu kujua! Tufanye mpango tuwakutanishe na pia tuwaeleze namna tunavyopendana." James alifurahi sana. Walipanga siku ya kujitambulisha kwa wazazi wao. Siku hiyo iliwadia. Celine alifika na mama yake, James alifika na Baba yake. Kwani kila mmoja wao ndio mzazi aliyekuwa naye. Chakustaajabisha, mama Celine na Baba James ni wapenzi waliopotezana kwa muda mrefu. Katika kupotezana kwao, walipata watoto ambao ndio hawa wapenzi [Celine na James]. Pamoja na hayo yote yaliyotokea wakati wamepotezana, lakini bado walikuwa wanapendana. Kila mtu alikuwa na imani yakwamba watakuja kukutana na kuwa pamoja tena........ Sasa, Siku hiyo ilipowadia ilikuwa ni gumzo! UNADHANI MAAMUZI GANI YAFANYIKE? UHUSIANO GANI UENDELEE?