PENZI LANGU 1 - 3

 PENZI LANGU 01

PENZI LANGU 01


ANZA ...Mkoani tabora walionekana watu wawili ambapo Kwa kuwatazama tu ni kama vile walikua wapenzi ambao wamuda mrefu sana wakati huo mwanamke alikua ameshika kimfuko kidogo huku mwanaume akiwa ameshika mkono wake wakiwa wanatembea Hadi walipofika kwenye kituo cha treni mwanamke akazungumza


"Suma naomba sana usinisahau sababu nakupenda sana na nakutegemea wewe Suma kumbuka wewe na mama Yako ndo familia yangu kwasasa na kumbuka wapi umenitoa Suma nakupenda sana"


"Aisha usijali nakuahidi kua kidogo chochote nitakachokipata nitawatumia sababu sitaki mpate shida we na mama yangu kumbuka kua naenda mjini ni vile nahitaji kubadirisha maisha yetu sababu sitaki tubaki kuwa wakulima wadogo naenda kutafuta Ili tuweze kuwa wakubwa zaidi na wenye kutumia pembejeo za kisasa mpenzi"


"nakuamini sana na kama alivyokupa baraka mama Yako na mimi pia nakupa baraka zangu"


Aisha alikua anahuzuni sana kuagana na mpenzi wake ambae alikua anaempenda sana na kumheshimu Kwa kiasi kikubwa.


haukupita muda mrefu mara treni ambayo alitakiwa apande illifika na Suma alipanda kwenye treni akakaa kwenye siti huku akimpungia mkono mpenzi wake Aisha.


na watu wengine walipanda pia Kisha treni ikaanza safari yake kuelekea dar es salaam.


Aisha alirudi nyumbani kwao na kumkuta mama yake na Suma akiwa amekaa kinyonge Aisha akamsogelea mama yake Suma na kumwambia


"mama usijisikie vibaya naamini kua anatupenda sana hawezi kutuacha wenyewe hata kidogo naomba tuweke Imani kwenye hilo sababu tukiwa na mawazo mabaya itamuwea vigumu hata Kwa upande wake"


"nakuelewa sana Aisha usijali Mimi nipo sawa kabisa na nitafurahia sana endapo nitamuona kijana wangu Suma amerudi salama na kuja kufunga ndoa na wewe mwanangu mpole mwenye heshima"


"Asante mama ila wacha niandae chakula alafu niende shambani nikamalizie kupalilia shamba"


basi Aisha alifanya hivyo na kisha akondoka kuelekea shambani na kumuacha mama Suma nyumbani sababu alikua mgonjwa wa miguu hivyo alikua anapata shida sana kwenye kutembea.


wakati Aisha anaelekea shambani mara Ghafla akakutana na mwanaume mmoja ambae alionekana kua na maongezi na yeye Aisha alipomkaribia tu kabla ya huyo kijana kuzungumza akamwambia


"Joel naomba tafadhali niache nipite sitaki usumbufu wa aina yoyote maana ukiendelea kunifata fata nitakuja kufanya kitu kibaya sana"


"hahaha Aisha unaonekana kuwa na msimamo sana lakini safari hii nimekuja mwenyewe ila siku ambayo nitakuja tena nitakuja na wenzangu najua kihelehele chako kitakuisha"


"huwezi kunitisha Kwa Chochote kile na ukijifanya mjuaji na mimi nitakukomesha"


Aisha alimsukuma Joel na kuondoka zake,Joel alimshangaa sana kujihuliza

"huyu mwanamke anajiamini Nini na mbona mpenzi wake ambae alikua anamtetea ameshaondoka kwanini Bado anajiamini kiasi hiki,lakini pia yupo tofaut na wasichana wa hapa kijijini labda ndio maana anajiamini sana maana wasichana wa hapa ukimuonesha hata elfu Moja tayari washakubali unaipata show Yako Moja kisha unatulia ila huyu Sasa ni mgumu sana ila nitamkomesha siishii hapa"


Joel aliondoka zake.


muda ulizid kwenda hatimae jioni iliwadia Aisha alitoka shambani akiwa na mizigo yake na Moja Kwa Moja Hadi Kwa mwenye kiti akamsalimia na kumwambia


"samahani mwenye kiti ninashida nataka nikuambie"


mwenye kiti nayeye alikua anamtamani sana Aisha Kwa muda mrefu sana lakini Aisha alikua na msimamo sana hapo kijijini sababu alikua anampenda sana na kumuheshimu Suma kutokana na jinsi alivyompat na kumsadiia,hivyo mwenye kiti Kabla Aisha hajasema shida yake akamwambia


"Aisha kwanza vipi kuhusu nilichokuambia sababu mpenzi wako ameshondoka tayari"


"mwenye kiti sikuja hapa kwaajiri ya kujadiri hayo mambo nataka unisaidie Kuna vijana wananisumbua na wamepanga kunifanyia kitendo kibaya muda wowote ambao nitakua peke yangu nikienda shambani au kisimani pia"


"ooh jamani usijari kuhusu Hilo Aisha mpenzi nitashughulikia Wala usiwe na wasiwasi"


Aisha alisimama na kuondoka zake huku akimuacha mwenye kiti amejawa na tamaa za kimwili na yeye,Aisha alipoondoka mwenye kiti akasema

"yani huyu mtoto Kila nikikutana nae lazima tu niwe na mshawasha hivi ananini lakini ,ila mh mtoto mashallah anavutia Kila idara kwanza mweupe ana shape nzuri yaani daha natamani Ile siku ningemuokoa Mimi lakini ningewezaje sasa wakati nguvu ya kumtoa nilikua Sina,ila ananichanganya sana huyu binti lazima nimpate"


Aisha alirudi nyumbani kwao na kumkuta mama yake mkwe anapika Aisha akamuhuliza


"mama kwanini unapika SI nitapika Mimi jamani?"


"Aisha unafanya kazi nyingi Hadi nakuonea huruma ona sasahiv ulivyokonda wakati haukua hivi,Aisha kumbuka kua wewe hukutakiwa kuishi Maisha ya shida ila sema ndio hivyo hatuna uwezo"


"mama Mimi najiona heli ya umaskini wenye furaha kuliko utajiri wenye unaishi Kwa wasiwasi na tangu nifike hapa kwako nimekua na amani sana na furaha hivyo usijari mama"


"kweli unafuraha ukiwa kwenye Maisha haya?"

"zaidi ya sana mama na Wala usiwe na wasiwasi kuhusu Mimi"


basi Aisha alisogea kibandani na kuendelea na mapishi ambayo akiyaanza mama yake na Suma.


upande wa kwenye treni Suma alikua anawaza tu endapo atafika huko mjini ataishi wapi sababu Hana ndugu Wala jamaa hio kitu ilikua inamuwazisha sana akilini mwake.


baada ya siku tatu walifika jijini dar walishuka kituoni na Kila mmoja kuingilia sehemu anayoijua yeye.


upande wa Suma alikua hajui mitaa Wala hakua anajua wapi anaelekea alichojua yeye amefika dar basi Kambi yake itakua popote ambapo ataona patamfaa.


alitembea sana siku hivyo Hadi inafika majira ya jioni,akiwa zake maeneo ya kwenye soko la tandale mara ilikuja gari ambayo ilikua imepata hitilafu kidogo na dereva alishuka kwenye gari mara Moja na kutaka kutazama shida Nini akawa haelewi Nini afanye mara akageuka geuka na kumuonua Suma akiwa amekaa kinyonge akamuita


"oya we kijana njoo mara Moja"

Suma alisimama haraka na kusogea pale Kisha akaambiwa

"em niangalizie hapa mana sielewi hata"

kwakua Suma alishajifunza funza kijijini kwao jinsi ya kutengeneza magari pikipiki na baiskeri hivyo haikumuwea vigumu kugundua tatizo la kwenye hiyo gari,akatengeneza fasta na kumwambia


"jaribu kuwasha gari"


mwenye gari alifanya hivyo na mara hii gari ikawaka safi kabisa Suma hakutaka kuwa na pupa alifunga pale palipofunguliwa Kisha akasogea pembeni na yule jamaa alikua anaongea na simu na baada ya kumaliza akamuita Tena Suma alisogea na Kisha akamwambia

"shika hii pesa itakusaidia pia Asante Kwa kunitengenezea gari yangu"


"kaka Asante pia ila Mimi sitaki pesa nataka unisaidie kazi na sehemu ya kulala "


"ooh kumbe hauna makazi?"

"ndio kaka mi ni mgeni hapa ndio nimefika Leo tu kutoka tabora"


"ohk panda kwenye gari tuondoke"

Suma alikimbilia mfuko wake na Kisha kurudi Kisha akapanda kwenye gari na kuondoka na huyo jamaa.


gari iliendeshwa Hadi kwenye maeneo ya kinondoni Kisha gari ikapaki kwenye nyumba moja hivi Kisha akamwambia

"hapa ndo napoishi karibu ndani"

"Asante saña kaka"

waliingia ndani na Kisha wakapata chakula pamoja Kisha akamuonesha sehemu ya kuongea Kisha akampa shuka akalala seblen na yeye akaingia chumbani kwake.


Suma alimshukuru sana na kusema

"Asante mama Kwa Dua zako Mungu amejibu maombi yenu Kwa siku ya kwanza napata msamalia mwema wa kunisaidia wengi naskia wanapata shida sana kuhusu sehemu za kulala ila Mimi Leo nalala ndani Asante saña Mungu wangu"


Suma alilala pale seblen Hadi asubuhi mapema,aliamka na kuanza kupanga vitu vizuri mara ghafla mlango wa chumba ukafunguliwa na akatoka yule jamaa na mke wake akimuweka vizuri tai na kumchana nywele Kisha akazungumza

"dogo huyu ni mkewangu Jana sikukutambulisha sababu alikua amelala hivyo huyu mkewangu na pia mama watoto huyu ni yule kijana ambae nilikuambia hivyo atakaa hapa huku nikimfanyia mchakato wa kazi na sehemu ya kuishi"


"Sawa mmewangu,karibu sana shemeji"

"Asante saña"

basi walitoka nnje na kumwambia

"dogo sikia Wacha Mimi niende kqzini afu Kuna sehemu pale nitakuangalizia Kisha kesho utaanza kazi au hata Leo nitamtma mtu akufate"

"Sawa kaka hakuna shida"

yule jamaa aliondoka na kumwacha Suma na mkewake.


upande wa kijijini sasa Aisha aliamka kama kawaida yake na kuelekea shambani lakini akiwa njiani simu iliita na kuanza kuzungumza na hakua miwngine alikua Suma alifurahi sana kumskia na baada ya kumuhulizia mama yake akamwambia kua yupo shamba na muda ambao atarudi atamwambia Ili ampigie ukweli siku hiyo ilikua ya furaha saña Kwa Aisha na aliwahi kufika mapema sana shambani na kuanza kulima lakini ghafla walitokea vijana watatu na kumbeba Aisha mpaka mafichoni kwaajir ya kutaka kum'baka wakati wawili wanafanya doria kwaajir ya watu ambao watakaokua wanapita hapo mara ghafla.....


usikose itaeendelea....


PENZI LANGU 02

Kwenye harakati za kutaka kum'baka Aisha mara Ghafla walifika vijana wengine wanne walionekana kuwa na nguvu sana kisha wakasikia sauti ikizungumza




"vijana mnajifanya wanaume ambao mnajari sana hisia zenu kuliko utu wa mtu sio?,Sasa basi leo nitawafundisha jinsi ya kuishi na watu vizuri,vijana shika hao waadhibiwe haraka"




wale vijana wanne waliwakamata Joel na wenzie walipigwa saña na wakachomwa moto kabisa,Kisha mwenyekiti akamwambia Aisha


"umeona nimeamua kuwateketeza Kwa namna Ile ya kukutoa wasiwasi mpenzi na yeyote ambae atakusumbua basi niambie mapema nitamshughulikia,lakini Sasa naweza kupata penzi lako?"


"lakini sio Leo mwenye kiti sababu nipo kwenye siku zangu naomba nivumilie kidogo"




"ooh kumbee sawa Binti ukiwa tayari utaniambia maana Nina hamu saña ya kuwa nawewe faragha maana Kila nikikutazama yaani napandwa na hisia saña angalia kwanza mtoto una kiuno kizuri macho yako yanavutia saña urembo wako rangi yako ndo umezidi kuniteka mwenzio"




"basi mwenyekiti inatosha Wacha nirudi nyumbani Sasa"




mwenye kiti alimruhuau Aisha alirudi nyumbani kwao lakini moyoni alikua anawaza saña jinsi ya kumuepuka mwenye kiti huyo maana tayari ameshaanza mazowea n kijinga kwake na ukizingatia ye na Suma tayari wamekula kiapo cha kutoslitiana Maisha Yao yote.




alipofika nyumbani kwao aliondoa sura ya huzuni na kuiweka sura ya furaha Ili mama yake na Suma asigundue chochote haraka alimsalimia Kisha akamwambia


"mama Suma alinipigia wakati naenda shambani amefurahi saña hata Mimi nimefurahi kuongea nae na pia alisema anataka kuongea na wewe"




mama yake pia baada ya kuskia hivyo alifurahi saña na kumwambia


"mpigie nimeshammisi mwanangu jamani"




Aisha alitafuta Ile namba ambayo ilimpigia lakini alipokea mwanamke na kumwambia kua hakuna mtu yoyote ambae alimpigia kifupi aliwajibu vibaya saña kiasi kwamba Aisha alihisi huenda Suma amepata mwanamke mama yake akamwambia




"Aisha usijari labda Suma aliazima tu simu Kwa mtu usimfikilie vibaya najua umejitahidi saña kumuelezea lakini amekua mgumu kuelewa najua na Nina imaani kua Suma atapiga Tena.




upande wa dar Suma alikua kuchukuliwa na kijana wa boxa boda na kjpelekwa aehemu ambayo aliagizwa na baada ya kufika akamwambia


"dog hapa ndipo utakapokua unafanya kazi changamka usiwe na unyonge ikija gari msaidiane Ili mpate pesa sawa"




"Asante saña kaka"


"poa badae basi"


yule jamaa aliondoka na kumwachia Suma akiwa na wenzake wanapiga story.


Kwa muda mfupi tu suma alikubalika Kwa story zake na Kwa muonekano tu alionekana kua na mipango na akili nyingi saña.




Moja akamwambia


"kwahiyo Suma we mtu wawpi?"


"Mimi mtu wa tabora na nimetoka huko nyumbani nimeacha mama na mwanamke ambae ananipenda saña"




wenzake wakamtazama na mmoja akasema


"we ndo hujielewi yani Kwa sifa ulizotoa kuhusu mwanamke wako huwezi kumkuta kama ulivyomuacha broo yaani hapo ukipata demu wa huku pita nae usawazishe mana uwezi kubaki na ugumu simu zite eti Hadi upate pesa ya watu wako kuja mjini wakati huku mademu wapo wengi tu,ona sisi tupo hapa mwaka wapili Sasa lakini hatuna chochote mpaka sasahiv afu wewe unakuja kutuletea umama hapa"




"sikia ndugu zangu Mimi nimekuja mjini Kwa malengo maalum na sijakurupuka na Kila nitakachokipata tayari ninampango nacho kama mmekuja kwaajiri ya wanawake sjui manini me sipo hivyo"




wakati wanaendelea kupiga story ilifika gari Moja nzuri saña wote walisogea karibu kutaka kuiwahi kuiosha lakini mlango wa gari ulifunguliwa na kushuka mwanamke mwenye shape nzuri saña amependeza saña saña urembo wake shepu yake vilibebwa na rangi yake pia,alifunga mlango wa gari na kuzungumza




"washkaji zangu nani alinioshea gari yangu maana Sina kawaida ya kuosha gari Kila siku lakini ona Leo nimekuja Tena"




Kila mtu alikua anajikataa yule mdada kasema


"yule mbona kajitenga ni mwenzenu au?"


"ndio boss ni mwenzenu lakini mgeni hajazoea mazingira na ndio kwanza kafika Leo"


"anhaa ohk anaitwa nani?"


"sumaa njoo hapa"


mmoja akamuita Suma alismama na kupiga hatua Hadi pale yule mwanamke akampa mkono Kwa kumsalimia


"habari yako Suma?"


"safi tu karibu"


"Asante mbona uko umekaa kule wakati wenzio wanachangamka?"


"aah nilikua nasubiri muelewane ndo nije kusaidia"


"anhaa ohk sasa washkaji sikia Leo nipo mwenyewe hapa siondoki na gari yangu namkabidhi Suma alioshe akinizingua kama mlivyozingua Jana nitaondoka na sitarudi Tena kuosha gari hapa"


"hapana madam boss usiseme hivyo"


"Sawa basi Suma fanya hivyo"


Kisha akatoa pochi na kuwapa hela ya chakula Kisha akaingia kwenye gari na kuwaacha mziki Kisha akasogea kivulini kwaajiri ya kusubiri gari yake.




Suma alijitahidi saña kuiosha gari Kwa umakini saña Kisha akasogea Kwa huyo mdada na kumwambia


"madam boss gari Iko tayari"


huyo mwanamke alismama na kusogea karibu na gari na baada ya kuchunguza akaona utofauti mkubwa saña akampatia elfu20 Kisha akamwambia


"hii pes ya kwako usimuoneshe mtu yoyote na hii elfu 20 mtagawana elfu5 Kila mtu"


"Asante saña"




Suma alisigea Kwa wenzake na kuwapa Kila mmoja Tano Tano lake madam boss wao aliondoka na kuwaacha wakiendelea na story zao juma akamuhuliza Suma


"kwahiyo unaweza kutuambia huyo mwanamke ulivyompata maana umesema wewe ni Domo zege mbele ya msichana huyo mwanamke ulimpataje?"




"nistory ndefu saña ila wacha nifupishe tu ilikua hivi Mimi na mama yangu tulilikua tunarudi shambani manira ya sa11 jioni sasa tulifika aehemu Moja hivi ya msituni kulikua kunawaka moto alafu pia kulikua na sauti ikisikika kuomba msaada na niliposogea nikasimia kabisa inaomba msaada sana lakini watu waliokuwepo Hadi mwenye kiti alikua anasua kutoa msaada basi nikamuomba mama anipe baraka zake na bila ya kuchelewa nikazama msituni moto ukiwa mkali sana lakini sikujali chochote nikamkuta huyo mwanamke amefungwa kamba Tena akiwa na midamu mingi kutokana na kipogoa nikamfungua na kumbeba na kutoka nae ukweli nilikua nimechoka sana kutokana na kukosa kupumua vizuri kutokana na Moshi lakini yule dada tayari alishazimia sababu ya kuwa ndani ya moto Kwa muda kidogo basi nikamlaza chini watu wakiwa wamenijalia pale na Kwa bahati hua tukitoka shambani tunalitia mtoni kubeba Maji hivyo nilichukua ndoo ya Maji na kujimwagia Mimi na yule msichana Ili joto lipungue mwlili mwake pia na Mungu alitusaidia na muda mchache tu aliweza.kuamka.




na mwenye kiti akamkabidhi Mimi yule mwanamke huku akiisema kua atafanya uchunguzi ajue chanzo cha msichana huyo kuwepo pale.




basi niliondoka na yule dada Hadi nyumbani nikaanza kumuhudumia Kwa dawa na Kila kiti na baada ya kumuhulizia juu ya kilichotokea akanisimulia Kila kitu na kuomba kuishi pale na sisi mama hakupinga na Mimi pia sikua na sababu ya kukataa.




basi baada ya siku chache nikaona mabadiriko maana msichana yule alianza kunishika shemu tofauti za mwili wangu na mwisho akaniambia kua ananipenda na vile sikua na mahusiano na wasichana wa pale kijinini basi ikawa fursa kwangu ukweli tulikua na furaha sana hasa baada ya kuweka huru mapenzi yetu wengi waliona wivu sababu nikianza kutakaka Kwa penzi lake moto.


na yeye ndio alienishauri nije kumtafuta Maisha huku kwaajiri ya Maisha yetu ya baadae"


juma akasema


"nyie huyu Suma anainekana ni muongo sana hivi nyie hii movie hamjawahi kuiona kabisa?"


wote walicheka Kisha mwingine akasema


"juma sio Kila kitu ni movie mbina yanatokea hàyo mambo?"


"aah ramso sio Kwa Suma bwana huyu bwana anaonekana kabisa ni muongo"




Suma akamwambia


"kama unahisi ni uongo sawa lakini siku Moja utakuja kuamini kile nachokuambia"


Suma alismama na kuwaambia


"muda umeenda Wacha niondoke"


"kwahiyo Suma unaondoka sa12 hii wakati muda Bado kabisa Kuna magari ambayo hujaga usiku wewe"


"hapana Kwa Leo nimepata hii oes itanisaidia Kwa kesho Wacha tu niende"


Suma aliondoka eneo like na baada ya kufika mbele kidogo akasogea kibandani na kuomba kupiga simu aliweka namba na kupiga simu Kisha wakaongea sana na vipenzi vyake na Kisha akawatumia Ile elfu 20 Kisha akaagana nao.


kutoka hapo Hadi sehemu aliyosaidiwa ni mbli sana na ilikua usiku wa SAA Moja Suma hakuweza kutambua njia Ili apite Ili aweze kufika kwenye huyo nyumba ukweli ilikua inamchanganya saña akaamua tu kurudi ambapo ametoka na kabla hajafika popote wahini walimvamia na kumpole elfu5 ambayo alibakiwa nayo siku hivyo ilikua ya uchungu sana kwake lakini akajisemea


"Asante Mungu sababu Nina furaha kua nilichokipanga Kwa familia yangu nimetimiza na pesa iliyobakia nimeibiwa sawa lakini Mimi mwanaume nitavumilia tu na mengine yataendelea...


Suma alipiga hatua kurudi pale wanapooshea magari na kutafuta sehemu nzuri na kujihifadhi.


usikose itaendelea....


 yajayo yanafurahisha


PENZI LANGU 03

Usiku mzima Kwa upande wa Suma ulikua wa mateso kwasababu ya baridi kali sana na mbu walimshambulia sana Hadi inafika asubuhi.




Kwa upande wa yule jamaa ambae alimsaidia alipoamka asubuhi akawa anajiandaa kwaajir ya kuelekea kazini alivyotoka sebleni hakumuona Suma akamuhulizia mkewake


"inamaana yule dogo hajarudi Jana?"


"haha me nimesubiri sana arudi lakini sijamuona"


"mmh nawasiwasi sana kuhusu yeye na hij inawezekanaje?"


"hata me sielewi mumewangu"


"Sawa Wacha nijaribu kupitia pale nilipompeleka kwanza nitakupa taarifa"




basi waliagana na mkewake na kisha kuondoka zake.




alipofika kwenye eneo husika alimuona mtu kwa mbali akiwa amelala na ilikua muda ya sa12 asubuhi,alishuka kwenye gari na kumpiga hatua Hadi pale na kumuhuliza




"we Suma mbona umelala hapa shida Nini?"


"aah kaka za asubuhi?"


"nataka kujua mbona umelala hapa wakati nimekukaribisha kwangu au mkewangu amekuambia kitu Chochote kibayaa?"


"hapana kaka ila tu nilipotea na sikujua wapi Kwa kuingilia na pia Sina simu nikaamua nirudi kulala hapa maana hata wenzangu sikuwakuta"


"dah pole sana dogo vipi utafanya kazi au utaelekea kupumzika maana hapo ulipolala sidhani kama utakua Sawa kutwa ya Leo"




"usijali kaka Mimi nipo Sawa kabisa nitafanya kazi"


"poa basi jioni nitakupigia turudi nyumbani wote"


"asante kaka"




yule jamaa aliondoka na kumwacha Suma akiwa Bado kile kibaridi kinamtetemesha kidogo, alisogea kwenye benchi na kukata Huku akiwaza sana mbele yake itakuaje na tayari amewakumbuka sana mama yake na Aisha mpenzi wake.




mara juma na rama walifika na kumsalimia Suma aliitikia na kuwakaribisha na story iliwasigundue Chochote kuhusu yeye aliogopa kuchekwa,na hawakusubiria sana mara mwenzao mwingine alifika na kuendelea kupiga story.




upande wa kijijini kwao taarifa za vijana watatu kuchomwa moto ilifika kituo Cha polisi na Baada ya kuhoji chanzo Aisha yeye alikua msemaji hivyo akaona ni fursa ya kumuweka mbali mwenye Kiti hivyo alielezea Kila alichokiona Hadi sababu kuu ya kufanya hivyo na mwenye Kiti alifungwa Kwa kosa la kujichukulia sheria mkononi maana hai vijana hawakupaswa kufa ila walipaswa kuolewa adhabu Ili wajifunze na kupewa nafasi ya pili lakini yeye hakutaka kuwaonya Wala kuwapa nafasi hivyo Kwa ushahidi tosha wa Aisha ulimfanya mwenye Kiti kuvuliwa cheo chake na kutumikia kifungo Kwa kosa la mauwaji.




mama yake Suma akamuhuliza


"Aisha mbona hukuwahi kuniambia kuhusu tatizo hilo huoni ni jambo kubwa na umenificha muda wote huo?"




"mama kumbuka haupo Sawa kiafya lakini pia najua kuwa ningekua nakuambia Kila kibaya nachopitia ningekua nakichosha Kwa mawazo mengi Huku uniwaze Suma Huku uniwaze mimi ukweli sikutaka uwe kwenye wakati mgumu mama"




"lakini Aisha...!!"


"mama usijali Mimi ni mtu mzima naweza kujimudu na isitoshe Kuna jambo nataka kukwambia nahisi utakubaliana na mimi"




"jambo Gani Tena mara hii tu tayari ushataka kunibadirishia mada?"




"hapana mama sio hivyo lakini nataka tu kukushirikisha,siwezi fanya maamzi bila kukuambia wewe"




"Sawa mwanangu niambie tu Wala hata usijali"


"mama nimeona kuwa Sasa ni muda sahihi wa Mimi kurudi mjini mama Tena sio mimi tu na wewe pia siwezi kukuacha hapa"




"unamaanisha nini,na unataka kwenda kufanya Nini wakati ulisema kuwa unawindwa?"




"nikweli mama lakini nimeongea na mwanasheria wa baba amenipa taarifa kuwa wote wakifanya kitendo cha kikatili Kwa wazazi wangu pia walifanya kwenye familia nyingine pia hivyo walishashtukiwa na Sasa wapo kwenye mikono ya sheria"




"Mimi naogopa sana kwenda huko mjini Aisha bora niishi hapa Kwa amani kama ilivyokua unasemaga mwanzo mwenyewe"




"nikweli mama na ninajua fika kuwa adui huwa wengi sana lakini sioni sababu Tena ya kujificha sababu Sasa hivi Nina nguvu kutokana na Nina family ambayo inanipenda sana"




"hapana Aisha siwezi kwenda naogopa kufa kabla ya kuona mjukuu wangu na nyie mkiwa kwenye sura mpya ya ndoa"




Aisha aliendelea kumbembeleza mama yake Suma Ili waende mjini lakini Bado mama yake na Suma hakua mlahisi kihivyo hivyo ikabidi amuache afikilie na akiwa tayari atamwambia lakini Aisha tayari akili yake ilishakumbuka mjini na kutamani kuyaona makaburi ya wazazi wake.




upande wa mjini siku nzima walifanya kazi kama kawaida Yao lakini Suma hakua vizuri Kuna hali flani ambayo alikua anajihisi Kwa muda lakini inakuja na kupotea kitu ambacho juma kilimfanya amuhulize




"vipi mzee wa bongo movie uko Sawa kweli?"


"hii juma inamaana ushampa jina mwenzio?"


"rama we huoni kama Suma ni muongo sana?"


"aah we juma ukianza kubishana humalizi ngoja tu niendelee na kazi yangu"




rama aliwaacha kisha juma akamuhuliza Tena juma na safari hii hakua ameleta Tena utani


"Suma Naina kama haupo Sawa Leo unatatizo Gani?"


"aah juma siko Sawa kabisa Yani ila naamini kua nitakua Sawa"


"pole sana kijana utakua Sawa"


basi walisaidiana kufanya kazi zao maana siku hiyo ilikua ya neema sana kwa upande wao maana magari yalikua yanasubiria foreni ya kuoshwa hivyo wote walifanya kazi kwa kujituma na bidii ya Hali ya juu sana.




mpaka inatimu jioni wote walikua wamechoka sana na kabla hawajao pumzika vizuri ilikua jgari nyingine kwaajir ya kutaka kuoshwa pia Suma akawambia


"kama mmechoka Wacha Mimi nioshe kisha tuondoka au mnaonaje?"


"Suma bwana Wacha iende tu hiyo gari maana kama unataka kuiosha Sawa ila sisi tunaondoka"


wale watatu wakaondoka na kumwacha Suma pekee Suma alianza kuliosha like gari Huku akisubiri kuja kufatwa na kaka yake hadi anamalizia kusafisha gari Bado kaka yake alikua hajafika




Suma alikua anatamani sana kwenda kupiga simu kinadhani ila alihisi akitoka tu pale ataibiwa hivyo alikua mtulivu sana paleoale Hadi inafika sambili usiku Bado huyo kaka yake hajafika.




ukweli ilikua inamuumiza sana kuzidi kuwaza kwanza mitaa haijui na simu Hana alikua na subra palepale.




mara Ghafla ilipita gari Kwa Kasi lakini Ghafla ilirudi na kupiga honi Suma aligeuka na kuhisi kua huenda ni kaka yake hivyo alisogea haraka eneo liliposimama gari lakini alipofika akamuona mwanamke akamsalimia vizuri yule mwanamke akashuka kwenye gari na kumuhulza


"nafikiri kama sijakosea wewe ni suma?"


"aah ndio ni Mimi umejuaje gari yangu?"


yule mwanamke alitoa miwani na kumwambia


"nilikuja Jana ukanioshea gari yangu"


"ooh madam boss..!!,sikuweza kutambua kama ni wewe kutokana na gari hii sio Ile ambayo umekuja nayo Jana"


"ndio lakini Mimi naitwa Nadya sio madam boss sababu hilo jina Hawa vijana ndio hupenda kuniita ila sio jina langu"


"anhaa sawa pia ni vizuri sababu kwanza linakupendeza sana"


"anhaa Asante pia lakini mbona uko mwenyewe wenzako wameenda wapi?"


"wao wameondoka lakini Mimi...."


"Suma haupo na sehemu ya kuishi sindio?"




Suma kama vile alipatwa na kigugumizi flani 


"aah mi,ni ...aah"


"Suma usijali sawa ingia kwenye gari twende"


Suma aliangaza Huku na huko kisha akapanda kwenye gari ya nadya kisha Nadya aliwasha mziki na kuondoka maeneo yale Hadi nyumbani kwake.




Baada ya kufika nyumbani kwa Nadya Suma hakuacha kushangazwa na uzuri wa nyumba ambayo anaishi nadya na magari yalivyojipanga kwenye parking utafikilia kua ni ya watu au wafanyakazi wa kampuni husika,Suma akishindwa kuvumilia akamuhuliza


"inamaana Kila kitu unamiliki wewe madam boss?"


Nadya alimgeukia Suma na kumshika mabegani na kumwambia


"naitwa Nadya sitaki hilo jina,hata twende ndani"




Suma ilimbidi afunge Domo lake Huku aliendelea kushangazwa na uzuri wa bustani na mazingira ya Ile nyumba.




upande wa yule jamaa alirudi nyumbani kwake na kusahau kabisa kua aliagana na Suma kuwa ataenda kumfata.




alifika alioga maji Akala chakula na kuingiza kulala mkewake akamuhuliza


"mumewangu Leo ni siku ya pili shemeji Suma hajarudi lakini kwanini?"




"aah nimeshachoka Mimi pesa anapata anashindwa kujiongeza kuchukua boda boda hadi hapa nimechoka kumfikia bwana yule hanihusu Kwa Chochote kama anashindwa kujiongeza basi bwana Leo ndio mwisho wangu na kama hatirudi Tena itabidi tu nguo zake zichomwe moto kabisa"




"mumewangu sio vizuri lakini"


"ndio hivyo mwanaume gani unakaa nyua nyumba kama mifuko ya suruali achana nae na ulale sitaki kelele mimi hapa"




basi yule mwanamke aliamua kutulia na kuheuka upande wa pili na kulala.




humu Kwa Suma mambo ni moto maana nadaya aliandaa chakula kizuri Kwa haraka na kumkaribsha Suma mezani ,japikua alikua na kauoga flani lakini Nadya akamwambia


"kuwa huru humu ndani Niko mwenyewe tu usiwe na wasiwasi"


Suma japokua alitolewa wasiwasi lakini hakuweza kumuamin Nadya bado alijisemea mwenyewe kua wasiwasi ndio akili.




wakati wanaendelea kula chakula mara mlango uligongwa Kwa nguvu sana nadya aliaotwa na wasiwasi sana sababu tangu aanze kuishi hapo hakuwahi kugongewa mlango usiku Tena kwanguvu hivyo na hali ya wasiwasi wa nadya ilimshtua Hadi Suma pia ikabidi pia aache kula na kujificha jikoni,Nadya alipiga hatua Hadi mlangoni na kugusa kitasa Cha mlango Kwa kusita sana na kufungua mlango ....


usikose itaeendelea....




Previous Post Next Post

نموذج الاتصال