MSALA Sehemu Ya Tisa-09
MSALA Sehemu Ya Tisa-09 |
MSALA
Ilipoishia “Mkuu tunafyeka wote kisha kikosi kazi nacho kinafyekwa na kikosi maalum” alisema Balozi, haraka Rais bila kujiuliza mara mbili alinyanyua simu yake na kumpigia IGP Hassan Kitulo aondoke Kijijini hapo haraka sana Halafu akanyanyua simu kwenda kikosi fulani kwa ajili ya kufyeka kijiji kizima wakati huo huo alipiga simu ya dharura kule BLACK SITE na kuagiza Makomandoo kwa ajili ya kufyeka kikosi maalum ambacho kitafyeka Kijiji kizima.
Endelea
SEHEMU YA TISA
Nilipigwa, niliteswa na wale wanaume walioficha sura zao huku wakinitaka niseme Elizabeth yupo wapi, jambo moja lililonifikirisha ni Namna ambavyo walinitaka niseme najua nini kuhusu M21, Kiukweli kitu hicho nilikua sikijui
Nilizidi kupigwa na zile Nyanya nikiwa nina ning’inia pale juu ya ule mnyororo, walipofikiria nawaficha walinikata kidole kimoja cha Mguu, maumivu yake yalikua zaidi ya ile risasi iliyopenya mguuni, nilipiga yowe kali sana. Damu zilinivuja kisha waliniacha hapo nikiwa nimechoka vibaya sana.
Mara alifika yule Mwanamke aliyekua akinihoji muda wote kisha akafuatiwa na Mwanaume mmoja aliyeficha sura yake akiwa ameambatana na Mpenzi wangu Suzan wa Arusha, nilishtuka sana waliwezaje kumjua hadi mpenzi wangu, hapo ndipo nilipogundua kua Watu hao hawakua na mzaha kwenye jambo hili na ilionekana kua ni jambo zito mno, haraka nilijiuliza ‘Elizabeth ni Nani?!!”
Walinishusha kutoka juu ya Mnyororo, mwili wote ulitota kwa maumivu makali, alama za nyaya ile zilikua pote mwilini, damu ya kukatwa kidole ilikua sakafuni. Udenda ulikua ukinitoka huku macho yangu yakiwa yamelegea kwa uchovu
Suzan naye alikua amepigwa vya kutosha, wale Watu walitulazimisha tuseme ilipo M21
“Mtatupiga na kututesa lakini hakuna jibu nitakalo wapa zaidi ya kusema simjui yule Msichana” nilisema, moyoni nilipasuka kwa maumivu ya kuteswa kwa Mwanamke niliyempenda, tena aliteseka kwa jambo ambalo alikua halifahamu kabisa.
“Benjamin, ni kitu gani hicho, huyo Msichana ni Nani waambie basi” alisema Susan akiwa na mpasuko kwenye mdomo wake.
“Hakika sijui kitu Mpenzi wangu Suzan, tunateswa bure. Nilimsaidia yule Msichana lakini simfahamu” nilizidi kuusema ukweli ulio ndani ya Mkasa ule lakini hakuna aliyenielewa, tulitenganishwa kila mmoja aliingizwa kwenye chumba cha Mateso.
**
Sauti za Magari zilisikika huko nje, magari ya vikosi vya Polisi na kikosi maaalum kutoka Ikulu yalianza kuondoka Kijijini Mwambisi, Elizabeth pamoja na yule ambaye alijitambulisha kwa Elizabeth kama Mzee Kimaro walishangaa kwa Pamoja, haraka Mzee Kimaro akaenda kuchungulia
“Ndiyo, wanaondoka” alisema Mzee Kimaro mwenye nywele nyingi nyeupe zilizo shamiri mvi, Elizabeth akasogea Mlangoni na kuona kweli Magari yalikua yanaondoka.
“Ondoa familia yako hapa Kijijini, Rais hawezi kushindwa kwenye hili. Upo mpango” alisema Elizabeth kisha haraka alirejea kwenye lile sanduku
“Msaidie Mama kuondoka hapa Kijijini haraka sana” alisema Elizabeth akimwambia Binti wa Mzee Kimaro, ni kama alishashtuka kua pengine Rais alikua na mpango mzito dhidi ya Kijiji kizima. Elizabeth akamtupia Bunduki Mzee Kimaro, akaonesha umahiri wake wa kuiunga na kuiweka sawa ndani ya sekunde kadhaa tu, Elizabeth akakubali kua Mzee huyo alikua ni Askari Mstaafu wa jeshi.
“Changamka” aling’aka Elizabeth akiwa na M2 Carabaine Mkononi, namna alivyojitanda isingelikua rahisi kujulikana kua Msichana anayesakwa na Vikosi vya Polisi alikua ni yeye, kitu kilichotakiwa kwake ilikua ni Flashi aliyoisweka ndani ya Chupi yake kwenye zipu ndogo, ndani ya kichwa chake alijua fika kua endapo atafika Picha ya ndege atakua amepata Msaada kutoka kwa Mtu wake aliyewasiliana naye kwa njia ya simu.
Haraka yule Msichana alimtoa Mama yake nje ya Kijiji akiutumia Mlima mdogo ulio kando ya Kijiji hicho cha Mwambisi. Halafu nyuma yao walitoka Mzee Kimaro akiwa ameificha Bunduki ndani ya Kiroba, mbele yake alikuwepo Elizabeth aliyeificha Bunduki ndani ya gauni alilolivaa
Kijiji kilikua kimya mithiri ya Maji mtungini, hapakua na sauti yoyote iliyogonga ngoma zao za Masikio, hata sauti ya Mbuzi na kuku haikupata kusikika hivyo umakini kwao lilikua ni jambo la kwanza
Lahaula!!
Sauti tata ilisikika nyuma ya Mzee Kimaro, sauti iliyomgutua zaidi ilikuwa ikitoka kwa Polisi mmoja mwenye silaha Mkononi, alikua ni miongoni mwa Askari walioachwa na IGP Hassan Kitulo kama Mtego wakati alipopokea simu ya dharura ya Rais Mbelwa.
Elizabeth alipiga hatua mbili kabla naye kusimama kwa tahadhari kubwa
“Mikono juu” alisema Polisi huyo mmoja aliyesimama nyuma yao, Mzee Kimaro akazidi kutepeta kwa woga huku akianza kutetemeka kwa hofu iliyomnyong’onyeza haraka mno, alitetemeka hadi alitaka kuachia kiroba chenye silaha chini.
Yule Polisi alizidi kumsogelea Mzee Kimaro aliyempa Mgongo, Elizabeth akagundua kwa haraka kua endapo watatumia muda mrefu kusimama hapo basi ipo hatari ya kukutwa na askari wengine walioachwa hapo Kijijini, Bunduki yake aliyoificha aliipapasa kama anaifuta vumbi huku akiiweka vyema kutaka kukabiliana na Kidudu Mtu.
Wote walimpa Mgongo Askari huyo mwenye sare za jeshi la Polisi, hali ya ukimya iliendelea kuwazingira kutoka kila kona. Mapigo ya moyo ya Mzee Kimaro yalikimbia kama saa mbovu huku yule Polisi akiwa tayari amemfikia, kwanza alikiona kitako cha Bunduki kwenye Kiroba, haraka akapiga filimbi ya kuita Polisi wenzake, pale pale bila kupoteza sekunde
Elizabeth aliichomoa Bunduki na kumimina risasi sita mfulilizo zilizotua kwenye kifua cha yule Polisi, zilimkatisha uhai papo hapo, taharuki ikaanza Kijijini Mwambisi, mara moja hali ya tahadhari ilianza Kijijini hapo huku kundi la Askari Polisi likizidi kuongezeka
Hapakutokeka tena, walitafuta maficho kando ya Zizi la Nguruwe na kujificha ndani ya Zizi hilo lililozingirwa na Mapipa yenye chakula cha nguruwe, kifo cha yule Polisi kilichochea hali ya kumsaka Elizabeth, haraka simu zilipigwa kwenda kwa IGP, naye akaisambaza taarifa kwa Rais aliyekua ofisini na washirika wake
Zikatumwa Helkopta mbili zenye uwezo wa kukisambaratisha Kijini chote bila kujali kama kulikua na WanaKijiji wasio na hatia, alichotaka Rais Mbelwa ni kutaka kuficha siri iliyobebwa na Elizabeth ndani ya Flashi
Helkopta hizo zilitoka mahali ilipo Kambi ya Kijeshi ya wanajeshi wa anga, zilianza safari ya kuelekea Mwambisi haraka sana. Wakati Helkopta hizo zinaelekea Mwambisi tayari kikosi kingine kilitumwa na Rais kuhakikisha hakuna ushahidi utakaoachwa, yaani alitaka hadi hizo Helkopta ziteketekee, kikosi cha Pili kilitoka Black Site
Mzee Kimaro aliitoa Bunduki ndani ya Kiroba kwa ajili ya kujibu Mashambulizi, Elizabeth alizijua mbinu nyingi za Kijeshi kitu ambacho kilimshanga Mzee Kimaro, alifyatua risasi kwa mahesabu na hakuruhusu risasi yake ipotelee hewani.
Wanakijiji walianza kukimbia kwa fujo, Askari wakajikuta wakianza kuwashambulia na kuwauwa bila kujua mahali alipo Elizabeth, wakachomoka ndani ya zizi ili kukikimbia Kijiji ambacho kilijaa taharuki ya kutosha.
Helkopta ilikua ya kwanza kukatisha Kijijini hapo, dakika tano baadaye zilikuja Helkopta za kivita kwa ajili ya kukitekezeka Kijiji chote, Elizabeth akamtaka Mzee Kimaro akimbilie Mlimani mahali ambapo pangekua salama kwake
Mabomu mazito yalianza kutupwa ndani ya Kijiji cha Mwambisi, moto ulifuka, kijiji kilizizima ndani ya dakika moja tu, hapakuonekana hata nyumba moja wala Mtu akikimbia, Helkopta mbili za Kivita zilisimama juu ya anga la Kijiji huku wakiangalia kwa makini kama kuna kilichosalia
Miili ya Wanakijiji ilisambaa kila kona ya Kijiji, haikuchukua hata dakika mbili zile Helkopta zilianza kudunguliwa moja baada ya nyingine, pakawa kimya kabisa, halafu sauti ya Helkopta ikasikika ikipaa na kukatisha juu ya Kijiji ikatokomea kusikojulikana baada ya kufuta Ushahidi.
Elizabeth alikua amefukiwa na mchanga. Tukio zima la Kijiji kuteketea lilikua mikononi mwa Rais Mbelwa aliyekalia kiti cha Ikulu akiwa na washirika wake ambao walikua na uhakika kua walimmaliza kirusi aliyewasumbua.
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya Kumi ya MSALA hapa KIJIWENI