PENZI LANGU 04 - 6
Nadya Baada ya kufungua mlango akakutana na mzee akamsalimia na kumwambia
"mzee kigo umenishtua sana kwakweli kaka unavyojua naishi mwenyewe humu ndani alafu ulivyogonga huo mlango nimeogopa Sana"
"aah samahani mjukuu wangu lakini Kuna muda uliniambia nije ila sijakukuta nilikuja kukwambia kua tayari kazi ulinipa nimemaliza na hiyo hela nilikua nahitaji Kwa haraka sana"
"ooh Sawa babu ngoja nikupatie ,kweli ndio nimerudi muda mfupi tu Leo nilikua na kazi nyingi sana"
"napenda mabinti wanaojituma kama wewe lakini kwanini unaishi pekee kwenye hii nyumba"
"usijali babu hivi karibuni nitaanza kuishi na mtu usijali"
"anha nilijua hakuna kabisa nilitaka kuja kuhamia"
Nadya alicheka sana Huku akifunga mlango na kuanza kumuita Suma
"Suma..! Suma...!,uko wapi em njoo bwana"
Suma alitoka alipokua amejificha Nadya alicheka sana na kumwambia inamaana kama kingenitokea kitu kibaya wakati mwanaume upo ndani kweli Suma?"
"hapana madam boss unajua...."
"Suma ukitaka kunikwaza niite Tena hilo jina"
"Sawa samahani lakini nimeshazoea,ila tuachane na hayo lazima nijirinde sababu jinsi ulivyo alafu unasema nyumba yote hii uko peke Yako huwezi kuamini hivyo nikajua Moja Kwa Moja nimefumaniwa nikaamua kujificha kujiokoa"
"Suma Sina mume Wala mpenzi nimeamua kufokasi kwenye kazi kuliko mapenzi na Kila napojaribu naona mauzauza tu ndiomaana nikaamua kuwa hivi"
"Sawa bwana hongera"
"Asante kwahiyo utakula Tena au niondoe vyombo?"
"aah hapana nimeshahisi nimeshiba tayari"
"basi Sawa Kaa pale ungalie movie"
Suma alikaa kwenye sofa wakati huo Nadya anaondoa vyombo mezani kisha akaingia chumbani kwake akaoga maji na safari hii alivaa khanga nyepesi kabisa tofauti na mwanzo alioga na kuvaa tenge na tisheti lakini Baada ya kula alioga Tena na kuvaa khanga nyepesi na kutokea sebleni wakati huo Suma alioga na vuaa Tena nguo zake zilezile.
Nadya alivyotoka chumbani akaja kukaa kwenye sofa karibu na Suma,Suma alikua bize kuangalia movie hakumtazama kabisa Nadya na hakuweza kujua Nini amevaa alikua mshamba wa TV hakuwahi kuangalia tv Kwa uhuru tangu azaliwe.
nadya alivyoona Suma hamjali Yuko bize akamshika kifuani kwake na kumwambia
"Suma muda umeenda twende basi ukalale"
"aah hapana Wacha tu nitalala hapahapa usijali"
"Suma naogopa kulala pekeangu bwana"
Suma alivyoskia sauti ya madeko kutoka kwa Nadya ikabidi Sasa amtazame Nadya kwanini kazungumza hivyo.alivyotupa jicho akamuona Nadya mwili wake ,na hasa pale jinsi alivyokaa na kile kikanga kifupi hivyoasilimia ya mapaja yake yalikua nnje Suma akishindwa hata kupepesa macho Kwa kuyatamani maungo ya nadya na alipopandisha macho yake juu akakutana na chuchu zikiwa zimesimama ipasavyo Suma akajihusi msisimko wa ajabu sana na nadya alimgundua mapema sana Suma wa jinsia livyoonekana.
mara Ghafla kwenye ile movie ikasikika mripuko flani hivi ambao ulimfanya Nadya ajisogeze Kwa karibu zaidina Suma na kumkumbatia Kwa kungu Huku akiigiza kua anaogopa,Suma akishindwa kumtoa kwasababu tayari mambo yalishamuwea magumu kwake.
Nadya alijisogeza zaidi na kumkalia Suma mapajani kwake na kuchua rimoti na kuzima tv Kisha akaanza kumchezea vindevu ambavyo vilikua vimeota vibaya sababu ya kukosa pesa yaani Kuna ndevu za kimaskini na ndevu za kitajiri,afu Kuna ndevu za kukosa hela😁😁au basi...
Nadya alianza kucheza na ndevu za Suma mara aguse kifuani kwake Huku akicheza na mwili wake Suma wakati huo pia Suma hakua nyuma na yeye alikua anampapasa mgongoni kwake Hadi kwenye kiuno chake na kurudi juu mpaka pale walipoona tayari mambo Yako moto.
nashughuli ilianzia sebleni na kwenda kumalizika chumbani,hapo kila mmoja alikua hoi sana na haikuchukua mda mrefu Kila mmoja alipitia na usingizi.
upande wa kijijini pia mama yake na Suma alikua hazungumzi na Aisha kutokana nayale mambo ya kumwambia kuwa waende mjini lakini Kwa siku hiyo Aisha nae aliamua kuwa mbali kidogo na mama yake suma maana hakutaka kumkwaza Tena.
mama yake Suma akamuita
"Aisha kipenzi nisamehe sana kwa kile kilichotokea najua nawewe nimekufanya uwe mwenye mawazo lakini yote kutokana na uoga wangu,lakini Sasa nimefanya maamzi yangu mwanangu"
"mama usijali kuhusu hilo sijajiskia vibaya lakini sikua nataka kukukwaza ndiomaana nilianza kukaa mbali ,na Nina shauku ya kutaka kujua umeamua kipi?"
"Aisha mwanangu nimekubali kuungana nawewe kuelekea mjini"
Aisha alifurahi sana na kumkumbatia mama yake Suma Kwa furaha sana kisha akamwambia
"Asante sana mama kwa kunikubalia ombi langu na Nina furaha isiokifani natamani hata nikupe zawadi kwaajir tu ya kukubali ombi langu"
"usijali hata Binti yangu najua umepitia kipi na sikua nataka kufanya ukose furaha kwa kitu ambacho umekipanga pia najua ukiwa unafuraha wewe hata na mimi nakua na furaha hata mwanangu Suma pia atakua na furaha sababu mioyo yenu tayari ipo karibu na inafanya mawasiliano sana"
"kweli mama na natamani hata angelikua na simu nikamueleza hili lakini hapana ninataka kumfanyia saplaizi au unasemaje mama?"
"ndio ni vizuri sana natamani pia atafurahishwa na safari yetu"
"basi saa mama sasahivi ni usiku pumzika kesho tutapanga vizuri kuhusu safari yetu"
mama Suma akilala akiwa anatabasamu Baada ya kumuona Aisha anafuraha sana.
Asubuh mapema Suma aliamka na kujikuta amemkumbatia nadya Tena wakiwa uchi kabisa akataka kujitoa kwenye lile kumbato lakini Nadya hakutaka kumuacha Suma ndio alizidi kumkumbatia Kwa ukaribu zaidi kitu ambacho kiliamsha hisia za Suma upya na kujikuta wanapata Tena na cha asubuh kisha Nadya aliamka kwaajir ya kujianda kwenda kazini.
akiwa bafuni anaoga Suma alikua mwenye kujilaumu sana kwa kile kilichotokea na nadya Baada ya kutoka bafuni akamkuta Suma hayupo Sawa akamuhuliza
"mbona upo hivyo Suma unanini?"
"Nadya kwanini umenipitisha kwenye majaribu kwanini uliamua kufanya hivyo?"
Nadya alimsogelea Suma Kwa ukaribu na kumwambia
"ni kwasababu Moja tu Suma kwanza kabisa nilitamani kuwa na mpenzi Kwa muda mrefu lakini sikua nae sababu sikua na hisia na mwanaume yoyote lakini we nilipokuona Kwa mara ya kwanza tu moyo wangu ukaripukwa na upendo nikawa nashindwa jinsi ya kuanza lakini nashukuru mungu kwa kunipa ujasiri huu nilioupata kwaajir yako pia nimeinjoy sana na penzi lako maana sijawahi kuinjoy mapenzi tangu nianze kutajua ila wewe ndio fundi wangu"
"unaongea ujinga sana nadya Mimi Nina mpenzi wangu HUKO kijijini ananitegemea kwanini umefanya nimsaliti kwaajir yako?"
"ooh mpenzi kijijini? unajuaje kama yeye anaweza kujikontroo usijipe donda la roho Suma huwezi jua yeye huko kijijini anafanya mangapi changamka wewe au mie sio mtamu eeh?"
Suma alichukia sana na maneno ya nadya akasimama na kutoka zake nnje Nadya alitabasam na kumwambia
"I love you Suma na hapa ndio umeshafika huwezi kuniacha labda nitake mie"
Nadya alichukua handbag yake na kutoka chumbani na kumkuta Suma amekaa alisogea na kum'busu kisha akamwambia
"naondoka Suma mpenzi jla sitachelewa kurudi ukiwa na njaa stoo chakula kipo kwenye friji pia Kuna mahitaji pika ule usikae na njaa na sitaki utoke humu ndani"
Nadya aliondoka zake,Suma alibaki akiwa amekaa anawaza anawezaje kuishi hapo kuendelea kumsaliti mpenzi wake Aisha ambae anaempenda sana kuliko kitu Chochote.
ukweli ilimuwea vigumu saña Kwa upande wake na alikua na mawazo sana sana.ikanidi ajiinue na kwenda kuoga Ili kuufanya mwili uweze kufikilia jambo la kufanya tofaut na mawazo ambayo alikua nayo.
upande wa Huku kibaruani kwake matafiki zake walifika na Kila mmoja kumuhuliza mwenzake kuhusu Suma lakini kila mmoja alisema waliondoka kivyao wakiwa wanaendelea kubishana mara ilifika gari na akateremka mwanaume ambae ni yule jamaa ambae alimletea Suma kufanya kazi hapo akawahuliza
"nyie mwenzenu yupo wapi?"
"kaka sisi hatujui hata Yuko wapi lakini Jana tulimuacha hapa akisema kuwa anakusubiria wewe"
"ndio nilimwambia anisubiri lakini nikapitiwa sikuja kumchukua na hata nyumbani hakuja pia na Sasa basi kama amepotea au yukowapi atajua mwenyewe sihitaji kujua na nimekuja na nguo zake kifupi simtaki Tena nyumbani kwangu"
"lakini broo yule kama mdogo wako kwanini umchukulie hasira wakati ni mgeni huwezi jua amekumbana na Nini huko alipo"
juma alizungumza na wote wakatikisa kichwa kua wamekubariana na alichozungumza lakini jibu la yule jamaa nikuwa
"akija mwambieni kua simuhitaji kwangu hivyo myajua wenyewe jinsi ya kumsaidia"
Kisha karusha kifuko Cha nguo za Suma kisha akondoka zake na wakati ameondoka mara kuna gari ilifika pale na waliposogelea gari hiyo wakamkuta Nadya ambae ndo hupenda kumuita madam boss walimsalimia kisha akawahuliza
"nimeona yule jamaa binge hapa alikua anawafokea kwani ndio boss wenu?"
"hapana yule bwana ndio aliemleta Suma hapa na anasema siku ya tatu hajalala kwake na ukiondoa siku Moja ambayo alimkuta kala hapa hapa"
"MMH kwahiyo hata nyie hamjui Suma yupo wapi?"
"ndio madam boss tupo hapa tunajihuliza wapi alipo maana Jana tulimuacha hapa akimsubir yule jamaa lakini anasema alipitiwa na hakuja kumchukua haya nani mwenye makosa na ukizingatia Suma ni mgeni?"
"anhaa poleni sana washkaji zangu badae nitapita kwaajir ya kujua Nini kinaendelea kama amepatikana au lah"
"Sawa boss Asante Kwa kutuunga mkono"
Nadya alitoa pesa na kuwapa washkaji zake wakapate chai kisha akondoka zake bila ya kuwambia kua Suma yupo kwake...
usikose itaendelea...
PENZI LANGU 05
Maisha ya Suma na nadya kwenye nyumba ya nadya yaliendelea na Suma hakua mnyonge Tena,kifupi alimtolea uvivu kabisa Kila anapohitaji Nadya Suma humpa kile anachohitaji Tena Kwa Kasi hasa.
kifupi Suma alishakubariana na Kila kitu kuhusu Nadya na kusahau kabisa kuhusu Aisha.
maisha yaliendelea hivyo na Suma alikua anafanya Kila kazi pale ndani kwa Nadya kiasi kwamba hata usiku Nadya alihitaji penzi la Suma ,Suma hua anakua amechoka saña japokua anampa anachohitaji lakini Nadya alikua haliziki kabisa.
upande wa kijijini pia Aisha na mama yake Suma walikua na furaha ya kujiandaa kwaajir ya kwenda mjini.
mama yake Suma akazungumza
"kwahiyo Aisha utakuaje kuhusu mashamba yetu na mazao ambayo tunayaacha na vipi kuhusu nyumba yangu na vitu vilivyomo ndani?"
"mama usijali kuhusu Chochote maana Kila kitu tayari nimeshaandaa sababu kwanza hapa nyumbani nimeongea na msichana ambae atajua anaishi pia kule shamba nimemuachia maagizo yote ambayo ni sahihi"
"kama ni hivyo sawa nimekuelewa kama ni hivyo Sasa tunaweza kwenda"
wakiwa wamekaa mama yake Suma akamuhuliza
"mbona hatuendi stendi?"
"mama hatutamuia gari la watu wote tutatumia gari binafsi"
kabla Aisha hajamaliza kunielekeza mara ilifika gari aina ya BMW kisha Aisha akamwambia
"gari hiyo hapo twende mama"
mama Suma aliamka na Aisha alimfungulia mlango wa nyuma na mama Suma akaingia kisha akachukua mabegi Yao na kuweka kwenye Buti kisha ye akaingia kwenye gari kisha safari ikaanza Huku wakipiga story za hapa na pale.
hasa Aisha alikua anamuhuliza huyo dereva kuhusu kulivyobadirika huko mjini,mama Suma alikua Hana Cha kuhuliza sababu hakua anajua Chochote kuhusu Jiji hilo hivyo alikua kimya tu.
ilikua siku ya jumamos Nadya akamwambia Suma
"Leo nahitaji kutoka na wewe mpenzi si tunatoka pamoja eeh?"
"aah Nadya mie siwezi kutoka"
"kwanini?"
"lakini...."
"Suma hakuna Cha lakini lazima tutoke kama wewe ni mpenzi wangu hivi hutaki marafiki zangu wakujue shemeji Yao?"
"aah sawa kama umeamua hivyo nipo tayari"
basi Nadya alifurahi saña Baada ya Suma kukubali kutoka nae.
maandalizi yalikua pambe tu nadya alimtolea nguo Suma na kumwambia
"baby hizi nguo nimekununulia mda mrefu lakini nilisahau kukupatia sababu ya mambo kuwa mengi"
"ooh asante saña Nadya wangu ndiomaana nakupenda saña"
"usijali bwana basi Wacha nikaoge kwanza maana hili joto ni lahatari"
Nadya aliingia chumbani na kuweka vizuri nguo ambazo zimo kwenye kabati like ambalo ametoa nguo na kumpatia Suma kisha akafunga kabati na kurudisha funguo kwenye handbag yake.
aliingia bafuni alioga kisha akabadirisha nguo na kutoka sebleni akamkuta Suma ametulia zake kwenye sofa ,Nadya kama kawaida yake yaani hupenda saña kumtumiia Suma wakati anajua mwenzake amechoka.
alienda kukaa karibu nae Huku manukato nzuri ikinukia na kikanga chake kifupi,Suma akamuhuliza
"mbona umevaa hivyo Nadya unataka nini?"
"Suma inamaana hujui nachotaka kwako hivi we ni mwanaume wa aina Gani lakini eeh wenzako wengine wanatamani waoate kutwa mara tatu kwa kila siku lakini we unajilegeza tu hapa aah ohk basi am sorry"
Nadya alikasirika na kuingia chumbani kwake alivaa viatu vyake na nguo zake nzuri ambayo ilimpendeza vema saña Kisha akatoka na kumwambia Suma
"me naondoka zangu na kuhusu kutoka na wewe nimebadirisha wazo langu hivyo nitakukuta Kwa heri"
Nadya aliondoka zake na kumwacha Suma akiwa hajali Wala Nini.
kama mjuavyo safari ya kutoka tabora Hadi dar hua ni safari ndefu saña watumia trein hufika kama sio siku tatu au nne inategemea,hivyo hata Aisha na mama mkwe wake siku hiyo hadi inafika usiku Bado walikua njiani ikabidi Aisha atafute hotel ya karibu Ili kuweza kupumzika usiku huo.
"mama mama amka basi tumefika hotelin twende ukajinyoshe kidogo"
"hapana mwanangu usijari mimi nimeshalala hapa panatosha"
basi Baada ya mama Suma kusema vile Aisha hakua na jinsi ikabidi tu na wao washushe siti zao waweze kulala kwenye gari mle mle.
upande wa Suma alikua amewakumbuka saña familia yake na zilipita kama wiki 4 hivi bila ya kuwasiliana nao na kwasababu hakua na simu lakini tayari Nadya alimfantia shopping ya vitu muhimu hivyo ikiwemo na simu.
aliingia chumbani na kuchukua suruali yake ambayo alikua amevaa wakati amefika hapo na kusachi kwenye mfuko na kukuta karatasi ya namba akachukua simu na kubifya sehemu kadhaa kisha akaingiza namba na kupiga.
simu ambayo ilimshtua Aisha kutoka usingizini alipokea na kuzungumza na Suma Kwa furaha saña
"vipi mpenzi wangu tumekua na wasiwasi saña kuhusu wewe kwanini ulikua kimya saña?"
"aah Aisha jamani nimekumisi pia mkewangu lakini kama unavyojua mambo Bado yameniwea magumu lakini afadhali Sasa kua nimepata simu tayari nivumilieni kidogo nitakua nawatumia pesa ya mahitaji mkewangu"
"Suma nakupenda sana mpenzi wangu zaidi ya sana naomba usinisaliti mwenzio nitaumia sana"
"aah .. a..Aisha siwezi kukufanyia hivyo najua wapi tumetoka mpenzi wangu"
"basi sawa pumzika kipenzi changu"
Suma alikata simu hku akiwaza kua tayari Aisha amemdanganya na vipi kuhusu mama yake kuanzia hapo Suma alikuaa nawasiwasi sana na mawazo yalikua mengi kupitiliza.
ilikua yaoata majira ya sa7 usiku Nadya alirudi akiwa amelewa sana siku hiyo,Suma alimshangaa sana sababu hakuwahi kumuona kabla Nadya akiwa yupo hivyo,alimchukua na kumpelekea chumbani akamlaza kitandani akamvuta viatu na kumfunika shuka kisha akawa anamtazama tu hakua amemuhuliza Chochote kile.
alitoka sebleni akiwa Bado anawaza saña.
asubuh mapema aliamka mapema na kufanya usafi kwenye nyumba mzima kisha akaandaa supu kwaajir ya nadya kisha akaenda kumwamsha Nadya aliamka na kumkumbatia Suma na kumwambia
"baby nimekumiss sana mwenzio"
"Nadya kipenzi amka ukaoge kwanza kisha nimekuandalia kitu ambacho kitakusaida kukuweka sawa basi amka usiwe mvivu"
Nadya aliamka na kuingia bafuni alioga maji kisha akarudi na kubadirisha nguo kisha akatokea sebleni na kukuta mambo ya supu mkate na mayai alikula na kumshukuru sana Suma
"Suma mpenzi Asante saña Kwa kunijari pia nisamehe kwa kilichotokea Jana sikutegemea kufanya vile ila nilikutana na mara fiki zangu ambao walipa vishawishi Hadi nikanywa kupitiliza"
"usijari kuhusu Hilo Nadya wangu nakupenda sana"
Suma alisogea karibu na nadya na kum'busu kwenye lipsi zake kisha akaondoa vyombo na kuiweka kwenye vyombo vichafu kisha akarudi kumwambia
"Leo kwakua jumapili basi nenda kapumzike Mimi namalizia kazi kisha nitakuja pia"
"really baby?"
"ndio nitakuja"
Nadya aliingia chumbani kwake na kujituoia kitandani alitoa Ile khanga aliyokua amevaa na kubaki mtupu akajifunika shuka akimsubiria Suma wake.
upande wa safari ya wahamiaji kutoka kijijini ilikua imetaradadi pia dereva alikua anakanyaga mafuta sio poa Huku story za hapa na pale zikiendelea.
Aisha alikua anawahulizia marafiki zake majirani Huyu dereva alikua anampa story mbali mbali ambazo zilikua zinamfurahisha sana Aisha na kumuhuzunisha pia.
Suma alimaliza kusafisha vyombo kisha alikaa sebleni akiwa anawaza
"hivi Nadya ananichukuliaje Mimi,kwanini ananitumikisha sana kingono hata kama nikimwambia kua nimechoka yeye Bado hunihitaji tu tatizo lake nini hasa mbona nashindwa kabisa kumuelewa Huyu mwanamke..mmh naona Huyu dada ananitumia pasi na mafanikio yoyote mana kama anaenipenda asingeniweka tu ndani kama mfanya kazi wake sawa nakula nalala lakini Sina Imani nae kabisa lazima nichangamke sikuja Huku kufata mapenzi nimekuja kufanya kazi kwaajir ya familia yangu Sasa nikisema nibweteke mama yangu na Aisha wangu watapata shida sana eeh Mungu nipe ujasiri kijana wako"
je unadhani itakuaje usikose itaeendelea....
PENZI LANGU 06
Hatimae wasafiri walifika salama jijini dar es salaam na Moja Kwa Moja gari ilielekea maeneo ya msasani ndiko ambapo kulikua na nyumba Yao ambayo watu wengine hawaifahamu.
yule dereva akamwambia
"dada Aisha nimekuleta hapa sababu ndio sehemu salama kwako hivyo utaishi hapa Huku tukiendelea kufanya kitu kizuri kwaajir Yako"
"aah sijaelewa unamaana Gani kusema hivyo kwani Kuna kitu gani nyuma ya hili ambacho sikijui?"
yule dereva aliona anaelekea kujaribu mipango hivyo akajikuta anampoteza Aisha Ili asishtuke akajifanya kumuhuliza
"KUMBE Bado unawasiwasi na kilichotokea?, usijari dada Aisha ni muda mrefu sasa umepita na usichokijua ni kwamba hao waliohusika tayari wameshatiwa kizuizini hawawezi kukufikia Tena"
"ooh Dan nenda tuachen tupumzike kwanza"
"Sawa dada Kila kitu kipo stoo ila ukihitaji chochote nipigie simu nitakuja"
"Sawa kwaheri"
Dan aliondoka na kuwaacha Aisha na mama yake Suma ,Aisha akamwambia mama mkwe wake
"mama hapa ndio nyumbani na tutaishi hapa"
"nyumba ni nzuri sana lakini ipo kimya sana"
"nikweli mama sababu hakukua na mtu yoyite ambae anaishi hapa tangu wazazi wangu wamefariki ilikua imefungwa tu na hatukua tunaishi hapa kabla,tulikua tunaishi kwenye nyumba nyingine huko masaki"
"ooh wazazi wako walikutengezea mazingira mazuri sana binti ila vijana wenye roho mbaya ya kwanini ndio iliyowafanya wateketeze familia Yako pole sana"
"Asante mama na sitaki kukumbuka kile ambacho kimetokea nataka kuanza upya na familia yangu mpya ambayo ni wewe na mpenzi wangu Suma sababu nawapenda sana"
"Aisha Wacha tu nikwambie kua na sisi tunashukuru sana Kwa ujio wako umetuvumbua mambo mengi sana pia hata akili zetu pia umezinyoosha kutokana kutotaka kutafuta amenedeleo kwenye maeneo mengi sababu ya uoga lakini Suma pia alikuaa muelewa kwako na akaamua kutuacha na kuja Huku bila ya uoga japokua ilimuwea vigumu sana kutuacha watu ambao anatupenda lakini hakua na jinsi"
"mama usijari kuhusu Hilo naamini kua Suma ridhiki yake kama iliandikwa atapata Kwa kuja mjini basi atapata mafanikio makubwa sana"
"nikweli mwanangu,ila tuachane na hayo ukweli nimechoka sana Nina uchovu mwingi sana nahitaji kupumzika"
Aisha alimpeleka chumbani na kumwambia
"utakua unalala Huku ndani siku zote na mimi nitakua nalala chumba cha pili kama ukiona huelewi utanishtua tu nitaamka hata atakaporudi Suma pia tutakua na furaha zaidi"
"Sawa mwanangu"
Aisha alitoka chumbani na kurudi seblen kisha akajilaza kwenye sofa Huku akikumbuka mambo mengi ambayo yametokea kipindi Cha nyuma Cha maisha yake.
alikua anawaza sana kuhusu kuripiza kisasi Kwa wale watu ambao wamemuulia wazazi wake lakini moyo wake ulijawa na wasiwasi sababu alikua anawaza kama ataianzisha vita upya atawapoteza Suma na mama yake hivyo ni jambo ambalo lilikua linamfikilisha sana.
""hahahaha Binti mrembo sana mashallah bwana Abdul na mkewake wamebahatika kupata Binti mrembo sana angalia macho yake kama mzungu pua yake mdomo wake angalia hata mwili wake pia,akiwa mkubwa atakua mtam sana huyu,hahahahahah""
ni sauti ambazo zilikua zinajirudia kwenye kichwa cha Aisha na Huku alijaribu kukumbuka sura za watu ambao wamewafanyia ukatili wazazi wake.
aliamka kutoka pale seblen akaingia bafuni akajimwagia maji kisha akajipumziaha kitandani kutokana na kuchoka Kwa safari iliyokua ndefu sana.
Kwa upande wa Suma pia alimaliza kazi zake mapema sana kisha akajilaza kwenye sofa mara akasikia mngurumo wa gari Suma alijifanya amelala fofoo,mara mlango wa nyuma pia ukafunguliwa na nadya akaingiapia nakufunga mlango kisha akasogea Hadi karibu na Suma kisha aka m'busu kwenye paji la uso na kuingia chumbani kwake akajimwagia maji na kutoka sebleni akiwa na kanga yake nyepesi kama kawaid yake akasogea karibu na alipoegesha Suma kichwa chake na kutoa mto ambao amelalia na kumuweka kwenye mapaja yake huku akichezea nywele zake.
"mpenzi jamanii kulala Gani huko jamanii nimerudi mkewako"
Suma alijifanya kujinyoosha na kutaka kuamka Nadya akamzuia na kumwamkia
"sitaki uamke kipenzi yaani natamani hata nisiwe naenda kazini tuwe tunakaa hivi Kila mara nataka kuimarisha upendo wangu kwako Kila siku"
"ooh Nadya unanipenda kiasi Gani?"
"yaani Suma sijawahi kumpenda mwanaime kama navyokupenda wewe sababu kwanza ni watofauti na wengine hauna tamaa mpole mkarimu kifupi unanivutia saña"
"ooh asante saña kipenzi changu,ila Leo nimeandaa chakula kizuri kwaajiri yako"
"baby lakini nimeshiba tayaro Leo ofsini kulikua na...."
"nadya tafadhali nataka ule japo kidogo tu mkewangu"
Nadya alivyoitwa make Tena alifurahi saña na kukubali kula chakula alichopika Suma.
walikua huku story za hapa na pale zikiendelea Suma nikama akitaka kuzungumza kitu lakini alipokumbuka kihusu maneno ambayo ameyazungumza Nadya kuwa yeye ni mwanaime wa tofauti Hana tamaa ikabidi ajitulize na kile alichotaka kumwambia abaki nacho moyoni mwake.
walkkula chakula Hadi wakashiba na kuzima taa kwaajiri ya kwenda kulala.
usiku huo ulikua wa mawazo saña Kwa Suma sababu alikua na mipango mingi saña kichwani kwake na ya kupata pesa hivyo akwa anatafuta njia ya kumueleza Nadya kihusu mpango wake.
Asubuhi mapema kama kawaida Suma aliamka na kuandaa Kila kitu na kumuamsha Nadya wake akajiandaa kisha akatoka sebleni kwaajiri ya kunywa chai.
wakati Nadya anakunywa chai muda huo Suma alikua anasafisha viatu vya Nadya na kuviweka mlangoni na kisha akamsogelea na kumwambia
"Nadya mkewangu Leo nataka kuwafanyia saplaiz marafiki zangu wakina juma sababu nimewamiss saña mana nilipotea machoni mwao tu ghafla na nataka nikwambie sehemu walipo Ili wasiwe na wasiwasi juu yangu"
"ooh Suma sitaki ukawambie sehemu ulipo kama unaenda tu kupiga nao story ni sawa ila sitaki uwambie ulipo Kwa Sasa"
"ooh kuhusu Hilo tu mkewangu ondoa shaka si unaniamini basi Wala hata usijali na sitachelewa kurudi,nitarudi mapema na kukuandalia chakula kama kawaida"
"sawa mpenzi wangu nakupenda saña Suma usiniache sawa mmewangu?"
"naanzaje kukuacha mwanamke mzuri kama wewe"
Suma akitaka kum'busu Nadya lakini ghafla simu yake ikaita hivyo hiko kitendo kikakatishwa na hiyo simu Kisha akapokea na baada ya muda mfupi alimuaga Suma Kwa haraka na kuondoka zake.
Suma alimshika kiuno chake na kusema
"chelewa Chewa utakuta mwana si wako Suma"
Suma aliingia chumbni na kuanza kupekua alifunga drop ya kitanda akakuta funguo nyingi akachukua zote na kuanza kufunguka kabati ambalo lilikua kubwa saña akafungua mlango wakwanza akakutana na nguo za kiume nyingi saña akafungua mlango wapili akakuta viatu vya Kila aina pia vya mwanaume na akaendelea kufunguka milango yote na mwisho kabisa akakutana na kisanduku akakifungua pia na alichokikuta kilimfanya astaajabu saña na kumfanya ashangae saña.
usikose itaendelea....