PENZI LANGU 07 - 9

 PENZI LANGU 07




Suma alivyostaajabu akajikuta anashindwa kufanya maamzi akafunga liale sanduku na kulirudisha kabatini na kufunga milango yote na kurudisha funguo kwenye droo na kutoka sebleni huku akihaha saña.


kichwani mwake ikamjia akili ya ghafla akarudi chumbani haraka na kuchukua Tena funguo kisha kufunguka kabati na kufunguka Tena lile sanduku na kuchukua vibunda viwili vya pesa kisha akafunga na kurudisha sehemu yake na kuingia chumba kingine na kuanza kuhesabu zile pesa zilikua nyingi saña kiasi kwamba alihisi kibunda kimoja kitamtosha saña hivyo alirudisha kimoja na kubaki na kimoja kisha akaweka kwenye begi lake na kutoka nnje na kufunga mlango kisha akapanda kwenye gari na kuondoka zake.


mtakua mnajihuliza gari alikua hawezi kuendesha jamanii ukiishi na mtu mwenye hela na aliyotofauti na wewe lazima na wewe uwe kama yeye hivyo hata Suma pia alikua mjanja saña alionekana mpole na mkarimu lakini mambo yake alikua anafanya kimya kimya.


alidika Hadi kwenye car wash ambayo alikua anafanya kazi akapiga honi kama kawaida vijana walichangamkia fursa na baada ya kufika Suma alishusha kioo kitu ambacho kiliwashangaza wote pale hasa juma ndio alikua mkaidi saña Kwa Suma siku hiyo akapiga salute.

walisalimiana kna kuanza kupiga story za hapa na pale kisha Suma akawambia

."nikweli nilipotea ghafla lakini zote ni changamoto tu ndugu zangu na Kuna msemo usemwao Kila kinachotokea hua kimepangwa na kuna sababu malum iliyofanya kitu hiko kitoke hivyo basi nataka kuwa bia kua nimepata bahati mwenzenu nimesaidiwa na mama mmoja hivi anapesa saña mwanzo alinifanya kama mfanya kazi lakini alivyozidi kuona namuheshimu basi ameniamishia ndani"


"broo kwahiyo unamkula huyo mama?"

rama alihuliza maana walikua wanashauku saña ya kutaka kujua vingi kuhusu Suma ,Suma akawambia


"sikilizeni mimi sio kama wengine sawa kwanza kabisa ngoja nisije kusahau kitu"

alizama mfukoni na kutoa pesa na kuwakabidhi Kila mmoja elfu20 kisha akawambia

"mtakunywa soda ila naomba nitoke na jyma kidogo ndugu zangu"


juma mwenyewe alikubali Kwa haraka tu kisha wakatoka Hadi sehemu walivyoona inafaa kuzungumza wakazungumza vizuri walichotaka kuzungumza Kisha Suma akataka kumrudisha juma kazini juma akamwambia hapana nataka kwenda kwangu,Suma alimpeleka juma kwake na wakiendelea kusisitiziana kile walichoongea kisha Suma akarudi nyumban kwa Nadya na kuendele na mambo yake mengine.


upande wa Aisha simu hiyo wakichelewa saña kuamka kutokana na uchovu alipomtazama saa ilikua saa4 asubuhi aliamka haraka akafanya usafi na kuandaa kifungua kinywa kisha akamwamsha pia mama yake na kisha baada ya kujiweka sawa walisogea mezani kwaajir ya kupata chakula, lakini kabla ya Aisha hajaanza kula mara ulisikika mlio wa simu ukitokea chumbani kwake,haraka aliwahi na baada ya kutazama aliona jina la Suma haraka akatoka chumbani na kumwambia mama yake

"mama Suma anapiga"

mama yake alichukua simu na kuipokea

"hallow mwanangu unaendeleaje lakini mbina umetususa hivyo?"


"mama nimeongea na Aisha akanambia uko sawa na sababu ulikua umelala nikamwambia akuache upumzike lakini samahan mama "


"Suma upo wapi baba mbona moyo wangu unaenda mbio mwanangu umefanya kitu kibaya Chochote mwanangu Nina wasiwasi sana juu yako"


"mama aa . kumbuka ku.... kua hakuna kitu kibaya nilichokifanya ondoa shaka kabisa kuhusu mimi mama"

"Suma usinifiche nieleze Mimi ni mama yako"


Aisha alichukua simu na kumuhulizaa sum Kwa taharuji

"Suma unanini mbona unamuweka mama kwenye wasiwasi umefanya Nini kibaya?"


"aah Aisha subiri takupigia"

mara Suma alikata simu na kumfanya Aisha aingiwe na uoga na wasiwasi pia kuhusu Suma hivyo hata chakula hakikulika kabisa sio mama yake Wala Aisha wote walikua na mawazo sana.


upande wa Suma pia ilikua inamuumiza sana sababu alikua anjihuliza mama yake amejuaje kuhusu alichokifanya na mara ghafla mlango ulifunguliwa na akaingia Nadya kitu ambacho kilimshangaza zaidi Suma maana hakuwahi kurudi mapema kiasi hiko Suma akamuhuliza

"vipi baby Kuna kitu umesahau?"

"aah ndio kipenzi na nachukua tu kisha narudi ofsini"

Nadya hakua na mengi ya kuzungumza aliingia chumbani na kuchukua afunguo kwenye droo na kufungua kabati lake kwenye mlango wa mwisho kisha akakifungua kle kisanduku wakati huo Suma alikua anachungukia kupitia tundu la kitasa Cha mlango huku jasho likimtoka kwenye mstari wa mgongoni likimtoririka sababu alijua vema kuwa anaenda kuumbuka hivi karibuni.lakini Nadya alikua hzie na mambo yake kisha akachukua kiasia alichohitaji na kuhifadhi sehemu husika kisha akatoka sebleni na kumkuta Suma amejilaza akiwa ana mawazo sana maana alishajua kipi anafanya hivyo akishajikatia tamaa kua Chochote kitakachotokea kitokee tu sababu amekipanga.


basi Baada ya nadya kufika sebleni akamwambia

"baby badae ila Leo nitachelewa kidogo nivumilie sawa mpenzi eeh"

"sawa mkewangu nakupenda"

sauti ambayo alikua amezungumza Suma ilikua yenye wasiwasi sana Nadya akasogea karibu na kumuhulizaa

"unanini lakini mumewangu mbona unaniogopesha kiasi hiko?"

"aah ni vile tu ni ...."

kabla hajamaliza kuzungumza simu yake iliita na akasimama na kumuaga Suma huku akimdanganya boss wake kua yupo kwenye foreni.


kuondoka kwa Nadya ndio ilikua nafuu ya Suma alishusha pumzi ndefu kisha akajihuliza

"inamaana Nadya hajagundua Chochote? itabidi nirudishe pesa ya watu kabla ya kugundua nilichokifanya"


Suma alitafuta namba ya juma na alitaka kuipiga hiyo namba lakini akasita na kuizima simu yake na kuweka Kando.

aliendelea na kazi zake kama kawaida na alikua mwenye mawazo sana siku hiyo hadi usiku,Tena siku hiyo kabla ya nadya kurudi alikua ameshalala.


Nadya alivyorudi akamkuta Suma amelala hakutakua kumsumbua kea Chochote kile alimuacha aendelee kulala.

zilipita kama wiki mbili Suma aliendelea kumkwepa Nadya siku hiyo Nadya akamtolea uvivu alipomkuta amelala akamwamsha na kumuhulza


"Suma unamatatizo gani sikuizi mbona sikuelewi eeh shida Nini hasa kial siku wewe ni wakwanza kulala na wa mwisho kuamka shida Nini eeh kama unaumwa unasema mtu anajua anaanzia wapi kama unahis nimekukosea pia unasema"


"aah Nadya nisamehe najikuta tu nakua mchovu sana"

"Suma unatembea na mwanamke mwingine nnje sio?"

"Nadya mama ni mambo gani ambayo unayazungumza?"

"sawa kama unajifanya huelewi ila nikija kujua kama unamwanamke mwingine nnje ukimuondoa huyo wa kijijini nakuuwa wewe na huyo malaya wako"


Nadya alikua na hasira sana Suma akaona atumie fursa hiyo kumtuliza mtoto apunguze hasira hivyo kama kawaida yake alishajua wapi anampatia basi walifika safari yao mwenyewe Nadya aliomba msamaha kwa Suma Kwa kile alichokisema

"baby nisamehe nimezungumza vibaya sana"

"usijali sana alafu unajua ukiwa unakasirikaga hivi huaga inakua tamu sana si unaona Leo umeinjoy sana eeh?"

"ndio baby nakupenda"

"nakupenda pia mpenzi haya Sasa lala Ili kesho uwe na siku mzuri kazini"

"Suma naomba utamu wako usimuonjeshe mtu mwingine yoyote yule zaidi yangu Mimi"


"na mimi pia Nadya na sasahivi nimeshasahau kuhusu mwanamke wa kijijini apambane na hali yake wewe na mimi tuutamu wangu ndio utamu wako sawa Nadya wangu?"

"sawa baby tulale"


Nadya hakuchukua mda mrefu alipitowa na usingizi lakini upande wa Suma alikua anapanga mipango yake kichwani kwake.


upande wa Aisha akazungumza

"mama hii wifi ya pili Sasa Suma hapigi simu hata kusema Chochote kile hivi hajui kama tunawasiwasi juu yake?"


"Aisha unachojihuliza wewe na mimi najihuliza hiko hiko kwani Suma amebadirika hivi"

"mama unavyosema hivyo unanifanya niingiwe na wivu juu yake"

"sijamaanisha hivyo amebadirika mambo yake yaani sio mpigaji wa simu tena na ameshindwa kusema ukweli Nini kinamsumbua inanipa wasiwasi sana"

"mama twende chumbani ukapumzike Mimi sitalala nitahakikisha namsumbua Hadi atapokea simu yangu."


Aisha alimpeleka mama yake chumbani na kumfunika shuka huku aliendelea kumtafuta Suma Kwa meseji Kwa njia ya kumpigia pia lakini hakua na majibu ya aina yoyote Yale.


asubuhi mapema Aisha aliamka nakuendelea kumtafuta Suma lakini hakujua na tofauti na usiku wa Jana,mara mlango ukagongwa haraka Aisha alifungua na kumuona Dan akamuhuliza

"Dan vipi mbona asubuhi mapema Kuna shida gani?"

"dada Kuna tatizo kubwa sana inasemekana kua wale wafungwa kule wamegudnua kua Bado unaishi wakati walikua umeshakufa hivyo muda wowote ule wanaweza kukuvamia hapa na kupoteza hivyo Kuna tiketi hapa ya wewe kuondoka haraka iwezekanavyo"


"Dan hizo tiketi naenda wapi Mimi eeh sikiliza Dan Sina popote pa kwenda na ikiwezekana nitapambana Hadi tone langu la damu la mwisho siwogopi Chochote kile sababu kwanza Sina moyo wa huruma Wala uoga Tena Dan wamenifanya niwe na moyo mgumu kama jiwe la mtumba Sasa utajua kama jiwe lamtunba ni la aina Gani"

Aisha alichukua Ile tiketi na kuichana mbeke ya Dan,Dana akamwambia

"lakini wazazi wako wame..."

"wazazi wangu wamefariki najua lakini wanataka niripe kisasi sababu nikiwa nakimbia sitaripa kisasi kwaajir ya wazazi wangu"

"Aisha dada lakini mbona upo hivyo wewe kwani usiwe muelewa tu jamanii?"

"nitakua muelewa kama utanielewa Nini namaanisha Dan nenda"

Aisha alifunga mlango Kwa hasira na kukaa chini akiwa na maumivu sana maana Dan nikama vile alimtonesha kidonda chake ambacho kilianza kupona.


upande wa Suma baada ya kuagana na nadya kuelekea kazini alimoigia simu rafiki yake wakaagana kukutana sehemu na wakakutana na juma alimkabidhi pesa Suma na kumwambia

"Suma nakuona mbali sana kwa sababu unaakili sana kaka endelea hivyo hivyo"

"usijali kaka nimekushirikisha wewe sababu wote nataka tuendelee na hata ikiwezekana tuzidi kuifanya car wash iwe yenye ubora na tuwatiwe na marafiki zetu pia kaka tufanye biashara"

"Sawa Suma hamna shida basi nitakupa taarifa zote"

"Sawa kwaheri"

Suma na juma waliagana na Kila mmoja kuondoka zake,Suma alipofika tu alirudisha zile pesa Kwenye sehemu husika na kusema

"Asante Mungu kwa kunirinda na hili jambo bila ya nadya kushtukia hili"

akawasha mziki na kuanza kucheza Kwa furaha mara ghafla mlango ulifunguliwa... usikose itaeendelea....


 PENZI LANGU 08

Wakati Suma anaendelea kucheza mziki mala ghafla mlango ulifunguliwa na nadya ndiye aliyeingia na kumkuta Suma anacheza Kwa furaha alivyogeuka na kumuona Nadya akamsogelea na kum'busu Kwa furaha kisha akamshika kiuno chake na kuendelea kucheza japokua alikua hajui style ya kucheza na mwanamke lakini Nadya ni jambo ambako kilikua linampa wasiwasi saña kwani Suma awe amebadirika ghafla vile lakini hakutakua kujionesha mbele ya Suma kuwa anamaswali mengi kichwani kwake waliendelea kucheza Hadi nyimbo ilivyoisha Kisha Suma alistop na kumuhulza


"umefurahi Kwa mara ya kwanza kucheza na mshamba mmoja kutoka kijijini?"


"jamanii suma ndio maneno gani hayo baby Mimi sikuchukulii kama mshamba bwana ila tuachane na hayo vipi mbona umekua na furaha saña hivyo?"


"Nadya unanifanya kuwa mwanaume mwenyw furaha Kila siku na vile nakupenda najihis naelekea kuwa chizi kabisa Kwa mapenzi yako"


"hahaha Suma acha bwana huwezi kua chizi yaani nilikua nimechoka saña sijihisi hata kuchoka Tena na Kwakua umesema una furaha na Mimi pia nafuraha Kwa ulichonifanyia Jana ukweli Jana ndio nimeusikilizia utamu wako na nikasahau kama kuna kufa Sasa basi baby Leo staki yule nyumban nataka twende tukale hotelini"


"ooh alafu hela unatoa wewe au Mimi?"


Nadya alitoa waleti Kwenye begi lake na kumkabidhi Suma na kumwambia


"nilipanga hili Kwa muda mrefu saña shika hii itakua waleti yako na Kuna kadi ya benki humo na namna ya Siri pia na pesa ambayo utaripia chakula usiku wa Leo"



Suma alifungua wallet na kutoa kadi ya benki na kumkabidhi mwenyewe Nadya na kumwambia


"Nadya sitaki hata kadi ya benki Sina matumiz ya aina yoyote Ile Kwa Sasa kwahiyo Wala hata usiwe na wasiwasi na Mimi"




Nadya ndio alizidi kumhisi vibaya Suma sababu akifikilia Dunia ya Sasa nani umpe kadi ya benki na aikatae kirahisi tu Nadya hakutakua kuongea Chochote akaingia chumbani kwake na Moja Kwa Moja akaanza kutafuta sanduku Ili aangalie maana alihisi huenda Suma amemuibia pesa zake.




nawakati Nadya anawaza hivyo upande wa Suma pia alikua anajiamini Kwa Chochote sababu mzigo tayari alisharudisha.




Nadya alitazma Kwenye sanduku na kuhesabu kisha akasema niliweka bunda kumi na nimeondoa vinne Bado sita,vipo vile vile kwani Suma anafuraha hivi huyu ni mwanaume wa aina Gani?




ni maswali ambayo alikua anjihuliza saña Nadya na baada ya kutoka chumbani akamkuta Suma anaitazama saña Ike wallet na baada ya kugeuka na kumuona Nadya haraka alimkumbatia na kumwambia


"mkewangu Asante saña Kwa zawadi yako nimeipenda saña"


"Amna shidaa basi twende tukaoge tuondoke baby"


"nenda kaohe sitaki nikuchoshe haraka nataka tukirudi huko ndo nikutengeneze vizuri"




Nadya aliingia ndani huku akiwaza kiasi Cha kumfanya awe na wasiwasi sana juu ya Suma.


aliingia bafuni alioga kisha akamwambia Suma kua yupo tayari na Suma pia alioga maji na kama kawiada yake Nadya alimtolea nguo na viatu Kwenye kabati na kumpatia simu hivyo Suma akamuhulizia



"Nadya hizi nguo ni zanani mbona umekua ukifanya hivi Kila wakati?"


"Suma sijawahi kukwambia kabla lakini nilikua na mpenzi wangu ambae nilimpenda sana lakini alikua akanisaliti baada ya kwenda kusoma huko nnje ya nchi na mpaka leo hii hajarejea hapa nchini,lakini hivi vitu navyokupatia wewe nikama vile nakuona ni yeye lakini siwezi kukufananisha NAE sababu yeye amekua mtu mbaya sana kwangu nakupenda wewe tu pekee Kwa Sasa"




"ooh pole sana Kwa kilichokutokea"


"Asante alafu pia usinihulize kuhusu mapenzi yangu yaliyopita yananiumiza na kunirudisha nyuma"


"sawa nisamehe Bure"


basi walitoka nnje wakiwa na furaha sana japokua Kila mmoja alikua anamuwaza mwenziwe kwani amekua hivyo.


walifika Kwenye hotel moja yenye viwango flani hivi Kisha wakaagiza chakula na kuanza kula Kwa mahaba yote yaani siku hivyo ndio Nadya alioneshwa mahaba yote na Suma alikua anamdekeza sana Nadya akasahau shidaa zote na kumuamin suma kupita maelezo.


walirudi nyumbani na kufikia kulala sababu ya kuchoka sana.


siku zilienda sana 


ilikua siku ya jumapili ambapo wakimaliza kufanya kazi kwa pamoja kisha wakapumzika Kwenye bustani Kwa bustani Tena Kwa mikao ya kimahaba ,Suma alikua amenyosha miguu kisha Nadya akalala Kwenye miguu yake huku akichezea nwele zake wakati huo Nadya alikua bize na mitandao ya kijamii,mara simu yake iliingia ujumbe na baada Nadya haraka aliusoma huo ujumbe ulisomeka


"Nadya mpenzi narudi baada ya wiki moja nakupenda sana na nimekukumbuka sana,marafiki zangu wengi wamekua wakinitambia na watoto zao na mimi nataka unizalie mtoto mzuri sana kama wewe mwenyewe hakika nitakua na furaha zaidi na zaidi nakupenda sana"




Nadya aliamka pale alipokaa na kuingia ndani akiwa amechanganikiwa sana na hata huo ujumbe hakua ameujibu maana alitokea online Kwa haraka sana"




Suma alitumia fursa hiyo kushika simu yake na ndipo alipoona jumbe nyingi na calls nyingi saña akanihuliza


"hee kumbe mbona ni zamuda mrefu sana na harafu sikuwahi kuwapigia Wala kuwaambia Chochote mama atakua na wasiwasi sana haraka alipiga simu,simu iliita bila ya kupokelewa alijaribu kupiga kama mara tatu lakini simu haikupokelewa na yeye alianza kujiskia vibaya sana maana alihisi huenda mama yake amepatwa na jambo baya..


aliingia ndani akiwa amechanganikiwa pia Nadya alivyomtazama Suma akahisi huenda labda amekasirika baada ya yeye kutoka kwenye bustani bila ya kumwambia Chochote.




akaamua kumsogelea na kumuhulizaa


"vip baby mbona umekua hivyo?"


"sijui Nadya sjui mama yangu amepatwa na nini simu yake inaitwa tu bila ya kupokelewa"




Nadya akafurahi maana alihisi huwenda Suma amekasirika Kwa yale mambo basi Nadya akasimama na kujisemea moyoni bora Kila mtu apambane na hali yake.




Nadya alikua amechoka sana na hajui Nini afanye maana hakutegemea kile alichoambiwa.


alioga maji na kumuaga Suma kuwa anatoka Suma Wala hata hakumjali maana nae Apia alikua na mawazo yake.


upande wa Aisha alikua nyumbani kwao na marafiki zake wanaongea mambo mbali mbali huku wakimwambia asiwe anakaa tu ndani siku Moja Moja awe anawatembelea pia Aisha alikubali na kuwaahidi hivyo lakini wakati wanaongea mama yake na Suma hakua akipenda kabisa alichukia ujio wao na hata vishawishi vyao Kwa mkwe wake.




baada ya kuondoka Aisha akaandaa juisi na kumpelekea mamkwe wake alipokea na kukaa walikunywa pamoja kisha Aisha aliingia chumbani kwake na kushika simu akakuta amepigiwa na Suma mara tatu haraka akampigia Suma hakuachelewa akapokea simu na kabla ya salamu alichihuliza ni kuhusu mama yake


"mama yangu Aisha yupo wapi?"


"Suma ndio tabia Gani hujasalimia hata"


"Aisha niambie mama yangu yupo wapi?"


"sawa mama yuko sebleni Mimi nili..."


"mpe simu mama yangu tafadhali"


Aisha alimshangaa sana Suma mbona amekuwa hivyo lakini hakua na jinsi alimpelekea simu mama yake wakaongea kisha akakata simu.


Aisha akiwa anasubiria labda yeye ataitwa lakini hata hakuitwa alipotoka Tena chumbani kuja sebleni akamuhulizia mama yake


"mmeelewana mama?"


"ndio tumeelewana"


"sawa jambo zuri"


Aisha alichokitegemea labda kuambiwa kua Suma amemmisi au kusalimiwa hakuskia Chochote akahisi tu lazima kitakua na jambo kinaendelea,


alichukia simu na kuingia chumbani na kumpigia simu Suma lakini haikupokelewa Aisha aliumia sana na kujisemea


"najua sana kua tayari Suma ameshabairidka na hwezi kunikumbuka Tena ila Leo ndio mwanzo na mwisho wangu wa kumtafuta kama kuishi na mama yake nimeishi nae vizuri tu Sasa nimuda wangu wa kufanya mambo yangu na sio kurudi nyuma kisha mapenzi hapana"


Aisha alikua anahasira sana na Suma lakini hakutakua kujionesha.




majira ya usiku Sasa Suma alikua amelala zake sebleni mara akasikia sauti ya kirevi ikiwa inatukana sana na mlango ukafunguliwa Nadya akaingia akiwa amelewa sana kitu ambacho kilimshangaza sana Suma maana alifanya hivyo kabla na aliapa kutorudia na leo karudia Tena anatukana matusi makubwa sana Hadi Suma alikua anajiskia vibaya sababu alikua vema hakuna miwngine anaetukanwa hapo zaidi ya yeye anaeyaskia hayo matusi.


aliambeba nadya nakumpeleka chumbani kisha akamlaza kitandani na yeye akarudi kulala sebleni akiwa anajihuliza kwanini nadya awe hivyo?


usikose itaeendelea....


 PENZI LANGU 09

Suma aliamka asubuhi kama kawaida yake na kumuandalia Nadya supu kisha akaenda kumuamsha Nadya aliamka na kuoga maji kisha akatoka sebleni akiwa amepndeza mwenyewe akamuaga Suma kua anaondoka Suma akamuhulizia


"Nadya Kila siku huondoki bila kunywa chai na Leo nimekuandalia supu kwaajir ya pombe ulizokunywa Jana"




"Suma sijiskii kula Chochote badae bwana"


Nadya aliondoka zake na kumwachia Suma mwenye mawazo sana akachukua simu yake na kumkuta missed calls za Aisha akazifuta na kumpigia lafiki yake juma wakakutana hapo kwenye duka la vifaa vya magari na akamuhulizia


"vipi Ile hela ambayo nikikuelekeza umefanya kama nilivyokuambia?"


"yaani Suma mbona Bado kidogo tu kila kitu kinakua sawa"




basi Suma baada ya kumaliza kuzungumza na juma alitoka Hadi kwenye matengenezo na kumkuta Kila mtu Yuko bize na kusimamia matengenezo ya sehemu ya kuosha magari.




wote walismhukuru sana Suma Kwa moto aliokua nao wa kuwainua kutoka pale walipokua Suma akawambia kua wasijari Kwa Chochote kile.




Suma alirudi nyumbani mapema na kuandaa chakula vizuri na kukihifadhi kwenye hotpot kisha akwa anaangalia movie.




siku hiyo nadya alichelewa sana kurudi Suma alilala pale pale Hadi alishtuka baada ya kung'atwa na mbu na baada ya kumtazama saa ilikua saa7 usiku Bado Nadya hajarudi nyumbani ikabidi achukue simu kwaajir ya kutaka kumpigia simu iliita na kukatwa muda huo huo na baada ya muda mfupi Nadya aliingia ndani akiwa amelewa Tena kama siku iliyopita Hali ambayo ilikua inampa mashaka sana Suma.




aslimama na kwenda kumdaka maana akitaka kuanguka na kuumia vibaya kutokana na viatu virefu alivyokua amevaa.


sum aliumia sana kutokana na Ile Hali basi alimbeba na kumpeleka chumbani Tena na kumlaza kitandani huku alizungumza


"nadya hiki unachofanya unanifanya niogope sana na mbona umebadirka ghafla niambie kama numekisea nijirekebishe lakini sio kunitenga na kunifanyia haya yote mkewangu kumbuka mimi ni binadamu pia Nina moyo Nadya tafadhali"




nadya aliziba maskio yake na kugeuka upande wa pili kulala zake kitendo ambacho kilimuumiza zaidi sum basi hakua na namna akarudi sebleni pia akalala.




hiyo ilikua siku ya jumatatu na ikumbukwe kuwa tayari Nadya alishatumiwa ujumbe na mpenzi wake kua baada ya wiki moja anarudi hivyo hatujui huyo ni mpenzi wake au ndio kama alivyomwambia Suma kuwa alimsaliti.




upande wa Aisha hakua analala sababu ya mipango yake ya kuhusu kuripa kisasi na kilichokua kinamuwazisha ninani ayamuamini kufanya nae kazi maana limuamini sana mpenzi wake Suma lakini amehisi kua amemsaliti lakini hii siri ya Suma kumsaliti Aisha tunaijua Mimi na wewe ndugu msomaji ila Aisha na mama yake wote hawajui ispokua Aisha anahisi kutokana na vijitabia mbalimbali.




"kama Suma ameweza kunisaliti nani naweza kumuamin Kwa kufanya nae kazi ya kuripa kisasi,na pia najua kua nikazi ngumu haitahitaji vijana wavivu na najua pia itatumia pesa nyingi saña lakini sijali kuhusu Hilo nia na malengo yangu ni kuripa kisasi tu na lazima nifanye hivyo"




Aisha alichukua simu yake na kubofya sehemu kadhaa kisha akaweka simu sikioni kwake na simu iliita na kukata yenyewe na baada yakutama muda akatabasamu na kusema


"eeh kumbe ni usiku wa saa7 mmh aise lazima ndiomaana hajapokea itakua amelala"


Kisha nae akavuta shuka na kulala zake.




asubuhi mapema Aisha aliamka akavaa traki na vest yake na raba akatoka bila ya kumuaga mama yake Suma.


na upande wa Suma aliamka mapema kama kawaida yake kuandaa kifungua kinywa kwaajir ya nadya na aliamka na kuaga maji na kuondoka wakati huo Suma alikua bize na kazi zake nyingine na alivyorudi chumbani kwaajir ya kutaka kumuamsha Nadya hakumkuta na alipojaribu juangaza kote hakuona hata gari ya nadya alikua anajihuliza sana saña na ilizidi kumfanya ajionee sio wathamani Tena hivyo akajisemea


"najua Sasa nimechoka sana ndiomaana haya yite hutokea huyu sio Nadya ambae nimenzoea siku zote wanasema jiongeze kabla haujaongezwa hivyo hapa akili imo kichwani mwangu Sina muda wa kupoteza Tena.




alichukua simu yake na kubofya sehemu kadhaa ya keypad yake na kuweka sikioni kwake.




upande wa Aisha alikua kando ya barabara alikimbia na kufanya mazoezi ya viungo akiwa na hasira sana mara alipita kijana mmoja ambae nae pia alikua anafanya mazoezi akamwambia


"usitumie nguvu kufanya mazoezi maana utafanya mili wako uchoke kupitiliza"


"ahaa asatne sana kwa ushauri wako"




mara simu ya Aisha ikaita alifungua zipu ya traki yake na kutoa simu Kisha kupokea bila ya kutazama nani alikua anapiga ikasikika tu sauti


"mama shikamoo..!"


"marahaba Suma lakini Mimi sio mama yako"


"Aisha unathubutu vipi kuitikia Kwa kujiamini hivyo we mjinga sana Yani niambie mama yangu yupo wapi?"


"aah Sasa Suma Naina umeota mapembe enewei kama unahitaji mama yako basi moigie kwenye simu yake mjinga mmoja wewe"


Aisha alikata simu na kuiweka kwenye traki yake na kuendele na mazoezi yake na yule kaka akiendelea kumsemesha


"kwanini unafanya mazoezi Kwa hasira nahisi Kuna jambo unapanga kufanya kama sikosei"


"yeah nikweli lakini hayakuhusu"




yule kaka ilibidi awe kimya Kwa muda kisha kumuacha Aisha akiendelea kukimbia Kwa kwenda mbeke na kurudi nyuma lakini mara ghafla wakati anarudi nyuma kuna gari ilitokea nyuma yake na kumpush Aisha na kumfanya aanguke chini kwa kukosa pumzika kutokana na mazoezi ambayo alikua anayafanya yalikua yananguvu sana na yeye alikua anatumia nguvu na hasira pia.




na wakati like jambo limetokea yule kaka ambae alikua anamsemesha Aisha aliona na haraka akawahi kumbeba na kumwambia aliyemgongaa ampeleke hospital na hakua mwingine alikua ni Nadya kutokana na msongo wa mawazo kichwani kwake.




walifika hospital na baada ya kumfanyia vipimo akagundulika kuwa yupo salama ila alizima kwaajiri kukosa hewa mshtuko Yu lakini hakua ameumia,Nadya alifurahi sana maana hakuwahi kupata kesi ya kugonga hivyo alikua muoga sana.




baada ya kupata nafasi ya kumuona Aisha alimuomba msamaha na Aisha akamwambia Hana tatizo amemsamehe tayari kisha akaripia gharama za hospital na kuondoka zake.


Aisha alibaki na ye kijana Sasa wakati huo tayari walikua wanatoka hospital wakiwa wanatembea kawaida yule kijana akajitambulisha


"naitwa Samuel"


"naitwa Aisha ila kwanini ulinisaidia wakati nilikujibu vibaya kabla?"


"Aisha tunatakiwa kuwa na moyo wa ubinadamu sawa wewe ulinijibu vibya lakini Mimi sikutaka kukufanyia ukatili wa kutokusaidia sababu nisingepata faida yoyote kama ungekua umeumia alafu sijakusaidia,lakini nimekusaidia nimepata kufahamiana na wewe"


"ooh nikwi pia nisamehe kwa kukujibu vibaya"


"usijari kuhusu Hilo Aisha lakini nataka kukukaribisha nyumbani kwetu Kuna gym pia unaaeza.kuja kufanya mazoezi yote unayotaka wewe"


Aisha alitabsam na kumuhuliza


"serious unachosema?"


"ndio karibu sana najua pia itakua nafasi kubwa sana ya kufahamiana kwa ukubwa zaidi"


"Asante saña unaonekana mkarimu sana Samuel.."


Aisha alimtajia namba ya simu Kisha waachana kwenye njia panda na Kila mmoja kuelekea nyumbani kwao.




alidika nyumbani kwao majira ya saa6 mchana akamkuta mama yake na Suma amekua nawasiwasi alimsalimia na kutaka kuingia chumbani kwake mama Suma akamwambia


"kwanini unanikwepa Aisha?"


"mama kwanini nikukwepe mama?"


"Aisha umekua hivyo Kwa muda hata Mimi aliona ndiomaana nakuhuliza shida Nini?"


"hakuna shida yoyote mama ni mawazo yako tu hayo"


"Sawa unatoka wapi sasahivi na hunavaa hata nguo huko juu?"


"mama nimeanza kufanya mazoezi yangu Sasa na nitakua natoka Kila alfajiri ila bahati mbaya nikipata ajari kidogo ndiomaana nimechelewa Leo"


"ajari Gani Tena mwanangu ona Sasa jamanii"


"usijari mama ilikua ya gari lakini sijaumia ndiomaana nipo hapa"


"pole sana mwanangu nenda kaoge uje kula"


Aisha aliingia chumbani kwake akajimwagia maji na kujilaza kitandani kwake.


hatimae siku ya jumanne ilifuka usiku ndipo Aisha alimaka na kumwambia mama yake kua anaijiskia vizuri akachukua simu na kumpatia mama yake na kumwambia


"Suma alipiga akataka kuzungumza na wewe mpigie"


mama yake alichukua simu Aisha akawa Yuko bize kutengeneza maziwa ya unga kuweka maji ya moto kisha akachukua na mkate akaanza kula huku alijifanya yupo bize na tv.




mama yake na Suma akawa anongea na simu na mwanae


"mama uko sawa kweli?"


"Suma nipo Sawa na Aisha ananijari sana kwani shida Nini?"


"mama nataka kurudi nyumbani mimi maisha ya huku yamenishinda Sasa sitaki tena kuwa huku"


mama yake Baada ya kuskia hivyo mama yake akamuita Aisha Hadi Aisha alishtuka na kujikuta akimwaga maziwa yake na kumfata mama yake na kumuhuliza


"shida Nini mama?"


"Suma anataka kwenda kijijini"


Aisha alikata simu na kumwambia mama yake mama umeshaharibu najua Suma ameshakusikia tayari aaha"


Aisha alichukua simu na kuingia nayo chumbani,kitu ambacho kilimshangaza sanaa mama yake Suma akasogea sebleni na kumkuta maziwa yamemwagika akasafisha na kurudishwa kikombe kwenye vyombo vichafu.


upande wa Suma alianza kumtumia ujumbe Aisha kumuhuliza kuhusu alichokisema mama yake Aisha hakua amejibu meseji hata moja ya suma"


muda ulizidi kwenda Kwa kusubiri ujumbe kutoka Kwa Aisha na Huku akimsubiria pia Nadya.


siku hiyo alisota sana kusubiri vitu viwili Kwa wakati mmoja Hadi inafika asubuhi hakuna chochote alichokipata.


Suma siku hiyo akachukua karatasi na peni kisha akaandika walaka mzito sana na kisha akachukua nguo zote ambazo alikua amempatia Nadya na kuviweka kitandani kisha akatoka nnje na kufunga mlango na kuondoka zake hakuchukua kitu chochote zaidi ya kama vile alivyokua amekuja.




alifika dukani Kwa juma na kumwambia


"juma rafiki yangu pesa ambayo umekua ukiniwekea kwenye akaunti yangu inatosha sana kaunzia Sasa Kila pesa ambayo itakua unaipata hapa dukani ni yako na pia hili duka nilako na kule car wash utawachia rama na wenzie Mimi wacha nirudi nyumbani kwetu"


"Suma unamaana unarudi Kijijini?"


"ndio juma narudi kijijini kwetu"


"hapana usifanye hivyo Suma mbona tayari umeshaanza kutengeneza pesa nzuri tu jamanii?"


"usijari juma kwaheri kama Mungu akipenda tutaonana"


unadhani itakuaje usikose itaendelea....




Previous Post Next Post

نموذج الاتصال