PENZI LANGU 10 - 13

 PENZI LANGU 10

PENZI LANGU simulizi
PENZI LANGU 10


Suma alikua anatembea akiwa anawaza mambo mengi Sana kichwani kwake na hasa kuhusu mama yake na Aisha maana hakua amepata jibu sahihi kuhusu wao.


upande wa aisha na yeye kama kawaida yake alitoka nyumbani kwake mapema saña alikianza na zoezi la kukimbia kabla hajafika mbali simu yake iliita na mpigaji alikua Dan walisalimian kisha Dan akamuhuliza

"dada Aisha ulinipigia juzi usiku Jana nilikua bize saña sikuweza kukutafuta lakini Leo nipo Sina mzunguko wowote vipi kuna tatizo lolote?"

"Dan mdogo wangu naomba niandalie safari yangu ya kuondoka nchini nadhani nitakupa taarifa siku Gani naondoka lakini Kaa attention Kwa hili jambo"

"ooh sawa dada Aisha hakuna shida Kwenye Hilo vipi lakini unahitaj Chochote?"

"hapana Dan we endelea na mambo Yako tu usijari"

Dana alikata simu na kuonekana mwenye matumain Fulani maana alionekana kua na furaha sañaiwsho akasema

"hatimae sasa nadhani atakua na furaha sana Baada ya kuwaona"


upande wa Aisha akakumbuka kua siku ya Jana alipata namba ya mtu ambae alimwambia kuhusu gym haraka aligeuka na kurudi nyumbani kwako na kuingia ndani ilikua tayari saa mbili alimkuta mama Suma amekaa sebleni alimsalimia na kuingia chumbani kwake alitoka akiwa na funguo kichwani kwake akiwa amevalia kofia na Sweta jeusi na raba nzuri sana akamuaga mama Suma

"mama naondoka nitachelewa kurudi kidogo hivyo kama utajihisj njaa andaa chakula ule usinisubiri Mimi"


mama yake Suma alimsogelea na na kumshika mkono wake na kuzungumza Kwa upole sana 

"Aisha mwanangu mbona umebadirika sana tatizo nini mama?"

Aisha aliutoa mkono wa mama Suma na kumwambia 

"hilo swali Mimi sio wa kunihuliza mama naondoka zangu sasahivi"


Aisha alivaa miwani yake na kuondoka zake,na kumwacha mama Suma akiwa Kwenye sintofahamu.

Aisha alifika nnje na kupanda Kwenye gari alichukua simu yake na kumpigia Samuel simu iliita mara kadhaa kisha ikapokelewa

"Halo Samuel mambo Yako?"

"poa Aisha vipi unaendeleaje?"

"Niko poa Sasa basi mambo yasiwe mengi naomba unielekeze wapi ulipo nije Kwenye gym yenu"

"anhaa washa data na kisha zama Kwenye map utaona mahari nilipo"

"sawa Samuel nimekuelewa"

Aisha alikata simu na kufanya kama alivyomwambia Samuel na kisha akaona sehemu anayoishi Samuel hapakua mbali na sehemu ambayo anapishi hivyo aliwasha gari na kuondoka zake.


alikua ameweka headphones kichwani kwake huku anaendesha gari huku anapata mziki mzuri kutoka Kwa wasanii wenye vipaji wa huko marekani.

mara ghafla akiwa barabarani Kwenye mwendo wa kawaida akampita mtu ambae nikama anamfahamu hivyo ikAbidi arudi nyuma Ili ajue ninani au amemfananisha.

Aisha alirudisha gari nyuma na kumfikia huyo mtu na kumpigia honi alivyogeuka lahaula hakua mwengine alikua ni Suma Aisha alimshangaa saña akashuka Kwenye gari na kumuhuliza 

"usitake kunambia kua unaigiza maisha?"

"Aisha kwanini uko hapa,hivi ni wewe kweli?"

"Suma kwani Mimi si mkazi wa huku kwanini unataka kujua sababu ya Mimi kua hapa?"

"aah Aisha mama...."

"Suma kunasehemu naenda Kwa Sasa kwaheri"

Aisha aliingia Kwenye gari na kubamiza mlango wa gari Kwenye harakati za kuvaa mkanda aweze kuondoka Suma aliifungua mlango wa pili wa Kwenye gari hiyo na kuingia na kukaa kando ya Aisha kitu ambacho kilimshangaza saña Aisha akamuhuliza

"unataka nini Kwenye gari yangu?"

"Aisha siwezi kukuacha uwende popote pale nahitaji kujua mama yangu Yuko wapi?"

Aisha hakujibu kitu Chochote aliwasha gari akachukua headphone zake kama kawana kuzivaa kisha akaendelea na safari yake hadi sehemu husika.


aliingia gari enani ya nyumba yenye geti kisha akampigia simu Samuel na baada ya muda mfupi Samuel alitoka ndani akiwa na kitaulo chake Cha kujifuta jasho na baada ya kumuona Aisha alimkaribisha na kumbato kisha wakaingia ndani,wakati huo Suma alikua Bado yupo Kwenye gari hakutaka shobo sababu alikua fika kua pale sio nyumban kwao na Aisha na kama ingekua pale Aisha angesema Chochote lakini alovyojiwazia akilini mwake ndicho alichokiamua.


alisubirri Kwa muda kama lisaa1 na nusu Aisha Bado alikua hajarudi garini kitu ambacho kilianza kumfanya awe na wasiwas saña kuhusu Aisha akasema hatakama nimemsaliti lakini siwezi kuona ujinga unaendelea wakati nipo tu hapa nimekaa.


wakati anataka kufungua mlango wa gari mara akaona mlango umefunguliwa na Aisha alitoka ndani akiwa na taulo pia akijifuta jasho kisha akaingia Kwenye gari na bila ya kuzungumza Chochote na Suma.

muda wote Suma alikua anamtazama Aisha Kwa shauku ya kutaka kujua Nini kimetokea kule ndani lakini Aisha alikua bize na kuendesha gari huku akiimba nyimbo ambayo alikua anaiskikiliza.

walifika nyumban kwao Aisha alishuka Kwenye gari na kuchukua vifaa vyake na kuingia ndani akamkuta mama Suma amelala akapitiza Hadi ndani chumbani kwake.


Suma pia aliingia ndani kwa kuchelewa saña kutokana na kutazama ukubwa wa nyumba na mazingira pia,ukweli ilikua mitaa ya kishua saña.

alipita ndani na kumkuta mama yake amelala Kwenye sofa hataka alimsogelea Kwa furaha na kumwamsha

"mama..! mama ... mama Suma!"

mama yake alivyoamka na kumuona mwanae alimkumbatia kwa furaha saña akamwambia

"nilihisi naota kumbe uko hapa kweli?,mwanangu nilikukumbuka saña Suma wangu tazama Sasa Aisha amenifamyia Kila kitu amekua akinipenda saña saña Hadi amenifanya niwe natembea na Hadi afya yangu imerejea upya kwasababu yake"

Suma alijiskia amani ya moyo lakini alikua na mawazo saña kuhusu alichokifanya.

"mama Aisha ni Binti mwenye moyo wa kipekee saña na hakuna mwanamke mvumilivu na mwenye upendo kama Aisha na naamini kua sikufanya ubabaifu Kwenye chaguo langu"

"nikweli kabisa mwanangu,lakini mbona umekua hivyo shida Nini wakati tulipokua tunaongea na simu ilikua unaonekana mwenye furaha tatizo Nini?"

"mama Nina mengi ya kuwasimulia wewe na Aisha Wacha tumsubirie kisha nitawaambia"

"lakini Aisha ametoka mbona"

"mama nimerudi na Aisha Mimi hapa nisingeweza kufikia hapa bila yeye"

"ooh kumbe, nilikua sijamuona hivo"

"itakua yupo ndani"


mda mchache mara Aisha akijitokeza na kupitiliza Hadi jikoni akajiandalia maziwa yake kama kawaida kisha akasogea seblen akawasha tv na kuanza kutazama.


wakati anaendelea kula chakula na kutazama tv mara simu yake iliita na haraka akapokea na alijikuta akipaliwa na kukimbilia nnje kutapika upande was Suma ilimjengea picha tofauti sana alihisi hata Aisha alikua anamsaliti pia na huko kutapika hakuna kingine zaidi ya mimba,ikabidi amfate Aisha nnje na kumkuta ameacha simu inaingea yeye akiwa anaendelea kutapika, wakati huo Suma amesimama mlangoni akimtazama.


Aisha Baada ya kumaliza kutapika Aisha alichukua simu na kuzungumza

"Dani nimetapika najiskia vibaya sana je Leo unaweza kuja kumuona alafu nataka tuzungumze kitu muhimu naomba usichelewe kuja nitaboeka sana"

Aisha alipomaliza kuongea na simu alisimama na kurudi ndani lakini alivyopiga jicho mlangoni akamuona Suma hakutaka kuongea nae chochote alipita moaka ndani na kumwambia mama yake

"mama nipo ndani najiskia homa"

"Sawa mwanangu pumzika"

Aisha aliingia ndani na kuwaacha wenyewe wakizungumza.

upande wa Suma alitamani sana kuzungumza na Aisha lakini nafsi yake ilikua inamsuta sana Kwa kike alichokifanya yeye pia ilikua inamuumiza sana.


je unadhan itakuaje usikose itaendelea....


PENZI LANGU 11

Muda ulizidi kusogea hatimae ilifika jionj ,ilikua majira ya sa12 Aisha aliamka akaanza kuandaa chakula cha usiku Huku akiwa kimya kabisa ukweli alitamani sana kumuhuliza Suma kwanini alikua anamdharau kwenye simu hapokei simu zake lakini alishindwa kumuhuliza sababu hakutaka kujionesha kama ni dhaifu kwake hivyo alikua anasubiria Suma ndio aanze kumuhuliza.




alimaliza kuandaa chakula Kisha akakiweka mezani kwaajir ya kuliwa tayari ilikua saa9 mbili usiku alichukua sahani yake na kujiwekea chakula chake na kusogea sebleni na kumwambia mama yake


"mama ukiwa unajisikia kula chakula kipo tayari pale mezani"


Suma alipoona Aisha anaelekea upande wake akajua moja kwa moja anapelekewa yeye kile chakula alijikalisha vizuri kwaajir ya kukipokea lakini Aisha akasogea mikono pembeni akabadirisha channel na kumuwekea channel ya movie ambayo anapendaga mama yake na Suma.


Suma alizidi kujiskia vibaya Kwa kutengwa na Aisha akaamua kumfata Aisha pia na kumshika mkono ule ambao alikua ameshika sahani ya chakula na Ile nguvu aliyotumia kumshika Aisha alishindwa kujibalansi na sahani ya chakula ikaanguka chini Aisha alimtandika kofi Suma na kumwambia


"usijifanye wewe ni mwenye nguvu pekee Sawa eeh shida yak....!"


kabka hajazungumza akaanza kutapika Suma alimsogeza chini na kumtazama Kwa jicho la Maumivu sana Hadi alishindwa kujizuia.




upande wa Nadya kama kawaida yake alirudi usiku sana ila siku hiyo alikua mzima kabisa hakua amelewa na wazo lake lilikua la kuja kumwambia ukweli Suma kuhusu ujio wa mpenzi wake lakini alivyofika akakuta nyumba ipo kimya sana aliingia ndani na kuwasha taa zote na kitu cha kwanza aliingia chunbani kwake maana ukimya huo ulimtia mashaka sana na kuhisi Suma ameshamuibia pesa zake.


alipoingia chumbani kwake akakuta kitanda kimetandikwa vizuri sana na baadhi ya vutu vikiwa juu ya kitanda akaachana navyo sababu yeye alikua na mawazo na pesa tu Kwa muda huo.


alifungua kabati lake na kutazama kwenye sanduku akakuta pesa kama ilivyo vile vile akafunga vizuri na kurudi kitandani akakuta nguo zote ambazo alimpatia Suma na Kila kitu kilikuwepo hapo akawa badoa anajihuliza kuhusu Suma ni kijana wa aina Gani lakini kwenye harakati flani akaona karatasi nyeupe juu ya dressing table alisigea na kuichukua Kisha kuanza kusoma


"mpendwa Nadya


     nimeamua kuondka nyumbani kwao kutokana mambo mabaya ambayo umekua ukinifanyia mwanzo nilipotezea na kukupa muda zaidi wa kukufanyia ujifunze lakini Bado haukuonesha kubadirka nimekua nikifanya Kila kazi ambayo ulitakiwa kumfanya kwangu kama mwanaume lakini sikuwahi kukuambia sababu nilijua kua unaishi na mimi kwa nguvu ya. pesa zako.


Nadya nilimsaliti mwanamke ambae nampenda sana ambae alinifundisha Mimi mapenzi mwanamke wakwanza kwangu kujifanya Mimi kuitwa mwanaume nikamsaliti sababu yako.


nikweli kwamba mwanzo nilikua sikupendi na nilikuambia ukweli lakini hukujali nilichosema ukaja ukaniteka na penzi lako lakini nataka ujue Leo kua sikua na wewe kwaajir ya tamaa ya pesa sababu kama ningekua hivyo ningekua nakuibia pesa zako na kuwatumia familia yangu lakini tumekua tunalaka na pesa ndani lakini Kijijini kwetu mama yangu anaugua na kushinda na njaa lakini hkuwahi kuniskia kulalamika kwako hata mara moja.


Nadya naumia kuona kuwa hutokuja kupata mwanaume mkarimu na mwenye huruma kama Mimi na usimdharau mtu Kwa umakini wake jali utu pesa majumba magari ni vyakupita lakini upendo wa kweli unadumu milele na hauwezi kufutika.


najua umebadirika sababu ya kua mwanaume wake ambae ulisema amekusaliti amekuambia kua anarudi na nikiona hiyo meseji ukiisoma lakini sikutaka kumuhuliza chochote sababu tayari nikishajijengea akilini mwangu kuwa. maskini Hana kauli Kwa mtu mwenye pesa japokua nilikua naumia mara mbili kwa kumsaliti mpenzi wangu na wewe kunisaliti Kwa kila nilichokifanya kwako Nina mengi ya kuyaeleza ila sitaki kukuchosha nakutakia Maisha mema na yenye furaha na mpenzi wake kwaheri Nadya"


Nadya alipomaliza kusoma huo ujumbe kwenye karatasi na Kila kitu alichokisema Suma kilikua Cha ukweli hivyo ilikua inamuumiza sana maana hata yeye tayari alikua anampenda sana Suma.


lakini akiwa analia na kuumia moyo wake alikua anarejesha Kila kitu kwenye sehemu yake husika na mara Ghafla mlango ukaanza kugongwa Nadya haraka akatoka sebleni kwaajiri ya kufungua mlango na Baada ya kufungua mlango hakuamini macho yake.




upande wa Suma na Aisha Suma alikua anatetemeka Kwa hasira na Maumivu mbele ya Aisha akiwa ameinamia chini Suma akaanza kuongea


"Aisha najua nimekuumiza sana lakini hukuwahi kumtupa mama yangu ulimoenda na kumrinda na kumuheshimu lakini Mimi nilikua mbaya kwako Aisha lakini naomba unisamehe sana kwa nitakacho kueleza Aisha"


Aisha alikua anaumia sana moyoni mwake na alihisi tu kitu kibaya hivyo alimwambia Suma


"hapana sitaki kuskia Chochote kutoka kwako Suma usije kuniumiza bure"


"Aisha Mimi kuzungumza na wewe ni kama naondoa kitu kizito moyoni mwangu naomba unisikilize Aisha"


Aisha alikua anaumia sana na kutamani hata kulia sababu walipokua kijijini waliokua wanakua wote na kubembelezana pamoja ikitokea tu pale ambapo wamekoseana,lakini Kwa awamu hii Aisha alikua hataki kuonesha udhaifu wake mbele ya Suma.


Suma akizungumza Kila kitu kilichotokea na alichokifanya kitu ambacho kilimuumiza sana Aisha na kuamua kuingia ndani akiwa analia kwa uchungu sana( acheni tu nyie Maumivu ya mapenzi kwa aliekusaliti yanauma sana)


Suma alimkimbilia na kumshika Aisha aweze kumsamehe Aisha nae alimsimulia Kila kitu kilichotokea kijijini ya kutaka kubakwa na pia kuhusu mwenyekiti wao pia nayo Suma ilizidi kumuumiza na kujutia kumuacha Aisha wake.




walikua wamekaa kwenye sofa wakati huo wote walikua wamekaa vyakutosha sana mama yao akawambia


"najua wote mmepitia nyakati mgumu Kila mmoja Kwa wakati wake lakini Suma ulichokifanya sijakipenda hata kidogo kumsaliti mwenzio lakini naomba sana Aisha umsamehe mwenzio kama kosa tayari amekiri kikubwa ni wewe kumsamehe mwenzio"


Aisha akasema


"Suma Sina kinyongo na wewe nimekusamehe kuwa na amani kuanzia sasa pia karibu sana"


Aisha Baada ya kusema hivyo alisimama na kuondoka zake kuelekea chumbani kwake.


mama yake Suma akampa ishara mwanae kuwa amfate Suma alifanya hivyo akamkimbilia Aisha chumbani na wakati anafika mlangoni tayari Aisha alishabamiza mlango wa chumbani.


Suma alimuomba sana Aisha afungue mlango lakini Aisha hakufungua mlango.




alichukua simu yake na kumpigia Dani na kumwambia afanye mlango wa tiketi ya ndege na kwakua ilikua mapema Dan alimnunulia tiketi haraka kupitia mtandaoni Kisha akamwambia ipo tayari ndege ya sa12 asubuhi Aisha alianza kupanga nguo zake kwenye begi na Kisha akapanda kitandani kulala japokua ilikua ngumu sana kwake kupata usingizi lakini alijilazimisha Hadi akapata usingizi.




upande wa Nadya pia mpenzi wake alipomuona akamuhuliza


"vipi mpenzi hujafurahia kuniona? hujanimisi?"


"aah hapana karibu ndani basi"




aliingia ndani Nadya akamuhuliza


"nikuandalie Nini ambacho utakula sasahivi?.."


"noon baby inamaana umenisahau kabisa Nadya wangu sikia me nishakula tayari yaani hapo usinizungushe mwenzio nimekumiss saña eti"


kabla ya Nadya kuongea Chochote tayari alishavamiwa na kumpelekea chumbani mambo yalibamba ipasavyo...




asubuhi mapema Aisha aliamshwa na mlio wa simu yake alipitazmaa mpigaji alikua Dani akaamka haraka na kujiandaa Kisha akatoka na begi lake bila yoyote kushtuka alipofikia sebleni akamkuta Suma amelala kwenye sofa akamuwekea karatasi karibu yake na kuondoka zake.




Suma aliamka na kukutana na karatasi akaisika na kuanza kuisoma


"mpendwa Suma 


   natumai ni mzima wa afya kwanza kabla ya yite nisamehe sana kwa kutokufungua mlango usiku wa Jana najua umejiskia vibaya sana ila sikua na chaguo kingine,tukiachana na hayo Suma nakupenda sana sana nimeamua kuondoka sababu Sina chaguo lingine la kufanya kwasasa nimeamua kujitenga mbali na wewe sababu sitaki kuiona sura yako kwasasa Kila nikikuona nakumbuka mamno mengi yaliyotokea baina yetu hivyo nataka kukaa mbali nawewe Kwa kujipa muda angalau lakini nataka utambue kua nakupenda sana Suma mpenzi wangu mumewangu,


nimeacha funguo za gari chumbani na simu pia ambayo utaitumia na tutakua tunawasiliana kama utahitaji Kila kitu kipo ndani kama utahitaji msaada wowote Kuna namba nimesave Dan utamcheki niagie na mama kwaheri.."


Suma Baada ya kumaliza kusoma ule ujumbe alipandwa na hasira sana na kuanza kupiga kelele za hasira Hadi mama yake akatoka chumbani kutaka kujua Nini kinamsumbua Suma alipiga magoti kwenye miguu ya mama yake huku akilia sana kumwambia kua Aisha ameondoka .


taarifa zile hata mama yake zilimuuma sana kwanini aondoke.


je unadhani itakuaje usikose itaendelea...


PENZI LANGU 12

Nyumba ilipoa sana Baada ya Aisha kuondoka Kila mtu alijua anamawazo juu ya Aisha atakua wapi na atakua anafanya Nini Suma alikuaa anamawazo sana mama yake akamwambia


"Suma mwanangu kwanini tusirudi Kijijini kwenye Maisha yetu ambayo tumezowea kuishi nimechoka kuishi Maisha haya yasiokua na furaha Kila siku Maumivu yasiyoisha"


"mama usiseme hivyo Aisha ananipenda saña na amefanya hivi Ili kuupima tu moyo wangu naomba kuwa na Imani nae atarudi tu mama"


"mwanangu sasa huna kazi utategemea vitu ambavyo ameacha mwanamke kweli?"


"mama sio hivyo hata nilipokua nakaanilikaa Kwa akili na tahadhali pia najua nilifanya kosa la kuchukua pesa pasi na mwenyeewe kuniruhusu lakini niliirejesha kama ilivyo Baada ya kufanyia kule nilichohitaji mama na sasahivi Nina pesa ya kuanzisha kabiashara"


"ooh kweli mwanangu?"


"ndio mama"


"Sawa basi usichelewe kuanza kumfanya biashara maana huwezi kukaa tu kwenye hii miji ya watu"


"Sawa mama nitaanza kumfanya hivyo"




Suma na mama yake walianza kumfanya mpango wa kumtafuta sehemu ya kufanyia biashara,huku upande wa Nadya Sasa mambo yalikua moto penzi paja pika pakua na mpenzi wake akamsahau Suma Kwa haraka sana.




siku Moja wakiwa wamekaa kwenye bustani Nadya akiwa amelala kwenye miguu ya mpenzi wake ambae hata jina lake Bado halikua limetumika mara Ghafla alijiskia vibaya alihisi mvurigano wa ajabu na kujihisi anataka kutapika hivyo alisimama na kusogea Kando kwaajir ya kutapika.


mpenzi wake alimfata na kumuhuliza


"unajisikia vibaya sana mpenzi?"


"hapana nimejihisi tu tumbo linauma nikajikuta natapika tu"


"pole sana twende hospital basi"


"hapana isaya Niko sawa"


"basi Sawa hakuna shida"


isaya alirudi kwenye kimkeka na kukaa huku akichezea simu yake Nadya alisigea pale alipokaa isaya na kumkuta anatabasam akamuhuliza


"mbona unatabasamu hivyo?"


"aah usijari mambo ya mitandao tu mwenyeewe SI unaelewa mpenzi,haya njoo ulale mana napenda saña kushika nywele zako"


Nadya akajiskia Tena Ile Hali na haraka akaenda kutapika Tena isaya aliingia ndani na kutoka na funguo za gari na kumwambia


"tunaenda hospital usitake homa ikuzidie usiku tukaanza kusumbuana siwezi kuamka usiku kukimbiziana hospital"


isaya alimshika mkono Nadya Hadi kwenye gari Kisha akawasha gari na kuelekea hospital.




Baada ya kumfanyia vipimo vyote na majibu yalitoka kuwa Nadya mjamzito wa mwezi mmoja na wiki moja,isaya alimtazama sana Nadya na kumwambia kwa hasira


"nilikua hili kabla Nadya sababu marafiki zangu waliniambia kua wewe uniliki mwanaume ndani na ndiomaana hata siku ya kwanza wakati tunafanya tendo nilihisi utofauti mkubwa saña sikutaka kukuambia sababu najua wewe ni binadamu pia una hisia zako lakini hili suala la kupata mimba Mimi siafiki hata kidogo mama wee"




isaya alikuaa anahasira sana akamshika mkono Nadya na kumuingiza kwenye gari na kurudi nae nyumbani kwake na Kisha akaingia Moja Kwa Moja chumbani kwake na kutoka na begi Kisha akamwambia


"Nadya kama nilivyosema siwezi kurudia tena,nilikufamyia mpango wa kazi kwenye kampuni ya rafiki yangu na pia nilikua pesa nyumba na magari matati hayo hapo nnje lakini hukutaka kunivumilia Sasa basi naondoka zangu na usahau kama ulikua na mwanaume ambae aliitwa isaya akakuthamini na kukupa Kila kitu kwaheri"


"isaya naomba nisamehe naweza hata kutoa hii mimba Ili ubaki na mimi"


"unataka kumfanya mauwaji Tena,kama unataka kutoa mimba uananidhihirishia kua unaroho mbaya sana hata Mimi unaweza kuniua pia Wacha niondoke"




safari hii isaya alichukua nguo zake na kila kitu chake vyote na kuondoka zake,Nadya alibakia na maumivu yasiyopimika moyoni mwake.




upande wa Aisha alikuaa na siku kadhaa huko ulaya lakini pia alipokea na watu ambao hawafahamu na walikua nae Kwa wiki nzima bila ya kumwambia chochote ikabidi awahulize Kwa kutumia lugha ya kingeleza sababu alikua amesoma Hadi kufika chuo na matatizo yaliyotokea yakamfanya yeye kuacha chuo.


"kwanini mmenileta hapa nani amewatuma?"


mmoja akatoa simu mfukoni na kumuonesha Aisha Aisha alimuona Dana akamuhuliza


"Dan kwanini unanifanyia hivi lakini?,muda wote nipo tu ndani kwahiyo nimeletwa Huku kama mateka au?"


jibu lilitoka upande mwingine ambapo waliingia mwanamke na mwanaume na kitoto kidogo Cha kiume Aisha alishtuka sana na kusema kwamshangao mkubwa sana




"hii inawezekana vipi mama ,baba ,harisi...?"


baba yake akazungumza


"inawezekana sana mwanangu kwauwezo wa Mungu"


Aisha alisimama na kuikumbatia familia yake huku akitoa machozi ya furaha saña Kisha akawahuliza


"mama ilikuaje Yani mpaka mkawa hapa?"


"Aisha mwanangu ni story ndefu Sana ila ni kwa msaada wa Dani pekee"


"inamaana Dani ndie ambae amewasaidia na wale ninani ambao wameuwawa?"


"Aisha Binti yangu usiwe na wasiwasi kuhusu sisi okay? sisi tupo salama kama alivyosema mama yako ila Dan ndio msaada wetu mkubwa sana alimteka harisi na kumpeleka mafichoni pia akawateka watu ambao wanafanana na sisi miili na Kisha akawatengenezea sura ambayo zinafanana sura zetu Kisha hao vijana waliomtumia Dan Kwa kumripa pesa waliwauwa na kwenda kuwafukia mbali sana na wewe hakuweza kukusaidia kutokana na Hilo jambo lilikua la Ghafla sana pia kukuteka wewe alitumwa mtu mwingine"


"aah mama poleni sana lakini namshukur sana Mungu kwa miujiza iliyotokea kwenye mama lakini hata hao waliokufa ni wazi wa mtu pia na Nina hakika kua Dan atanipa taarifa zote kuhusu hao watu"


"unatakaj kumfanya nini Binti?"


"Hamna baba kua na amani tu"


basi pale walipiga story nyingi Kisha wakapata chakula Kwa pamoja kama familia Kisha wakaingia ndani kwaajir ya kulala lakini kabla Aisha hajalala mama yake aliingia chumba I kwake na kumwambia


"Binti yangu nani alikuokoa na ilikuaje hasa?"


"mama waliniwashia moto mkubwa sana kiasi kwamba walitaka kuniuwa Kwa Maumivu na mateso ya ajabu lakini alitokea kijana mmoja na kuniokoa huwezi Amin mama kulikua na watu wengi ambao walikua wanashuhudia msitu ukiungua lakini hakuna aliyesogeea ziadi ya huyo mkaka nikawa naishi kwao nilisahau matatizo yote sababu yake alikua mkarimu sana yeye na mama yake na nikajikuta nampenda na Baada ya kumuelezea kuhusu hisa zangu hata yeye hakuzipinga akakubali kua na mimi ukweli nampenda sana"


"Sawa nafuraha sana kusikia hivyo lakini mwanangu kwanini tusiishi hapa kuondoa hatari iliyopo maana najua Kila kitu vyetu kizuri na kikibwa kipo kule lakini hivyo vitu sio kitu muhimu kama roho zetu"


"mama nafahamu lakini tayari Niko na familia mpya mama na siwezi kuisahau au kuiterekeza mama"


"inamaana sie sio familia yako tena?"


"hapana mama sio hivyo na simaanishi hivyo lakini niliishi na Ile familia Kwa upendo sababu niliamini kua nyie tayari hamko duniani mama"


"lakini tupo Aisha"


"mama nenda kalale Bado nitakuepi na Kila siku nitakapokua hapa nitapata kuyajua maizngira huku nikiwa nayaka kufanya maamzi yangu basi nitawashirikisha"




mama yake Aisha alitoka chumbani Kwa Aisha na kumuacha mwenyew Kisha aisha alichukua simu yake na kumpigia Dan walipiga story nyingi sana Kisha akamuhuliza kuhusu kutafutwa na mtu yoyite lakini akamwambia hajawahi kutafutwa na mtu wowote Aisha alikataa simu na kumpigia simu Suma na Kwa bahati Suma alikuaa mtandaoni akaona namba ngeni akapokea ilikua video call akamuona Aisha wake alifurahi sana na haraka akaelekea jaribu na mama yake a kuanza kuzungumza nae Kwa furaha.


Aisha alimwambia kua amewakumbuka saña kitu ambacho kikiwarudisha kwenye matumaini mapya kuwa Aisha tayari ameshasahau yite na kutaka kuanza upya Suma akamuhuliza


"uanrudi lini Aisha wangu maana nimekumiss saña mkewangu"


"Suma siwezi kurudi Hadi nione umebadirika"


"Aisha Mimi mbona nimeshabadirika mpenzi wangu angalia tayari nimekonda Kwa kukosa kukuona Kwa zaidi ya wiki sasa"


"Suma acha utani wako"


"fanya urudi uniponye maradhi yangu Aisha"


"Suma nataka kulala sasa Bai"


"Aisha .usikate simu Kuna kitu nataka kukwambia"


"Suma kitu Gani Tena?"


"Nakupenda sana Aisha naomba tuanze upya mkewangu najua nimekukosea lakini makosa furaha kabisa nisipokua karibu na wewe nielewe mpenzi"


Aisha alijikuta anatamani kupaa na maneno ya Suma yalikua matamu ya upole sana hapo ndipo alikua anammaliza sana Aisha,akajikuta anamwambia kua anampenda pia na atarudi siku sio nyingi Suma alipigwa kelele za furaha sana na Aisha akakata simu na kuikumbatia Kwa furaha saña.


Maisha yaliendelea kua ya furaha Kila Baada ya kuzungumza kati ya Suma na aisha.




upande wa Nadya alikua anapitia mateso sana ya kumkumbuka Suma na Huku isaya alishafanya maamzi ya kumuacha Nadya maana hakutaka kutulia na mwanaume mmoja.


Kila siku ilikua ya Maumivu na mateso sana kwake ilifika hatua hata kazini hakua akienda kutokana Hali ya mawazo aliyokua nayo.


Nadya alianza Kwa kuuza magari Yake mawili na kubaki na gari Moja tu.


Siku zilienda na hatimae miezi Tisa ikatimia na Nadya alijifungua mtoto wa kiume mzuri sana ambae alifanana sana na Suma.




alikua anaishi mwenyewe na mtoto lakini Bado alikua anammiss sana Suma.


Aisha alirudi ulaya Kwa saplaizi ya kushtukiza siku Moja Suma alikua anajiandaa kwaajir ya kwenda kazini kwake lakini alipofungua mlango hakuweza kuamini kumuona Aisha wake alimkimbilia na kumbeba Kwa furaha sana Kisha akamshusha na kumkumbatia na kumwambia


"namshukru sana Mungu kua umerudi salama"


"nafurahi kukuona Tena Suma,lakini unaenda wapi?"


"nilikua naenda kwenye baishara yangu lakini siendi tena nataka nishinde na wewe tu mkewangu"


Aisha alitabasama sana akataka kubeba begi lake Suma akamtuliza na kumbeba Hadi kwenye ngazi ya kuingilia ndani Kisha akarudi kuchukua begi la Aisha na kumshika kiuno Aisha wake na kuingiwa nae ndani mama yake alipomuona Aisha alipiga vigelegele vya furaha akamkumbatia Aisha na kumwambia


"ni vema kuwa umerudi maoema maana nilikua nasiku chache nataka kurudi kijijini"


Aisha alimgeukia Suma na kumgeukia mama yake pia Kisha akamuhuliza


"kwanini urudi kijijini Tena mama?"


"sikua natarajia kama ungerudi Aisha ulitoka ukiwa umekasirika sana"


"mama ni hasira tu ambazo Kila aliyeumia huwa nazo lakini tayari tumeyamaliza na nimekuja kuishi na Suma Kama mke na mume"....


usikose itaeendelea...


PENZI LANGU 13

Suma na Aisha walikua na furaha sana sababu walikua wanafanya Kila kitu Kwa ushirikiano sana,aiku nyingine walikua wanatoka na kwenda Kwenye biashara wakiwa pamoja na watu wengi ambao walikua wanamfahami Suma Kwa muda mfupi hawakuacha kuwasifia kua wanapendezana sana wakiwa pamoja kitu ambacho kiliwafanya kuzidi kupendana zaidi.




siku Moja wakiwa wanarudi nyumbani ilikua tayari majira ya usiku sana Aisha akamwambia Suma


"alafu baby unajua sahivi nachoka sana kwahiyo sasahivi sitakua nakuja dukani kwako nitakua nyumbani na mama"




"Suma mkewangu hua napata Hali flani ya furaha pindi napokua nawewe dukani,au zile bidhaa ndo hua zinakuchosha"


"hapana baby nikwamba tu nahisi ni kwaajiri ya kukata mda mrefu pale ndani bila kujinyoosha afu pia baby naomba niendelee kufanya mazoezi kama mwanzo"


"ooh Hilo halina shida lakini tutajua tunafanya wote kabla ya kwenda kazini kwangu"


"Suma jamani..!."


"niite mumewako sio Suma Tena"


"Sawa mmewangu"


basi walipiga story nyingi na kupanga mambo mengi sana Hadi wanafika nyumbani kwao.




waliingia ndani na kumkuta mama Yao kama kawaid yake anapenda sana kufatilia tamthilia , walimsalimia kisha Aisha akaingia chumbani Suma pia alimuaga mama yake kua anaenda kuoga kisha aje kula chakula Suma alipoingia ndani akamkuta Aisha amejilaza kitandani akamuhuliza


"enhe vipi kujilaza hapo umeoga na kuhusu kula pia?"


"baby yaani sijiskii kula Chochote Wala hata kuoga pia"


"hee we Aisha amka bwana tukaoge wote basi maana wewe unataka kunifanya me mjinga"




Aisha aliamka na kwenda kuoga pamoja na kipenzi chake baada ya kutoka bafuni Suma alimlazimisha sana aende kula lakinia Aisha alikata Suma alitoka sebleni na kukwambia mama yake kuhusu Aisha mama yake akamwambia


"sio Hali ya kawaida na hafanyi kusudi Kuna kitu kinamsumbua"


"mama kitu Gani hiko mbona me nahisi kua ananidekea tu?"


"hapana Aisha sasahivi ni mjamzito lakini mwenyewe hajakua sababu hajawahi kubeba mimba na HII Hali wengie wanakua Bado hawajajua sababu ya kuwa mara ya kwanza kubeba mimba"


"mama unataka kusema Aisha ana mimba yangu?"


"shiiip usiongee Kwa nguvu hivyo Sasa ataskia,Sasa skia sitaki huyo mtoto azaliwe nnje ya ndoa nataka umuoe Aisha mwanangu mmekaa Kwa muda mrefu sana lakini tudhihirishe kama tayari ni halali kwako"


"aaha mama Hilo mbona halina shida nitazungumza nae na litakwisha tu"




Suma alichukua chakula na kuingia nacho chumbani kwaajiri ya kumlisha Aisha maana alikua hapendi kabisa kula chakula, alipoingia chumbani akamkuta tayari Aisha ameshalala alimwamsha hivyo hivyo na kujaribu kumpa chakula Kwa kufosi Hadi akatapika Aisha akamwambia Kwa ukali


"kwanini unilazimishe kula wakati sitaki Suma ona sasa ukijiona nimechoka usinichoshe Suma"


.Suma aliweka chakula pembeni na kumsafisha Aisha kisha akamwambia


"nisamehe sana mkewangu Kwa kukulazimisha kula lakini nataka ule uwe na nguvu usipokula utakuaje na nanguvu na hiyo...unatakiwa kula"


"niwe na nguvu ya Nini Yani Kwani hapa Sina nguvu?"


"basi mpenzi nisamehe sana naomba nikukumbatie mpenzi Ili upumzike"


Aisha anavyopenda kudeka Sasa hakujibu chochote akalala Kwenye kifua Cha Suma huku akiwa anatabasamu,Suma alijiwazia sana na kusema


"mmh kama kuishi na mjamzito ndo hivi yataka moyo sana ehe ni hatari sana"




basi walipitiwa na usingizi.lakini wakati wengine wanalala wakiwa na furaha lakini upande mwingine ni hali ya tofauti sana,Nadya alipojifungua aliambiwa ameathirika na virusi vya ukimwi na hakujua hivyo virusi amevioata Kwa nani maana ametoka na wanaume tofauti hivyo hakutambua nani nzima nani mgonjwa lakini mawazo yake yalimuondoa kabisa Suma sababu jinsi alivyokua anamuona Suma ni mwanaume wa tofauti mwenye kujari sana na mwenye hisia na malengo ya kweli hivyo Moja Kwa Moja hakutaka kunshutumu Kwa Hilo na wazo lake Moja Kwa Moja likadondokea Kwa isaya hivyo akimlaani sana isaya kwa kurejea kwake.


muda wote alikua ni mtu mwenye kilio na mwenye maumivu sana alitamani kumpata Suma lakini alivyoondoka alimwachia Kila kitu chake hadi simu na hakua anajua kama Kwenye simu ambayo alikua anatumia Suma kilikua na namba za marafiki zake Hilo hakua anajua hivyo ndo ilizidi kumuumiza.




na kama kawaida ukiwa unawaza mambo mengi lazima wazo Moja utakubaliana nalo hivyo asubuhi mapema Nadya aliamka na kujiandaa Kisha akamchukia na mtoto pia akamuweka Kwenye gari na kutoka nae.




safari yake ilikomea Kwenye car wash ambayo walikua wanafanya kazi Suma na wenzake alipaki gari kando wakati anasogea Kwenye eneo la ndni Kwa kuangalia labda atamuona mtu yoyote mara akasikia sauti Kwa nyuma


"madam mbona umepaki gari mbali isogeze ndani tulioshe".


"hapana ndugu yangu sijaja kuosha gari Kuna mtu nimekuja kumuhulizia au kuwahuliza"


"nani huyo?"


"Kuna kijana mmoja alikua anafanya kazi hapa anaitwa Suma na mwingine anaitwa juma mwingine anaitwa Ra..rama kama sikosei unawafahamu?"


"madam hàyo majina Kwa hapa sijawahi kuyaskia"


Nadya alizidi kuumia na aliweza kukubaliana nae mapema sababu aliona mabadiriko makubwa sana pale hivyo hàyo majibu ya huyo kijana yalimwaminisha Moja Kwa Moja kuwa hao vijana hawawezi kubaki Tena hapo wakati tayari wenye pesa washaingilia kati hivyo ikabidi tu ageuke na kutaka kuondoka lakini Ghafla akaisika sauti nyingine Kwa mbali..


Kwa upande wa Aisha na Suma pia waliamka mapema sana na walikua wanafanya mazoezi ya kukimbia lakini Aisha alivyokumbuka kuwa alitaka kugongwa na gari akamwambia Suma


"baby wakati nafanya haha mazoezi mwanzo nilikoswa na gari na mdada mmoja hivi sasa Kwa tahadhali naomba tuwe tunaenda kufanya mazoezi pale gym"


"Aisha gym Tena jamani ila Sawa kama upendavyo lakini sio Leo Tena"


"Bado muda baby tafadhali twende"


Suma hakutaka kumkasilirisha Aisha hivyo walienda hapo gym na kuanza kufanya mazoezi mara Aisha alimuona Samuel haraka akazima mashine na kwenda kumkumbatia Samuel na kumuhulza


"Samuel ulipotea machoni mwangu"


"aah Aisha Mimi nipo hapa Kila siku wewe ndio ulziba kabisa kuja hapa na Kila nikipiga simu Yako Iko bize tu"


"nikweli kabisa lakini Leo nipo na mumewangu hapa anaitwa suma,baby huyu ni rafiki yangu ambae aliniokoA Ile siku ambayo nilitaka kugongwa"


"ooh asante Kwa kumuokota Aisha wangu"


"usijari ilitokea wakati me nimeona hivyo ikabidi tu nimsaidie"


basi walipiga story nyingi Kisha aisha na Suma wakaondoka lakini wakiwa Kwenye gari Suma akamwambia


"Aisha sijapenda kumkumbatia yule kijana"


"ooh umeona wivu?"


"ndio na sitaki ijirudie"


"basi Sawa nimekuelewa na sitarudia Tena baby"


"ohk sawa lakini Aisha kwanini tusifunge ndoa tuishi Kihalali kama mke na mume?"


"ooh Sawa hilo halina shida baby ni wewe tu ila sitaki ndoa ya sherehe sitaki kuona watu wengi macho yangu yana aibu sana"


"usijari kuhusu hilo nitashughulikia"




mambo ya Suma na Aisha yametaradadi huku kwa Nadya mambo magumu sana..


baada ya nadya kusikia Ile sauti aligeuka na kumuona juma alifurahi sana na kutamani hata kumkumbatia lakini hakuweza sababu ya mambo flani juma akamuhuliza


"madam ukatususa kabisa au ulisafiri?"


"juma Nina mazungumzo marefu na wewe naomba kama hauna kazi twende Kwenye gari tukazungumze"




juma hakua mbishi walifatana huku wanapiga story za zamani huku wakielekea Kwenye gari


waliingia Kwenye gari jua alimuona mtoto akashtuka na kumuhulza


"madam huyu mtoto wako?"


"ndio ni mtoto wangu"


"hongera saña ni mzuri sana"


"ndio kafanana sana na baba yake"


"Sawa madam niambie"


"juma kwanza naomba sana unisamehe sana kwasababu nilieafanya kuwa Kwenye wasiwasi mkubwa sana baada ya kuniondoa rafiki yenu kwenu, namaniisha kua nilikua naishi na Suma nyumbani kwangu kama rafiki na mwisho wa siku tukaanzisha mahusian ambayo yaliota mizizi Hadi kupelekea kunipa zawadi ya huyu mtoto lakini..."




"madam inamaana ulikua uanishi na Suma pika pakua?"


"ndio juma yaani alikua kila kitu kwangu na nilimpata baada ya Ile siku kuagana na kaka yake sijui kua anakuja kumchukua lakini hakuja nilipita hapa nikamluta amekaa mwenyewe nikamsaidia kwenda nae kwangu lakini nikajikuta tu naanza kumpenda"


"ooh kwahiyo huyu mtoto wa Suma?,dah brother kajizaa kabisa Yani Sasa Suma Yuko wapi?"


"juma nimekuja kwako sababu nataka uniambie maana Suma aliondoka kwangu kwa hasira kutokana na nilikua simfanyii mambo mazuri na siku ambayo aliondoka sikua natarajia kama ataondoka lakini kuondoka kwake kumenipa mashaka sana sababu hakuwahi kutaka kutumia oesa zangu Kwa ufujaji na pia hakua na tamaaa hata kidogo na alivyoondoka ameacha Kila kitu ambacho nilimpatia ndio kitu ambacho kinaniaminisha kua Suma alikua kwangu kwaajiri ya mapenzi na sio pesa lakini sijamuona Tena"


"pole sana madam siku ambayo aliondoka alikuja kuniaga na kusema kuwa anarudi Kijijini kwao na alisema anaishi tabora sijui Kijiji Gani ila nilipojaribu kumuhoji alijibu tu kua amejeruhiwa".


"ndio nilimuumiza sana Suma lakini nilikua nataka kumpa taarifa kua anamtoto wake kwangu"


"hongera saña na pole lakini ameondoka kama alivyokuja hakua na simu Wala Nini.


Nadya alichoka sana baada ya kusikia vile.




Suma baada ya kumrudisha mkewake Aisha nyumbani kwao akaoga haraka na kuelekea kazini lakini akiwa njiani alikua na furaha sana akasema


"naijua kua Aisha hataki watu wengi Kwenye ndoa yetu lakini lazma marafiki zangu wake namba ya juma ninayo Wacha nimpigie nimpe taarifa hizi..


Suma alichukua simu yake na kuandika namba ya juma kisha akapiga iliita bila ya kupokelewa alipiga Tena pia haikupokelewa alipiga zaidi ya mara tatu lakini haikua na majibu yoyote Yale akaweka simu Kando na kuendelea kuendesha gari Ghafla simu yake ikaita na alivyopokea akasikia sauti ya Aisha idai kua amemmisi Suma alitabsam kisha akamwambia


"Aisha kipenzi nipo naendeshwa gari nikifika nitakupigia baby"


simu ilikatwa kisha Suma akasema


"mwaka huu mbona nitakoma na hii mimba..."


usikose itaeendelea....

Previous Post Next Post

نموذج الاتصال