PENZI LANGU 14
Suma alidika dukani kwako na kuendellea na biashara zake,alikuaa anauza duka la soea za boda boda magari biashara zaingine mbalimbali ila mwenyew alikuaa anakaa Kwenye duka la spea. |
upande wa juma na nadya walifika muafaka Kwa kumwambia atamtafuta Suma na akipata taarifa zake atamwambia Nadya alikubaliana na juma Kisha akaondoka zake na kumwacha juma Kwenye sintofahamu akiwaza kuwa inamaana Suma alikuaa anatembea na madam boss afu alikua hasemi kama ndie anaetembea nae.
juma aliamua kuondoka zake kuelekea dukani kwako maana hapo alifika kuwapa hai tu marafiki zake.
upande wa Aisha alikua amekaa sebleni na mama yake Suma walikuta wanapiga story zao mara simu yake ikaita akapokea
"hallow mambo Aisha"
"poa nani wewe?"
"Mimi Samuel uliniachia namba Yako baada ya kutokea gym"
"ooh samahani nilikua nimesahau kabisa vipi lakini uko poa?"
"Niko poa lakini nataka unisaidie kitu kimoja Aisha"
"kitu Gani hiko?"
mara Ghafla simu ikakata Aisha alimpigia lakini haikua ikipatikana akaiweka simu kando mama Suma akamuhuliza
"ninani huyo?"
"ni rafiki yangu alitaka kuzungumza kitu lakini Ghafla tu simu imekata"
"labda itakua imezima chaji"
"ndio labda"
basi wakiendelea na story zao lakini Ghafla Aisha alijiskia kutapika akatoka mbio mbio hadi nnje mama yake Suma alimfata na kumuhuliza
"Aisha unaumwa?"
"mama nimekua nikijiskia vibaya Sana Kwenye wiki hizi"
"twende hospital basi ukajue Nini shida"
"Yani mama ukizungumza mambo ya hospital Mimi napona kabisa Yani maana sitaki kabisa kwenda hospital"
"kwanini Sasa ,na ukikaa bila ya kwenda hospital utajuaje Nini kinakusumbua?"
"mama lakini Mimi..."
"nimegundua kua wewe ni muoga wa sindano ndiomaana hutaki kwenda hospital"
Aisha alicheka kidogo Kisha akamwambia
"mama mie hata siogopi sindano basi tu sitaki kwenda"
"hapana Aisha menda kajue tatizo Nini ukikaa bila ya kujua tatizo utazidi kujiumiza"
Aisha aliingia chumbani kwake na kumuacha mama Suma pale nnje alicheka Sana kusema mmh hizi mimba za kizazi hiki zinadeka Sana yaani hospital tu unakasirika hivi mmh sue enzi zetu ukifanya fyoko umebamizwa na mbao ya kichwa haijarishi unamimba Wala mtoto lakini sasahivi mmh lakini nashukuru Mungu mwanangu amenidhirishia kua yeye ni kidume Cha mbegu.
mama Suma alikua anazungumza mwenyeewe baada ya Aisha kuingia ndani.
Suma akiwa bize na wateja mara simu yake ikaita akachukua simu yake na kupokea Kisha kaunza kuzungumza
"oya juma mambo vipi ndugu yangu?"
"safi wewe ni Suma sindio?"
"ndio mzee vipi uko poa?"
"kidogo Sana Suma umeondoka zako umetuacha wapweke hutaki hata salamu ndugu yangu"
"hapana juma sikuwahi kuondoka maana dah..ila sikia juma nitakuja dukani kwako Leo si Bado upo pale pale?"
"ndio nipo pale pale,ila kama utakuja itakua vizuri Sana maana Nina jambo nataka kukushirikisha"
"poa basi nitakupigia simu badae"
simu ilikatwa na Suma alikua na Nuru na tabasamu zito usoni kwake.
upande na wa Nadya muda wote alikua anamtazama mtoto wake na kulia Sana Nadya akamsogelea mwanae na kumwambia
"najua unalia Sana mwanangu sababu ya kutomuona baba Yako lakini hivi karibuni tu utakutana na baba Yako naamini atafurahi Sana,baba Yako na naamini atakupenda Sana vumilia kidogo mwanangu"
Nadya alikua anazungumza kwa uchungu Sana Kila Baada anapomtazama mtoto wake na pia hakuwahi kumpa maziwa yake tangu alipomzaa Kwa kuogopa kumuambukiza maradhi aliyonayo.
muda ulizidi kusogea na hatumae ilikua yaoata saa mbili usiku Suma alimpigia simu juma na kumwambia kua anamfata juma alikubali na baada ya nusu saa Suma alifika ana ndinga yake akashuka wakasalimiana Tena Kwa mara nyingine wakiwa na furaha Sana juma akamuhuliza
"enhe umepata jimama jingine Nini naona mambo sio mabaya unaanza kunenepa Tena na vipi kuhusu safari ya kijijini?"
"juma ni story ndefu lakini wacha tu nifupishe sijapata jimama lingine ila sema yule mpenzi wangu wa kule kijijini alirudi mjini na kwao maisha safi kabisa hivyo kama bahati tu Ile siku ambayo nimetoka kwako hapa naelekea station nikakutana nae basi kilichoendelea mwenyew unajua"
"duh Suma unabahati Sana hivi umeogeshiea majani Gani mbona hiyo bahati siipati Mimi?"
"achana na hayo juma kwanza nataka kukwambia kitu kabla ya kuchelewa nikwamba nakuarika ndoa Mimi na mpenzi wangu tunataka kuowana mmewangu anaujauzito tayari hivyo amekua msumbufu Sana hakua anataka sherehe ila nimeona hata refiki zangu nyie nisiwapuuze"
"duh unataka kuowa Suma na yule mwanamke wako.."
"mwanamke wangu yupi juma?
"nakutania tu Mimi kaka nakutakia maisha mema na marefu na mkewako,mpendwa"
"Asante Sana lakini mbonahuna dalili ya kufunga hata duka hufungagi mida hii?"
"nafungaga sa 5 Hadi 6 huko"
"eeh sawa juma Wacha mie niende maana hapa simu unavyoona inaita muda wote ni yeye Huyu ameanza kunisumbua"
"eeh Suma we tutafutie na wenzio dawa tupendwe kama wewe sio vizuri"
juma alikua anazungumza kwa utani Kwa rafiki yake.
Suma aliaga na kuondoka zake na kumwacha juma akizidi kuchanganikiwa akawa anajihuliza
"nifanye Nini sasa maana kwanza namuonea huruma yule mtoto pia namuonea huruma huyo mwanamke aliyenae Sasa maana ni mpenzi wake wa zamani Sana na wetoka mbali Sana Hadi kufikia hatua ya kutaka kupata mtoto he akipata taarifa hizi maana inaonesha wazi kua Suma hajui Chochote kuhusu madam boss kama anamtoto wake aah nifanye Nini sasa mimi aah..!"
juma alikua anawaza nini chakufanya Kwaajir ya mashemeji zake,kweli kabisa ukiwa upande mmoja upande huu lazima ukuumize kichwa sasa juma alikua njia panda na haelewi Nini afanye na wapi atetee.
maisha yaliendelea hivyo hatimae Aisha na Suma walifunga ndoa Yao haikua na shrehe lakini ilipita salama majirani na marafiki walifika kuwasabahi na baada ya shughuli kuputa salama Kila mmoja akaondoka kwake.
baada ya siku kadhaa Suma akamwambia Aisha waende hospital maana tayari Aisha alianza kukonda kutokana na kutokula chakula Kwa wakati.walipofika hospital daktari akamchunguza Aisha Kisha akatoa majibu kua Aisha anaujauzito wa miezi mitatu na anatakiwa kuhudhuria kliniki haraka iwezekanavyo.
Aisha alishtuka Sana baada ya kuambiwa kuwa ni mjamzito baada ya kutoka Kwa daktari na kuingia kwenye gari Aisha alianza kulia Suma akambeleza na kumuhuliza kwanini analia Aisha akamjibu
"najua baadhi ya wanawake wanapoteza dira zao pindi wanapokua na ujauzito sababu wanaume zao wanakua bize na wanawake wengine naogopa Sana kuumia nikiwa kwenye Hali hii Mimi"
"Aisha wewe ni mkewangu na nimegundua kua mjamzito kabla na nilitaka tube hospital kwaajir ya kuthibitisha na wewe umsikie daktari Kwa maskio Yako,hivyo usijari Aisha wewe ni mpenzi wangu na nitakua na wewe kwenye shida na raha kama ilivyokua mwanzo nakupenda Sana huna sababu ya kuwaza Tena nipo karibu Yako muda wote Chochote unachohitaji nitafanya"
Aisha alimkumbatia Suma Kwa furaha Sana na kum'busu mabusu yasiyo na idadi Kisha Suma akawasha gari na kuondoka maeneo hayo.
baada ya kuambiwa kua anatakiwa kuanzia kliniki hivyo mwezi wa nne kwake ulivyoingia tu Ile siku ya tarehe Moja Aisha na Suma walijiandaa vizuri na kumuaga mama Yao Kisha wakapanda kwenye gari kuelekea kliniki.
na kea upande wa Nadya pia hiyo tarehe ilikua siku ya kumpeleka mtoto wake kliniki hivyo nae alijiandaa yeye na mwanae na kuondoka zake.
katika eneo la hospital upande wa kupimwa watoto Aisha alikua wakwanza sababu alifika na mumewake hivyo alikua wakwanza kwenda kumuona daktari.
baada ya kumpima daktari aliwapa ushauri ambao ulikua mzuri kufatwa na mama mjamzito kipindi chote Cha miezi tisa Kuhudhuria kliniki na mara baada ya kujifungia pia.
baada ya kumaliza kuongea Suma na mkewake walitoka Kwa daktari lakini wakiwa wanatembea kwenye korido waweze kufika kwenye sehemu ya kupaki gari mara ghafla Aisha alijiskia kutapika hivyo alimuacha Suma pale na kuelekea washroom.
Suma alisimama kwa muda hadi alihisi kuchoka ikabidi akae kwenye sehemu ambayo wamekaa wamama nawatoto zao ambao wabasubiria foleni ya kwenda kuwapima watoto zao mara ghafla alishikwa mkono na baada ya kufika sehemu yenye kificho alimuona Nadya akiwa na mtoto Suma akamuhuliza
"Nadya ni wewe kweli?"
lakini hapakua na maficho kiasi hiko wakati Suma anaendelea kumuhuliza Nadya baadhi ya maswali Aisha alirudi alipomuacha mmewake hakumkuta akamuhuliza mdada mmoja kamwambia kua Kuna mdada Ameenda nao huko nyuma ya Jengo, Aisha alipiga hatua Hadi kwenye nyuma ya Jengo Hilo akamuonya Suma akiwa anamshika Nadya mara mageuze sura yake mara amguse paji la uso kama anapima joto Nadya akamkabidhi Suma mtoto Suma alimpokea na kuanzia kumtazama Kwa makini huyo mtoto kweli alikua amefanana nae Sana Sasa alivyotaka kuzungumza kitu Kwa Nadya hakuwepo Tena pale,Suma alianza kutazama huku na huko lakini hakumuona wakati mambo yite hayo yanaendelea Aisha alikua anaona akaamua kurudi kwenye gari.
Suma alimtafuta sana Nadya lakini alivyotoka kwenye parking akaona gari la Nadya ndio linazama.
Suma alishindwa kujizuia kabisa kuhusu kile kilichotokea kwanza alikua anawaza nini atamueleza Aisha Hadi amuelewe na kwanini nadya aje kipindi hiko kigumu kwake ukweli alikua amechanganikiwa sana...
usikose itaendelea...
PENZI LANGU 15
Suma alisogea Hadi ilipo gari alifungua mlango na kupanda akamkuta Aisha ameshusha siti amejifanya amelala lakini hakua amelala hata.
Suma akitaka kumuamsha Aisha lakini Bado alikua anaogopa Aisha aliamka mwenyewe na kumuhuliza shida nini? na vipi mbona watoto Tena?"
"aah Aisha naomba tukazungumze nyumbani hili jambo"
"tuzungumze nyumbani huyu mtoto umempata hapa naomba nieleze hapahapa na kama vipi mpeleke huyu mtoto Kwa mama yake"
"Aisha nakupenda sana mpenzi wangu najua wewe ni muelewa sana naomba nielewe kipenzi changu"
Aisha alikua anaumia sana moyoni sababu alijua fika kua yule mtoto ni wasuma na Hana namna aliamua kushuka kwenye siti ya mbele na kukaa nyuma huku akilia sana,Suma hakujua Nini afanye kwaajir ya kumpooza Aisha akimtazama mtoto Bado mdogo ikabidi tu ambebe Ili aendeshe gari.
walifika nyumbani kwao Aisha alikua wakwanza kushuka kwenye gari na kuingia chumbani kwake na kujifungia mlango huku Suma akifata akiwa mtoto mama yake akamuhuliza
"Suma imekuaje mwenzio umemfanya Nini mbona amekua vile macho yamemvimba naoanekana wazi kua alikua analia na huyu mtoto vipi?"
"mama naomba nisaidie kwanza huyu mtoto,nimechoka sana"
mama yake alimchukua mtoto Kisha Suma akaelekea chumbani lakini Aisha alikua amejifungia Kwa ndani Suma alimuomba sana amfungulie alimwambia maneno yote mazuri mapenzi ni mapenzi tu nyie Aisha alifungua mlango na kumkumbatia Suma huku bado akiwa analia Suma alifunga mlango na kumsogeza Aisha wake kitandani na kumwambia
"najua unaumia sana Aisha lakini sikua nataka haya yote yatokee mpenzi lakini nilishindwa tu kujizuia naomba sana nisamehe"
"Suma unataka kunambia kua yule mtoto ni wako?"
"Aisha Kwa silimia zote yule mtoto ni wangu Aisha naomba nielewe pia nisamehe sana"
"Sawa Suma nimekuelewa na nimekusamehe sababu nakupenda sana"
"nafurahi sana kusikia hivyo mkewangu"
basi waliweza kumaliza tofauti Yao Kwa siku hiyo Aisha alikua anambeba mtoto yule vizuri na kuhakikisha kua anapata Kila hitaji ambalo anahitaji kupewa mtoto.
siku Moja Suma allichukua begi ambalo Nadya aliweka nguo za mwanae kwaajir ya kumbadirisha Suma alichukua na kumwambia kuwa ane da kununua nguo za kubadirisha mtoto wote walikubakiana nae lakini alipokua kwenye gari Suma alianza kupekua pekua kwenye baadhi ya mifuko na akakuta karatasi yenye walaka mkubwa sana ikabidi awe na shauku kubwa sana ya kutaka kujua walaka huo unahusu Nini akawasha gari na kutoka nalo nnje ya geti Kisha akapaki na kuanza kusoma
"kwako mpendwa Suma
kuondoka kwako keneye maisha yangu ilikua mateso makubwa sana kwangu najua nilikua nimekukosea sana kwa mambo niliyokua nayafanya lakini nilikua nafanya vile Ili ushindwe na uondoke sababu sikua na nguvu ya kukufukuza sikutaka ujiskie vibaya,najua kama umenichunguza umegundua mengi sana kuhusu mimi,Suma nisamehe kwa yote ambayo unajua ni mabaya kwangu na kusema ukweli nilikua nimekudanganya kua nimeacha a na mwanaume wangu haikua kweli japokua nikweli amekua akinisaliti alipokua huko nnje ya nchi na aliposema kua anarudi ndio nikaamua kukufanyia mambo ya ajabu na baada ya kurudi kwake sikuwahi kuwa na furaha hata kidogo sababu alikua mbinafsi sana na hakuwahi kuonesha kama ananijali alikua bize na wapenzi wake wa huko nnje japokua kabla ya kuondoka aliniachia baadhi ya vitu akanitafutia kazi nzuri lakini vyote havikutosha Mimi nilihitaji uwepo wake lakini hakuwepo nikaanza kutoka na vijana tofauti hatimae nikakupata wewe.
Suma ulikua mpole sana mwenye mapenzi ya dhati na sio mwenye tamaa ukweli ulistahili kuonesha heshima yako najua ulishanambia kua unamoenzi unaempenda lakini Bado sikutaka kushindwa kwako sababu nikiona kitu Cha tofauti Hadi nikiwa na wewe lakini nilijari sana pesa zangu na ubinafsi bila ya kujali moyo wako.
niachane na hayo kwanza nataka kuzungumza kuhusu mtoto Suma nilitelekezwa baada ya yule mwanaume kugundua kua Nina ujauzito na sikua na mwanaume mwingine zaidi yako nikaanza kukutafuta Kila sehemu lakini sikukupata mpaka nilipojifungua mtoto ndio alikua faraja yangu sababu sura yake ni Yako hivyo alinikua ananitazama sana pindi napokua nalia nilitamani kumtupa nafsi ikanisuta nikatamani kumpeleka kwenye vituo vya watoto yatima nafsi ikanisuta nikasema kua wewe upo hai kwanini usiwe baba baba Bora kwake nikamtafuta rafiki yako juma lakini nae alinambia kua hajui ulipo hivyo nikajipa Imani kua siku yoyote tunaweza kukutana na kukukabidhi mtoto wako.
Suma mlee vema mwanao huyo ni mtoto wako pekee Mimi nimeathirika sikutaka kumuathili na mtoto pia hata wewe usiwe na wasiwasi wewe ni mzima kabisa na nitabaki kukupenda siku zote Suma mtunze mtoto wetu aje kupata elimu Bora na maisha Bora pia kwaheri."
Suma baada ya kumaliza kusoma walaka huo alikua amechoka sana na Mara baada ya kumaliza kusoma ujumbe huo simu yake ikaanza kuita ba baada ya kuita alishtuka sana baada ya kupokea taarifa za msiba wa Nadya
alizidi kuumia maana tayari alishapoteza matumain.
kwkaua hakua mbali na nyumbani kwao aliingia ndani na kuwakuta Aisha na mama yake wamekaa na mtoto akiwa amelala Suma alimsogelea mtoto na kumbeba Kisha akamkumbatia Kwa nguvu sana kuhusu akitetemeka sana Aisha akamuhuliza
"Suma imekuaje huoni kua mtoto amelala,mbona hivyo?"
"Aisha mama huyu mtoto tayari yatima mama yake amejiua Aisha mama yake hyupo Tena duniani junior mwanangu ona mama yako amejiua junior wangu kwanini akuache ukiwa mdogo hivi kwanini lakini?"
Suma alilia kiume kiasi kwamba hata Aisha alishindwa kujizuia maana Suma alikua analia kwa hisia kalia sana.
siku zilienda mtoto aliendelea kujua vizuri sana na pia tumbo la Aisha pia lilikua kadiri siku zilivtozidi kusogea.
Aisha kwakua tayari alikua ameshawazoea rafiki zake na Suma siku Moja baada ya Suma tu kuondoka kazini Aisha alipanda kwenye gari nyingine na kuelekea dukani Kwa juma Kisha akamkuta juma na kupiga story baada ya hapo akawa anamuhuliza baadhi ya maswali juma alikua anamkubali sana huyo mwanamke kwanza mcheshi alafu pia anasifa ya upole had kwenye uzungumzaji wake hivyo juma alikua anajibu Kila anachohuliza mke wa Suma,basi Baada ya kumaliza jambo lake akamuaga na kuondoka zake juma akaanza kuzungumza mwenyewe kama kawaida yake.
"Suma akimpoteza na huyu mwanamke basi hatokuja kupata Tena mwanamke mzuri na mstaarabu kama huyu binti mrembo anazungumza vizuri eeh namimi Wacha niowe maana Kila siku nasifia wanawake za watu eeh Mungu nipe mwanamke mie hata ukinioa kulumbembe gegedu ilimradi tu heshima sitaki hata mwanamke mzuri Mimi nataka wa kuishi nae mwenye kujua thamani ya maisha na kuheshumiana tu"
mara akishtukiwa na sauti iliyoskika
"kaka kama kawaida yako unaongea mwenyewe tu yaani we utazeeka vibaya sana"
"aah rama we acha tu yani nilikua naongea na shemeji yangu Aisha hapa alikuja kuniona basi nimetokea tu kumpenda Bure yule dada mkarimu na mpole"
"aah mke wa Suma kile chombo mwanangu sana yaani ukizungumza nae tu kama hujapandwa na hisia je anapokua faragha Yani navuta picha tu hapa na ile suati ya kubembeleza"
"eeh juma basi acha kusifia sana hivyo"
"haya mwanangu lete story aah Sina story nimekuja kukuona tu umekua hadimu sana ofisini kwetu"
"aah Niko bize sana Yani..."
waliendelea kupiga story zao za kuhusu kazi.
siku moja usiku wakiwa wamelala na walikua wanalala na mtoto wao junior maana Aisha alikua anampenda sana,unajua Kuna kitu mda mwingine mtoto ankifanya Cha ajabu Hadi unajikuta tu unashangaa au unapata hisia za kitu flani hivyo usiku huo junior alikua amekumbatiwa na Aisha lakini Ghafla akajitoa na kusogea kwa baba yake na mara baada ya junior kusogea kando Aisha kuachukua hata dakika tano alianza kuhisi maumivu ya tumbo sana huku akitetemeka sana.
Suma aliamka na kumbeba Junior kumpeleka Kwa bibi yake kisha akambeba Aisha na kuelekea nae hospital.
baada ya kumpokea na kumpima akaonekana kua tayari muda wa kujifungia umewadia hivyo haraka wakaandaa vifaa kwaajir yake.
wakiwa Labor Aisha alikua anaugua kwamaumivu sana madaktari walimpa moto kua aendelee kua mvumilivu na kuweza kufata kile wanachomuelejeza daktari akamwambia
"bia Aisha jitahidi sana kuvuta pumzi ndefu kisha ishuhse Kwa nguvu kila kitu kitakua Sawa lakini ukiwa muiga utampoteza mtoto maana tayari ameshaanza kutoka..
Aisha alijitahidi saña na kuvuta pumzi kwa nguvu zote kisha akashusha Kwa nguvu pia mara alisikika mtoto akilia lakini Aisha alionekana hayupo Sawa kabisa madaktari walianza kuchanganikiwa sana maana Aisha alikua na hali mbaya sana macho yalikua yamemtoka sana na pia hakua akilia Tena Kwa maumivu Wala hata kufanya chochote hivyo hivyo alivyotulia ndivyo alivyo daktari akaweka mkono kwenye pua yake akashtuka na kumwambia
"hapumui Tena jamani fanya haraka tujaribu kuokoa maishaha yake".
haraka madaktari walishirikiana kwenye suala Zima la kumuwekea mfumo wa kupumulia na hapo sasa walianza akuona matumain wote walimshukuru mungu kwa kunyosha mikono yao juu kwa tabasam..
usikose itaeendelea....
PENZI LANGU 16
Baada ya madaktari kumaliza zoezi Zima la kumsaidia Aisha walitoka labor na kumkuta Suma akiwa nnje anasubiria majibu kuhusu taarifa yoyote mana wanasema ukiwa labor ni nusu mfu na nusu uhai kutokana na maumivu makali ambayo hupitia mama mjamzito pindi anapojifungua hivyo Suma alikuaa anasubiria kauli yoyote kutoka Kwa daktari japokua hakutamani kumpoteza yoyote kati Yao sababu alimpenda sana Aisha wake na alitegemea kupata mtoto mzuri sana na Aisha na mwenye sifa zote ambazo anazo Aisha.
wakati yupo pale nnje anaenda kulia na kushoto mbele na nyuma bila kuelewa Chochote mara daktari ambae alikuaa ameteuliwa kwaajiri ya kumsaidia Aisha alimuita Suma ofsini kwake.
"samahani kama naomba uje ofsini kwangu"
sumabhakupoteza muda alimfata Kwa haraka sana daktari,na baada ya kufika akamuhuliza kabla ya daktari kuanza kumuelezea
"daktari mkewangu anaendeleaje na vipi kuhusu mwanangu wapo sawa?"
"tulia ndugu yangu kama wamhekua natatizo nisingekua na utulivu wa kukuita ofsini muda huu ,lakini nimekuita hapa sababu Nina taarifa njema"
"Sawa daktari nakusikiliza lakini samahani kwa kua msumbufu"
"Sawa Hamna shida mana najua jinsi unavyojiskia ,ngoja niende Kwenye majibu Yako Moja Kwa Moja ,ni kwamba mkewako tumeweza kumsaidia kwa uwezo wa Mungu alifanikiwa kujifungua salama japokua Kuna tatizo lilitokea katikati ya safari lakini tumemsaidia na Sasa Yuko sawa kabisa"
"ooh asante Mungu wangu"
Suma alifurahi sana na kumshukuru daktari na kumuhuliza
"naweza kumuona?"
"Kwa sasahivi amepumzika lakini baadae utamuona akiwa Sawa"
Suma alitoka nnje akiwa na furaha sana alitoa simu yake na kumpigia simu mama yake kuwa Aisha amejifungua salama,mama yake pia alifurahi sana ,Suma alikata simu na kuanza kuwapigia rafiki yake hasa juma ndio alikuaa anamkubali sana maana juma ndie alikuaa mkaidi sana kwake..
ilikua usiku wakati mambo yite hayo yanaendelea,lakini Hadi kufikia asubuhi juma alikua tayari amefika hospital na baada ya kufika muda wa kupona wagonjwa Suma na juma waliingia wodini na kumkuta Aisha akiwa amekaa anacheza na mwanae.
Suma alipomuona mkewake alifurahi sana na na kutamani kumkumbatia lakini alikua ameshika mkono hivyo hakupata nafasi hivyo alimbusu mtoto na mkewake pia Kisha akamwambia
"pole sana mkewangu Kwa maumivu uliyipitia wakati wa kujifungua nilikua nakuombea sana ujifungue salama mkewangu"
"Asante mumewangu nahisi nguvu ya maombj Yako ndio yameniweka hai"
Suma alifurahi sana juma pia alimpa hongera shemeji yake na muda mchache tu mama yake Suma alidika hospital kumuona Aisha alimsalimia na kumpa pole Kisha akamwambia Aisha
"mwanangu Aisha pole sana hatimae Sasa umekua na uoga wote umeisha sindio mama?"
"Aisha alikua anaona aibu hata kumtazama mmewake juma na Suma wakaona kua mama Yao anataka kjwafukuza tu kimafumbo hivyo wakiwaacha mama yake na watoti wake wakiwa pale Aisha akaongea
"mama sikua najua maumivu anayopitia mjamzito lakini Jana mmh nimeona Wacha tu yani sijui kama nitazaa tena"
mama Suma alicheka sana Kisha akamwambia
"wakati wenzio tunaanza tulikua tunasema hivyo lakini mwisho wa siku tunaongea watoto maana Hali hii tunakua tumeshaizoea na haikimbiliki"
"Sawa mama nimemis junior wangu mlete kwanza"
walibadirishana watoto pale Aisha alimkumbatia junior yaani junior alifanana sana Suma yaani ukimtazama huulizi kabisa,ila mtoto wa Aisha alifanana sana na Aisha mwenyew sababu alikua wakike hivyo alifanana sana na mama yake.
baada ya kupiga story nyingi muda wa kutazama wagonjwa uliisha hivyo walitoka wodini na kumuachia Aisha na mtoto wake daktari aliingia na kumpima baadhi ya vipimo Kisha akamwambia
"presha Yako Iko kawaida Kwa Sasa na hauna shida yoyote Ile hivyo ikiendelea hivi Hadi jikoni tunaweza kukuruhusu"
"Asante sana daktari"
"usijari ila mtoto wako ni mzuri sana kama wewe mwenyewe"
"Asante "
daktari alitoka na kumwacha Aisha apumzike.
Suma na mama yake wakiwa wamekaa pale nnje wakijadiri mambo kadhaa juma aliweza kuwaaga na kuondoka zake Suma akabaki na mama yake na mwanae junior akazungumza
"mama natamani kufanya saplaiz kwaajir ya Aisha na mwanangu"
"unataka kufanya Nini?"
"mama nataka kumfanyia Aisha ajionee mwenye furaha sana akiwa na mimi hivyo nataka nifanye kitu kama Cha tofauti hivi kwake"
"mwanangu wala hata usijari fanya Chochote ambacho utahisi kitakua kizuri Kwa mkeo Mimi sina hata neno"
basi Suma aliwarudisha nyumbani mama yake na mtoto wake Kisha akatoka kuelekea kununua baadhi ya vitu akarudi navyo Kisha akaanza kusaidizana na vijana ambao alikua amewapata wakapamba Kwenye ukuta Kwa mauwa mazuri na Kila kitu vinavyohusika na mapambo Kisha baada ya kumaliza akawaripa hao vijana Kisha wakaondoka zao Suma akamwambia mama yake
"ni sherehe ndogo kwaajir ya mkewangu kabka ya 40"
"Suma ila usiwaarike lafiki zako iwe sisi kama sisi maana mtoto Bado kuonekana na watu tofauti Hadi amalize 40"
"usijari mama"
Suma alitoka na kuelekea hospital na Kwa bahati tayari Aisha alikua amelewa ruhusa hivyo alimsaimia baadhi ya vitu na kupeleka Kwenye gari Kisha Aisha pia alifika Kwenye gari Kisha wakaondoka zao.
walipofika Suma alimkaribisha mkewake kwa furaha sana Aisha alifurahi na kumshukuru mumewake lakini Kila kilichoandaliwa Aisha alijzuia kula hivyo walikuta wenyewe Suma na mama yake.
siku zilienda sana Hadi siku ya 40 wqkafanya kaaherehe ka mtoto walipata marafiki na baadhi ya majirani wengi sana na maisha mengine yakaendelea.
Aisha aliwapigia simu wazazi wake na kuwaeleza kuhusu kupata mtoto mama yake alilia machozi ya furaha sana na kutamani kumshika mjukuu wake Aisha alimuonesha mama yake mototo sababu walikua wanazungumza kupitia video call hivyo baada ya kumuonesha mtoto alikua amelala mama yake akamwambia
"mwanangu yaani alivyotulia kama ulivyokua wewe wakati uko mdogo mzuri sana binti yangu"
"mama sufa zikizidi utaaribu"
mara mdogo wake akachukua simu na kumwambia
"ndio dada wewe mzuri na jinis alivyomsifia mama mwanao kama mapacha natamani sana kucheza nae"
"usijari mdogo wangu nitakuja nae"
basi Baada ya kuongea mengi Aisha alikata simu.
alipotaka kuweka simu yake kando mara simu yake ikaita akapokea
"hallow Habari"
"safi naona namba ngeni"
"ndio ni Mimi Samuel za siku nyingi?"
"Samuel mbona umekua kama mzimu ndugu yangu,kwanza Ile siku nilikua Niko mskini kusikiliza lakini Ghafla tu ulikatika kwenye simu"
"nikweli ila nilikua kwenye misheni yangu muhimu na Sasa ni Kwa miezi kadhaa sijafanikiwa ila nataka tuonane niweze kukushirikisha jambo labda utanisaidia kitu,maana nimeshayimiza nusu ya jambo langu"
"Sawa Samuel ukiwa tayari we nijulishe nipo tayari kukusaidia"
simu ilikatwa na kumfanyia Aisha mwenye mawazo maana akikumbuka jinsi alivyokua anamtazama akawa anajihuliza tu mwenyewe
"au ananitaka Huyu mpuuzi,aah ila nilishamwambia kua Nina mumewangu na Alishamuona hivyo kama atasema ananipenda nitamkomesha hapo hapo.
yalikua mawazo ya Aisha kuhusu Samuel..
akiwa kwenye mzunguko wa mawazo hayo mara mlango ukafunguliwa akaingia Dan akasema saplaiz...
Aisha alishtuka sana baada ya kugeuka akamuonya Dan akamkumbatia Kwa furaha Kisha akamuhuliza
"we kijana ulikua wapi lakini mbona simu Yako ilikua haipatikani?"
"Aisha sikua nimekuaga sababu ilikua ghafla sana Ile umerudi tu wewe hapa siku ambayo nataka kuja kusalimia baba Yako akanituma mambo flani hivyo ikabidi nifanye hivyo Ndomaan sikuwepo"
"jamani Dan sijapenda yaani nimekosa msimamizi kwenye matukio memgi muhimu yaliyopita"
"nisamehe lakini Sasa nipo hapa kama babu wa Binti Yako,anaitwa nani kwanza?"
"anaitwa maira"
"wao waoo waoo Jina zuri kama mwenyewe Huyu Binti utasema kama hakunyi"
Aisha alicheka sana kwa mazungumzo ya Dan .
baada ya story tofauti aliamua kuaga na kuondoka zake.
upande wa Suma akiwa Kwenye mizunguko yake siku Moja ilikua mida ya jioni akiwa kwenye mitaa kadhaa akiwa na juma mara ghafla wakaona kvitu vinatolewa nnje na kutupwa huku mwanaume akimuomba sana baba mwenye nyumba amvumilie lakini huyo mwenye nyumba hakua na huruma Kabisa na hao watu Suma alipaki gari na kutaka kushuka kwenye gari juma akamshika mkono na kumuhuliza
"we unaenda wapi,hivi we umekua na huruma kiasi hiko eeh yule jamaa sindo alikua sikuile kukutukana pale kazini na kuturushia nguo zako japokua wewe ukuwepo ila sisi ndio tulishuhudia Sasa unaenda wapi?"
"juma ni sawa alinifanyia hivyo lakini bila ye ye kumbuka mimi nawewe tusingejuana na kumbuka yeye ndio alinipa chachu ya kuendellea kupambana"
juma alichukia sana maneno ya Suma alimuacha afanye anachotaka Suma alipiga hatua Hadi pale na kuwasalimia Kisha kuhuliza juu ya kinachoendelea,kwanza yule kaka alipomuona aliona aibu lakini mkewake alifurahi kuona ujio wake na kuchangamkia fursa.
alimsimulia Kila kitu Kisha Suma akiita gari ya usafiri na kupakia Kila kitu na Kisha wakaelekea kwenye nyumba moja nzuri sana ambayo walijenga tayari yeye na Aisha, walipofika akawambia.
"brother na shemeji mtakaa hapa Kwa muda Kisha nitawatafutia nyumba ya kuishi"
"Suma tunashukuru sana Kwa msaada wako bila wewe sisi tungezidi kudhalilika"
"shemeji usijari hata hivyo bila ya kaka hapa kunisaidia leo nisingekua hapa nasema Asante sana kwa kunipokea siku niliyokuja hapa jijini"
Suma alimtazama saa yake na kusema
"natamani kuwasaidia kuingiza vitu ndani lakini nimechelewa sana muda huu..
"usijari hapa tulipofikua tutamlazia sisi wewe wahi tu nyumbani"
Suma alitoa pesa kama elfu50 na kumkabidhi kaka yake huyo na kuondoka zake.
usikose itaendelea....
PENZI LANGU 17
Baada ya Suma kuondoka zake mkewake na yule jamaa akaanza kuzungumza
"mumewangu ona sasa kijana uliyemsaidia ukamuomdoa kwako Kwa hasira ona Leo ndio ametusaidia je angekua na moyo wa kutosamehe ingekuaje so angetucheka na kutudhalilisha?"
"kweli na Sasa nimeamini kua tenda wema uende zako usingoje shukran na sababu hujui kesho yako na Sasa nimeamini kua malipo ni hapa duniani,Leo bila Huyu kijana sijui hata ningekua mgeni wa nani"
"usijilaumu sana lakini pia Hilo ni funzo tosha usije kurudia tena makosa ambayo umeyafanya"
"kweli kabisa mkewangu nimeshajirekebisha"
upande wa Suma na juma walikua wanazozana tu
"Suma umeacha kunisaidia Mimi ambae Hadi Leo naishi nyumba ya kupanga unaenda kumsaidia yule jamanaa kusema ukweli Bado nitaendelea kukulaumu Kila siku"
"aah juma jamani usiwe hivyo rafiki yangu lakini nafanya Kwa kuripa fadhila tu kwao kwanini unakua hivyo pia binadamu tunasaidia hatupaswi kutazama makosa ya nyuma kuwa Nini kilitendeka"
"nishushe hapo Suma sitamani kuendelea na hii safari"
Suma alisimamisha gari na juma akashuka na kutokomea gizani Suma aliendesha gari hadi nyumbani kwao na baada ya kuwasalimia vipenzi vyake wakiwa wanapata chakula Suma akaanza kuongea
"mama na mkewangu nataka kuwaambia jambo Moja ambalo limetokea Leo najua sihawashirikisha lakini nataka kuwajuza kitu".
"kitu Gani hiko Suma?"
wote wakihuliza Kwa shauku ya kutaka kujua
"aah nilipofika hapa kuna brother wangu nilimsaidia kurekebisha gari yake na baada ya kuniona na kile kidurishi changu akajihuliza baadhi ya mambo nikamwambia kua mimi mgeni akanisaidia kunipeleka kwake nililla kwake siku Moja na siku ya pili akanipeleka kazini hapo ambapo nilikutana na juma na wale wengine na siku Ile nikijifanya kutaka kurudi lakini simuweza kupakumbuka ikabidi nirudi nilipotoka kabka ya kufika pale maeneo ya kazi walitokea vibaka na kunipora pesa ambayo nilitegema nitaamka nayo kwaajir ya chakula na sikua na jinsi basi nikarudi kulala pale pale palikua na baridi sana sababu hapakua na uzio wa aina yoyote Ile,nililla pale Hadi asubuhi na yule brother alikuja kunutazma aakanikuta akajilaumua sana kwa kutonifata na akaniahidi kua atanifata jioni ya siku hiyo sababu usiku ulipita alihisi kua nimepitia mengi magumu Mimi nilimkubarlia sababu alisisitiza sana kua nisilale pale Tena.
lakini Hadi inafika jioni hatimae usiku lakini hakutokea nikaja kusaidiwa na mama yake junior ndio ambaye alinipeleka nyumbani kwake tuliishi kama ndugu lakini alianza kubadirika na kunitaka kimwili nili...."
"Suma achana na hizo story twende kwa huyu aliyekusaidia usifike mbali kuhusu mama wa huyu mtoto"
"Sawa basi siku iliyofata yule kaka alikuja pale ofsini maana tayari ilikua ofisi yetu aligomba sana na kunitukana sana na kuwarushia nguo zangu na kuondoka zake na mimi kwakua sikua nimerudi Tena pale siku nilipokutana na juma akanisimulia Kila kitu,lakini mbali na hayo yote mama nimejikuta namsamehe Baada ya Leo kuwakuta wanafukuzwa kwenye nyumba waliyokua wamepanga nikaamua kuwasaidia na kuwapeleka kwenye ile nyumba yetu Aisha ila nisamehe kwa kuto kuwashirikisha hili"
mama yake akamuhuliza
"mbali na hayo yote lakini umewasaidia lakini sisi tuseme Nini wakati wewe ndo umepita hayo yote kama umefanya maamzi yako ni wewe ila ungemshirikisha mwenzio na kwenye maamzi ya kufanya hivi usirudie tena"
"Sawa mama nimekuelewa,mama maira wangu unasemaje kuhusu Hilo?"
"Sina usemi wowote ule"
basi walikua chakula na kuingia chumbani kupumzika zao.
maisha Yao yaliendelea kua na furahabwatoti wao pia waliendelea kukua vizuri san.
hatuamae maira alitimiza mwaka mmoja kwakti huo junior alikuaa na mwaka mmoja na miezi kadhaa Aisha Alianza kufanya mazoezi Tena na akiwa Kwenye mazoezi hayo Tena simu yake iliita na baada ya kupokea akasikia sauti ikisema
"Aisha Nina jambo nataka kukueleza muda huu naomba ufike gym haoanni Mimi Samuel"
Aisha alikata simu na baada ya muda mfupi aligika hapo gym na kukutan na Samuel baada ya salamu nyingi Aisha akamwambia
"Samuel umebadirika Santa aise umekuaje sjui"
"nikweli kabisa sababu nilijua nafanya mazoezi ya nguvu sana pia nikatoka nikapenda nnje huko kwaajiri ya kujifua vizuri kama naweza kupambana na watu wabaya"
"mmh umefanikisha Kwa asilimia ulizohitaji sawa niambie unachotaka kunambia mana nilikua narejea nyumbani"
"Sawa nisubiri Kwa dakika Moja Aisha"
Samuel aliingia ndani na kutoka na bahasha akatoa picha na kunikabidhi Kisha akaniambia
"Kwenye hiyo bahasha Kuna picha ambazo Kuna watu ambao wamesababisha vifo vya wazazi wangu"
"wazazi wako? inamaana kumbe huna wazazi?"
"ndio Aisha Sina wazazi Tena"
"Pole sana Samuel hata Mimi wazazi wangu nikajua wamefariki lakini kitu ambacho sijakiakini ndiomaana nilipotea Kuna kaka yangu ambae alikua anaishi na sisi akanikutanisha na wazazi wangu sikuweza kuamini kabisa"
Aisha alikua anaongea huku anafungua bahasha na alivyotoka picha zote picha ya juu kabisa akamuonya mama yake na baba yake alishtuka sana na kumuhoji Samuel
"we Samuel inamaana bawa ndio wamesababisha vifo vya wazazi wako?,kivipi Yani?"
"ni story ndefu lakini jua ndio hivyo"
"hapana sikubaliani na wewe Samuel hivi unajielewa wewe?"
"ndio najielewa vizuri sana"
Aisha akafikilia Kwa haraka akajikuta anamwambia Kwa hasira
"sikia Samuel kama ukitaka urafiki wetu ishia njiani sawa Mimi nauvunja urafiki huu Leo hii sababu ya ujinga na ushutumi wako wa kipuuzi"
"Aisha kwanini uvunje urafiki wangu wakati wewe ndio nimekushirikisha unisaidie"
"Samuel huwezi kushutumu wazazi wangu kua wamesababisha vifo vya wazazi wake hapana"
"eeh inamaana wewe ni wazazi wako Hawa?"
"sikia Samuel na iwe MWISHO na mwanzo kunitafuta mjinga wewe"
Samuel alikua ameshavurugwa sababu hakuwahi kufikilia kama watafikia hapo sababu mawazo yake yote alihisi huenda Aisha akawa msaada wake sababu jinsi tu unavyomtizama unamuona kama vile anaakili za ziada sana kichwani mwake.
Aisha aliondoka akiwa na hasira sana huku akizungumza Kwa kumtoa akili Samuel.
alipofika nyumbani kwao alopita Moja Kwa chumbani akaoga maji kuondoa uchovu Kisha akatoka sebleni kwaajiri ya kupata kifungua kinywa lakini alikua anawaza sana kuhusu maneno ya samule na kujikuta anamrudia akilini mwake sauti ya Samuel adia akjikuta anapandwa na hasira na kuvunja kikombe ambacho alikua anakitumia kunywea chai muda huo yaani nae pia alikua amevurugwa pia na kuhitaji warinda wazazi wake wasioate na jambo baya yoyote ambalo anapanga kufanya Samuel.
siku nzima alikua na mawazo mengi sana hakua anajiskia kula chakula Wala hata kufanya Chochote alikua anawaza tu njia na jinsi ya kufanya jambo kwaajiri ya wazazi wake.
mara Ghafla akapata wazo jipya akampigia simu Dani na kumwambia
"Dan Kuna mtu amejitokeza amedai kua wazazi wangu wamehusika na kifo cha wazazi wake hii ikoje nimechanganikiwa sana nataka kuwarinda wazazi wangu juu ya ujinga wake"
"Aisha kuwa mpole sawa Usiogope kwanza huyo mtu ni wa aina gani?"
"ni kijana mdogo lakini anaonekama kuwa amejioanga Kwa Chochote kile"
"ooh Sawa nataka uniunganishe nae niweze kukutan nae"
"Sawa Dan basi kesho asubuhi mapema njoo nyumbani alafu tutaelekea kwake"
"limeisha Hilo Aisha kua na amani tu"
Aisha alikata simu na muda mfupi mmewake aliingia na kuwaambia
"nataka kuwapeleka kule nilikowaambia siku zote kuwa nataka kuwapeleka"
"baby siko sawa Kwa Leo labda muende tu nyie na mama"
"hapana wewe ndio muhimu zaidi Aisha kwahiyo lini utakua na muda?"
"kesho kama nitakua sawa nitakuambia"
"Sawa kipenzi Leo nataka nikusaidie kupika chakula"
basi kama familia walikua wanaandaa chakula Kwa pamoja na kujumuika kula Kwa pomoja pia.
uaiku wa siku hiyo Aisha alichelewa sana kupata usingizi sababualikua anawaza juu ya kesho kama Samuel ataweza kumsikiliza kuhusu jambo analotaka kumwambia,pia na Kwa upande wa samule pia alikua anawaza kumpigia simu Aisha kesho aweze kumuomba msamaha juu ya shutuma zake Ili aweze kujua ilikuaje.
wote walikua wanawaza sawa je unadhani itakuaje usikose itaendelea....