I MISS YOU 1- 4

 I MISS YOU 01







Ilikua yapata majira ya sa3 usiku ambapo kulikua na mwanamke,mrembo maeneo ya bar,akiwa amesimamisha vyupa kadhaa vya bia kwenye meza yake,akiwa anakunywa moja baada ya nyingine,akiwa mwenyewe tuu huku machozi yakiwa yanamtiririka usoni kwake.

waliokua maeneo hayo walikua wanamtazama sana na kujihuliza kwanini anafanya hivyo maana alikua anakunywa bia kama anakunywa maji,na kwa muda mfupi tu meza ilikua tupu na akaagiza bia zingine.

Naam zile ambazo zilikua zipo juu ya meza tayari alishazimaliza akamuita muhudumu.

"Hey waiter hebu ongeza zingine sita hapa."

Waiter alipiga hatua hadi hapo alipokua mwanamke huyo na kumwambia.

"Boss umekunywa sana,na hizo ulizokunywa zimetosha sasa hatuwezi kuongeza tena,unapaswa uende kupumzika tafadhali."

"Aah unanilazimisha kuondoka hapa unaniripia wewe?,si nalipa kwa pesa zangu au,wewe kina kuwasha nini?."

"Najua ndio unaripia mwenyewe lakini ulizokunywa ni nyingi sana hatuwezi kutoa nyingine."


huyo mwanamke baada ya kuambiwa hivyo alianza kuangusha kilio papo hapo kuonesha kua anaumia sana,kwanini wamkoseshe raha,kwa pesa zake,basi ikabidi asimame aweze kuondoka maana alihisi kua amefukuzwa kwenye bar hiyo,alisimama kwa shida kutokana na kulewa sana,haikua rahisi kwake kutembea akiwa hivyo sababu ndio ilikua siku ya kwanza kunywa pombe nyingi kiasi hiko,na wakati huo alikua amevaa viatu virefu pia.

Kwa jinsi alivokua anatembea watu waliopo pale bar walisimama kumtazama huyo mwanamke,jinsi alivyokua anaparamiana na watu vibaya na wengine walikua wanamsukuma kwa kumuona kama mtu ambae anatafuta mwanaume kwa nguvu,yaani anajiuza lakini hakuwa hivyo.


Alifanikiwa kutoka nnje ya bar,hiyo na kuanza kutembea huku akiyumba yumba,kama mnavojua kua hakuna sehemu isiyo na wahuni,hivyo wakati anaendelea kupiga hatua ghafla,wahuni walitokea na kumfyatua miguu yake,na kwakua alikua amevaa viatu virefu mwanamke huyo aliachia pochi yake na kuanguka chini kwa maumivu sana huku akiomba msaada nawakati huo wale wahuni tayari walimchukua kila kitu chake na walishatoweka maeneo hago.


Kwabahati kwa nyuma kuna mtu alikua anakuja,na alipomuona mwanamke huyo analia kwa maumivu sana alimsogelea haraka ,na kumvua viatu ambavyo alikua amevaa na wale wahuni walikua hawajafanikiwa kuchukua viatu hivyo sababu ya mzunguko wa watu,hivyo huyo mwanaume alimbeba kisha akaita tax na kumuingiza kwenye gari na kuondoka nae.


upande wa pili kuna mwanaume ambae alikua anahangaika kupiga simu, mahari lakini kwa jinsi alivyokua anaonekana niwazi kua simu ambayo alikua anapiga ilikosa majibu kabisa,hivyo akatoa sikioni na kubofya tena simu yake kisha kuweka tena skioni na mara hii akasikika akisema.

"Baby huyu mjinga hajarudi hadi muda huu,ila sikia baby unajua kua siwezi kukuacha mwenyewe ,hivyo usijari nakuja sasahivi na yeye atajua mwenyewe huko aliko sijari hata kidogo kuhusuyeye."


Mwanaume huyo alikata simu na kuchukua shati lake akavaa na kufungua mlango na kuufunga vizuri kisha akaondoka zake,kumbuka kua ni majira ya usiku...

Baada ya kufika sehemu ambayo alihitaji kufika alifunguliwa mlango na mwanamke mrembo mwenye shape lake mashallah,alikaribishwa na busu la mahaba kisha akaingia ndani na mlango ukafungwa,na baada ya kuingia ndani mwanamke huyo akazungumza.

"Nathan sijapenda kwanini leo umechelewa sana kuja,hivi unajua mwenzako nakosa hata hamu ya kula bila ya kukuona eh,unajua hilo?."

"Aah jamani najua hilo suzy sasa unadhani ningewezaje kutoka bila ya yule kichaa kurudi eeh?."

"Anhaa kwahiyo amerudi au?."

"Nilikupigia simu na kukwambia hajarudi unadhani ningewezaje kukosa utamu wako,ndio maana nimekuja,haya tukalale basi."

"Jamani nathan umemsahau utaratibu wetu wa kila siku jamani si lazima tule,tuoge ndio tulale au?."

"Aah baby sawaa tufanye hivyo basi."

Walisogea mezani na kuweka chakula kwenye sahani kisha kuanza kula,lakini wakati huo wote nathan akili yake haikua hapo kabisa yani,mawazo yake yalikua mbali sana, kiufupi,suzy akamuuliza.

"Baby unajua sikuelewi leo kama unawasiwasi na mkeo basi ondoka kwangu hayo mawazo yako nenda kakae nayo nyumbani kwako hapa sitaki kujifanya kama umefiwa ondoka nathan"

Nathan ukweli alikua haelewi kabisa alitaka kuondoka lakini Suzy alimvutia chumban kwake na kufunga mlango.( Suzy ataka kufanya ubakaji😁).


Nnje ya jengo la hospital,ilipaki taksi na aliyeshuka alikua mwanaume ambae alikua amembeba mwanamke mikononi kwake na manesi ambao walikua wamekaa walichukua kiti cha magurudumu kwaajiri ya kwenda kumsaidia,huyo mwanaume akasema.

"Tafadhali naomba apatiwe huduma haraka sana iwezekanavyo anaonekana kua ameumia sana."


Hakujibiwa chochote sababu madaktari walikua wanamhangaikia,wakimfkisha emergency room,na walipomsemesha mdomo wake ulikua unatoa harufu ya pombe, daktari alitoka kwenye chumba hiko na kuzungumza na huyo mwanaume.

"Mr mkewako anaonekana amekunywa sana na hatuwezi kumpa huduma akiwa amelewa sana kiasi hiki."

"Doctor ameumia miguu lakini na sio sehemu nyingine yoyote naomba nimsaidie tafadhali."

"Subiri kwanza tuone tunafanyaje."

Doctor aliporudi tena ndani akamkuta mwanamke huyo anatapika sana,akawaita manesi,kuomba wamsaidie sehemu ya kutapikia maana kitandani palikua pamechafuka sana,na baada ya kutoka Dr alikua na hasira sana na kuanza kumfokea mr.


"Hivi unamuachaje mkewako anakunywa pombe kupitiliza eeh ona sasa ametapika chumba chote kinanuka harufu ya pombe."

"Samahan doctor mimi nilikua nimesafiri kikazi hivyo,nikama bahati tu kukutana nae njiani,wakati narudi ila nisamehe sana wakati unatoa bili yake utanijumuisha na kiasi cha kutapika kwake na kuchafua huko ndani."

Dr huyo hakujibu kitu akaingia ofisni kwake,na kuchukua baadhi ya vifaa vyake na kuingia tena kule ndani, akamkuta mgonjwa huyo amechoka sana maana alikua ametapika sana hivyo mwili ulikua umekosa nguvu,aliitwa mwanaume aliyemleta na alivyoingia akamkuta anatetemeka sana,alivua koti lake na kumfunika,kisha akamwambia.

"Pole utakua sawaa,lakini unajiskiaje kwa sasa?."

"Vizuri najiskia afadhali sasa."

Kijana huyo aliwaomba manesi watoke nnje ili aweze kuongea nae kidogo,na walifanya hivyo ili kumpa nafasi ya kuzungumza.

"Aah kaka bila shaka wewe ndio umenileta hapa, sindio?."

"Ndio ni mimi kuna tatizo?."

"Daktari aliniambia ni mumewangu nikawa najiuliza mumewangu,yupi maana..."

"Aah usifanye hivyo kwa sasa uangalie kuhusu afya yako achana na hayo mengine sawaa,ngoja nimuite daktari basi."

"Aah samahani,lakini kama nitakuchosha ila nisamehe sana kwa kukusumbua,maana muda huu ungekua kwako umepumzika lakini uko hapa kwaajiri ya ujinga wangu, nashukuru sana kwa msaada wako,nipo hapa unaweza kwenda kupumzika nyumbani kwako,nitakua sawaa."

"Hapana usijari nitakua na wewe hapa hadi nijue hatima yako,pia kabla sijasahau simu hii unaweza mpigia ndugu yako yoyote ambae anaweza kuja nikukabidhi kwake."

"Aah unajua kwamba mimi si....."

Kabla hajaanza kuzungumza chochote tumbo likaanza kumuuma ghafla, mwanamke huyo alikua analia kwa maumivu sana huku akiwa ameshika tumbo lake, mwanaume huyo alitoka hapo haraka hadi ofisini kwa daktari na kumwambia kua hali ya mgonjwa wake imebadirika ghafla, daktari alifika na kutaka kuanza kumfanyia vipimo,yule mwanaume alitaka kushuhudia vipimo lakini daktari alimtoa nnje ili aendelee na kazi yake,kisha akamwambia mwanamke huyo aweze kulala chali ,yaani macho atazame juu ya paa na baada ya kufanya hivyo bado akiwa anasaga miguu kwa maumivu sana,na daktari alivyosogea kitandani alishtuka sana baada ya kuona damu, akaanza kumfanyia vipimo vya haraka na baada ya kumfanyia vipimo haraka akagundua kua alikua na ujauzito wa miezi mitatu lakini tayari ulishaharibika,alimfanyia upasuaji haraka na kumuacha apumzike kisha akatoka nnje na kumuita bwana mr ofsini,na baada ya kufika ofisini daktari akamwambia.

"Pole sana rafiki yangu,maana mkewako amepoteza ujauzito wa miezi mitatu,na bahati mbaya ulikua umeharibika tayari hivyo hii pombe imekua kama sababu tu kutoka ila inaonekana kua uliharibika kama siku mbili au tatu nyuma zilizopita."

"Dah vipi lakini yuko sawaa?."

"Ndio tumemsafisha kwa sasa amepumzika kwanza."

huyo mwanaume alitoka ofisini kwa daktari huku akiwa na huzuni sana..

usikose itaendelea...


 I MISS YOU 02



Hatimae asubuhi mapema, daktari alipomuona mgonjwa akamuuliza anajisikiaje akajibu kua anajisikia vizuri,akaitwa mr alipoingia wodini daktari akaanza kuongea.


"Mr kama tulivoongea jana usiku kua mkewako ndio hivyo na hatakiwi kufanya kazi ngumu ambayo itampelekea kuhisi maumivu."


"Doctor mumeongea nini mbona mimi sijaambiwa chochote kile shida ilikua nini?."


"Aah please nitakuambia usijari,aah doctor unaweza kwenda wacha niongee nae kwanza."


Daktari alitoka nnje na kuwaacha wenyew mr akazungumza.


"Pole saña,japo katika mazungumzo yetu ya jana hatujaulizana majina yetu lakini mimi naitwa Muran."


"Naitwa reshma."


"Aah sawaa reshma tunaweza kuzungumza mara baada ya kutoka hapa?."


"Hapana niambie daktari amesema nini kunihusu nataka kujua."


"Aah sawaa daktari amesema kua ulikua na ujauzito ambao ulikua umeharibika tayari kama siku mbili nyuma na pombe ndio imekua kama kichocheo cha kutoka lakini kwa sasa upo sawaa ameshasafisha tumbo lako."




Reshma alishika tumbo lake na kulitazama na alipomtazama mr muran tayari uso wake ulikua unamachozi,reshma alishuka kitandani huku akitaja jina la..


"Nathan,nathan,nathan.....!"


Mr muran alikua haelewi kwanini amebadirika ghafla hivyo,reshma alitoka nje ya wodi na kuanza kutembea,miguu yake ilikua imevimba lakini hakujali maumivu hayo,mr muran alikua anamkimbilia reshma na kutaka kumsubirisha lakini reshma alikua na hasira sana,akapanda tax na kuondoka zake,wakati huo muran alirudi hospital na kufanya maripo,kisha akatoka nnje na kuchukua boda boda ambayo alimwambia afukuzie gari ambayo imetoka hapo mda mchache na hiyo boda akamwambia kua anamfahamu huyo mwanamke,hivyo waliifatilia gari hadi ilipofika kisha reshma alishuka kwenye gari na kuingia ndani kwa hasira sana,akaanza kumtafuta Nathan kwa hasira.


"Nathannnn! nathannnn uko wapi wewe mpuuzi."


reshma alimtafuta nathan nyumba mzima lakini hakuweza kumuona mumewake alipandwa na hasira sana akawa amekaa kwenye sofa amejiinamia analia mwenyewe.


Upande wa nathan akiwa na mwanamke wake suzy waliamka na kuogeshana kisha nathan aliaga na kuondoka zake lakini bado akiwa hana raha kabisa suzy akamwambia.


"Nathan huna furaha ila kama ukiwa hivyo naomba usije nyumbani kwangu tafadhali."


Suzy alifunga mlango na nathan hakusema chochote kile akachapa mguu hadi nyumbani kwao,wakati huo yule boda boda na muran walikua bado wametulia maeneo ya ile nyumba,yule boda akamwambia muran.


"Yule mumewake ndo anarudi."


"Anhaa kumbe ana mume eeh?."


"Ndio ila we acha tu kaka, subiri uone kitachotokea"


Muran alibaki hapo kutaka kuona kitakacho tokea,baada ya nathani kuingia ndani akamkuta reshma amejiinamia analia,kitendo cha yeye kufungua mlango reshma alisimama kwa hasira na kumshika kwanguvu na kumsukuma ukutani na kumuuliza kwa hasira sana na sauti yake ilikua juu sana.


"Nathan kwanini,kwanini umemuuwa mwanangu,nathan najua wewe ndio chanzo cha haya yote tazama nimempoteza mwanangu kwasababu yako nathan nakuchukia sana nakuchukia nathan."




Reshma alikua analia kwa uchungu sana kisha akamuachia nathan ambae nae alikua hawezi kuzungumza chochote kile sababu kila alichokisema reshma kilikua ukweli yeye ndio sababu kuu,reshma alivyotoka nje akaona boda boda inapita akaita na kupanda kisha akaondoka zake,wakati huo nathan alikua anajilaumu sana kwa tamaa zake za kijinga ,aliingia chumban na kuchukua picha ya mtoto ambayo ilikua imewekwa ukutana na kuanza kuzungumza nayo.


"Mimi na reshma tulipendana sana,na tulitamani kupata mtoto kwa muda mrefu sana,lakini nilikata tamaa haraka sana na kuamua kuanza uzinzi,bila kujua hali ya mkewangu,na leo hii naambiwa nimesababisha mkewangu kapoteza mimba ya miezi mitatu,kama si wewe nisingetoka nje ya ndoa yangu nakuchukia sana,mimi nakuchukia sana."


Nathan alikua anaongea na ile picha huku akiivunja vunja na kukaa chini huku akitafakali vipi anaweza kumrudisha reshma wake nyumbani.




Yule boda boda alimfikisha reshma kwenye duka la dawa akachukua vidonge na kutoka nje na kumwambia huyo boda boda ampeleke sehemu lakini wakati hayo yote yanaendelea tayari mr muran na boda boda huyo walishayapanga kila kitu na walipeana namba hivyo wakati hayo yote yanaendelea mr muran alikua hewani kusikia kila kitu lakini wakati huo anawafata kwa nyuma.


yule boda boda akamuuliza reshma.


"Dada vipi mbona kama haupo sawaa na kwanini umesema nikupeleke huku?."


"Aah adam rafiki yangu sina umuhimu wala sina sababu ya kuishi tena,nashindwa kufikilia kabisa kuhusu mustakabari wa maisha yangu."


"Unamaanisha nini kusema hivyo dada,unajua mimi ni mdogo wako niambie huwenda naweza kukusaidia."


"Hapana huwezi kunisaidia chochote kwa sasa,hebu simama nahitaji kujisaidia kidogo."




Adam alisimamisha boda na reshma alishuka kisha kuingia kwenye msitu,uliokando na barabara hiyo wakati huo Adam alitoa simu yake mfukoni na kuzungumza na mr muran


"Kaka anaonekana kama amenunua vidonge , nafikiri anataka kujiuwa."


"We unaongea hivyo yeye yuko wapi?."


"Ameenda kujisaidia,ila atarudi."


Lakini wakati adam anazungumza na simu reshma alivyokua anarudi kutoka kujisaidia alisikia yale maongezi ikabidi ageuze arudi tena kule msituni maana alijua tu kua Adam anaweza kumrudisha kwa nathaniel hivyo akaamua kurudi kule kwenye msitu na kukimbia zake, wakati adam anaendelea kusubiri mr muran alikua kwenye gari akielekea ofsini kwake kwa mwendo wakawaida sana lakini ghafla akiwa kwenye mwendo huo ghafla alihisi amegonga kutonana na mtu aliyekatisha barabara bila kujua kama ni salama au si salama,mr muran alishuka kwenye gari, alishtuka sana alikua ni reshma,na muda huo damu zilikua zinaruka kwa wingi sana mr muran alitoa simu mfukoni haraka na kupiga simu gari ya wagonjwa,na baada ya muda mchache gari ya wagonjwa ilifika na kumchukua reshma na muda huo huo polisi walifika haraka kwaajili ya kupima juu ya ajari hiyo.


Mr muran alimpeleka reshma kwenye hospital ya hadhi ya juu ili aweze kupatiwa matibabu kwa ustahiki anaoutaka yeye,na alipofika alianza kuhudumiwa kwa haraka tena alikua anapatiwa matibabu wakati mr muran yupo pia anashuhudia kila kitu,huku akiwa anaomba sana reshma aweze kuwa salama,na baada ya muda mfupi alipewa majibu na daktar kua yupo salama japo kuna majeraha ambayo yanamzunguka, lakini majibu kamili atapewa baadae,mr muran alishusha pumzi na kutoka nje kisha kumpigia simu adam na kumueleza juu ya kilichotokea,kisha akatoka nje kumsubiri adam.....


je unadhan itakuaje usikose itaendeleaaa....


 I MISS YOU 03


Muda mchache mara baada ya adam kuelekezwa sehemu alipo mr muran,aliwahi kufika na kwa bahati akakutana na mr muran nje ya geti,mr muran akamwambia adam.


"Adam asante sana kwa msaada wako ila kuna jambo limetokea reshma alipata ajari nyingine tena japo hali yake sio mbaya sana ila ndio hivyo naomba usimwambie mtu kama yupo hapa."


"Aah kaka usijari kuhusu hilo kila kitu kitakua sawa."


Mr muran mwenye asili ya kiarabu alichukua waleti yake na kutoa noti kadhaa za elfu kumi 6 na kumkabidhi adam kisha akamwambia.


"Adam kukiwa na jambo lolote basi usisite kunipigia ili kunijulisha,na mimi nitakupa taarifa zote kumhusu reshma."


"Sawa mr muran kwaheri."


Adam aliwasha pikipiki na kuondoka zake na mr muran nae alipokea ujumbe kua majibu yapo tayari,alirudi ndani na baada ya kuingia ofsini akaambiwa.


"Mr muran,baada ya kumfanyia vipimo tumegundua kua mgonjwa alikua anavidonda vibichi kizazi chake,kabla ya kupata ajari na hivyo imebidi tumfanyie usafi tena maana kizazi chake kilikua kimevujia na damu pia."


"Dr kwahiyo unataka kusema vipi?."


"Mungu ndio mpangaji kwenye hili ila hadi afya yake kujijenga tena na kizazi chake kuwa imara itachukua muda mrefu sana na anaweza asipate kabisa mtoto."


"Aah unasemaje daktari?, furaha yake ni kupata mtoto sasa itakuaje kama akiskia hili..?"


"Usijari tunaweza kuongea nae kupitia kwa mtaalam wa saikolojia hivyo atakua sawa."


Mr muran alitoka ofsini kwa daktari akiwa na mawazo sana,huku akielekea wodini ambapo alikua amelala reshma,wakati huo ila reshma alikua tayari amerudisha fahamu zake,hivyo alikua amelala kitandani huku akiwa amefumbua macho yake,na haelewi nini kimetokea.


Mr muran alikua anamtazam reshma,ambapo reshma nae alikua anajaribu kukumbuka jinsi ilivyokua,wote walishtuka baada ya simu ya mr muran kuita,mr muran aligeuka na kutoa simu yake kwenye mfuko wa suruali akaweka skioni huku akitoka pale,reshma akajiuliza.


"Huyu mbona kama sura yake sio ngeni niliwahi kumuona wapi,aah kumbuka reshma kumbuka....Naam ni mr muran ambae alinisaidia nilivyokua nimelewa,ndio natakiwa kumshukuru hata leo itakua kanisaidia tena,hapana lazima niweze kumshukuru."


Wakati anataka kuteremka kitandani mara ghafla mlango ulifunguliwa na mr muran nae aliingia na kumwambia.


"Reshma unaenda wapi sasa jamani unatakiwa kupumzika tafadhaii."


"Mr muran..."


"Ndio miss reshma,unahitaji chochote?."


"Hapana nilikua nataka kukushukuru kwa msaada wako,mara ya kwanza ulinisaidia pindi nilipokua nimelewa,na niliondoka bila kukushukuru,nimekuona pindi unazungumza kwa simu nikaona nikufate nikushukuru."


"Ooh asante kwa kushukuru,pia pole sana na sitaki kukuficha tena ila jua kua nilikugonga mimi ila kwa bahati mbaya umepa..."


Polisi walikatisha mazungumzo ya mr muran na reshma mara baada ya mlango kufunguliwa na kuingia kwenye wodi hiyo kisha kuwasalimia na kuzungumza.


"Nijambo jema sana kua upo karibu na mgonjwa uliyemsababishia tatizo,ila yote kwa yote,tulitaka kukupa taarifa kua kwanza haukua kwenye mwendo mkali ila ulikosa umakini wakati dada alipokua anavuka barabara hivyo uwe muangalifu siku nyingine,kwa leo tunakabidhi gari yako ikiwa haina shida yoyote."


Mr muran alimshukuru sana Mungu kisha akasema.


"Asanteni sana nilipoona sijapata taarifa zozote nilikua nataka kumuacha mgonjwa niweze kufika kituoni lakini mmefika wakati muafaka nitajitahidi kua makini."


Polisi waliwaaga na kuondoka zao kisha mr muran akataka kuzungumza lakini reshma akamwambia.


"Kosa ni langu la kuvuka barabara bila kutazama kama kuna gari inakuja au lah,kama ungekua kwenye mwendo mkali nafikiria kua ningekua kaburini sasahivi lakini ingekua bora zaidi kama ingekua hivyo."


Mr muran alimtazama kwa jicho kali sana na kuzungumza kwa ukali.


"Reshma hutakiwi kuzungumza hayo mambo tafadhaii,bado unanafasi kubwa sana ya kuishi,usikufuru wala kulaumu, Mungu anamakusudio yake na kile anachokipanga,reshma pumzika kwa sasa nakwenda kuchukua kadi yangu kule hospital,niliisahau nakuomba upumzike na ukihitaji chochote nesi yupo hapo nje ukiita tu atakuskiliza."


Mr muran alianza kuzungumza kwa ukali kisha akapunguza ukali na kuzungumza kwa taratibu sana na kumfanya reshma ageuke upande wa pili aweze kupumzika,mr muran alimtazama reshma kisha akaondoka zake.


Upande wa nathan alikua na mawazo sana juu ya mkewake akajaribu kumpigia simu reshma lakini simu ilikua haipatikani,nathan alishindwa afanye nini, alikua amekaa tu chini, alivyoskia nje mlio wa pikipiki ndipo akakumbuka kua bodaboda wao ni adam alichukua simu na kutafuta namba ya adam kisha kumpigia simu,baada ya kuzungumza na adam nafikiri majibu hayakuweza kumridhisha bwanaa nathan alirusha simu kwenye sofa huku akikuna kichwa chake maana alihisi kuchanganikiwa sana.


Adam alikua kijiweni kwake ambapo hua anapaki kusubiria abiria mara simu yake ikaita alitoa mfukoni na kuona mr muran ndio anampigia alitabasam sana hadi kuwafanya wenzie wamuulize.




"Kaka vipi mbona sikuizi sio mkaaji sana hapa alafu umepigiwa simu unatabasam umepata demu anakulea au vipi?."


"Tulia ndugu zangu naongea na billgett, hallow mr muran habari?."

"Nzuri sasa adam nataka kuzungumza na wewe kama utakua na muda."


"Hakuna shida mkuu nipo hapa hospital kijiwenu ndio napaki boda yangu."


"Anhaa mimi pia nipo hapa hospital nimefuata kadi yangu,baada ya kuisahau jana."


"Sawa boss tukutane hapa nje."


Simu ilikatwa na adam akataka kuwaacha boda aweze kuondoka rafiki yake alisogea karibu na kumwambia.


"Oya mwanangu kama unafanya uhuni na biashara haramu wakija polisi hapa tunakukataa na tutakuchoma pia mi nakuambia ukweli."


"Aah ndugu zangu nawezaje kufanya hayo wakati mnajua bimkubwa ananitegemea nyie msijari kuhusu mimi muwe na amani tu."


Adam aliwaondoa hofu rafiki zake na kuwaacha boda hadi kwenye geti la kuingilia hospital kwa bahati akaiona gari ya mr muran ilikua inatoka kwenye geti hilo alishusha kioo na kumpa ishara kua amfate adam alifanya hivyo, alimfata mr muran hadi alipoona panafaa mr muran alipaki gari na kushuka kisha adam nae akapaki boda yake.


Walisalimiana kisha wakaingia ndani ya hotel hiyo,na kuchagua meza kisha kukaa kusubiri wahudumu, mhudumu alisogea na kuwapa menu,walichagua walichohitaji kisha mr muran akaanza kuzungumza.


"Adam ukiachana na boda boda unafanya shughuli gani nyingine?."


"Aah hakuna boss mimi tangu nimemaliza kidato cha nne na nikafeli sikuweza kuendelea na masomo nikapata bodaboda ndio inanifanya naishi."


"Anhaa unafamilia,labda mke,mtoto hivi?."


"Hapana bado sina mke wala mtoto ila nina mpenzi tu,lakini bado naishi kwa mama yangu sababu mama yangu afya yake sio ya kuishi mwenyewe."


"Anha sawa hakuna shida,najua utakua na shauku kwani nataka kujua kuhusu wewe na mimi utashindwa kuniuliza kwaajiri ya uoga ila naitwa mr muran,nafanya kazi bandarini,nilikua na mke niliishi nae kwa miaka 3 lakini hatukufanikiwa kupata mtoto akaniacha mwenyewe na kuondoka zake,tangu aende ni miaja miwili na miezi sita sasa sijawahi kua na mahusiano japo naskia kua yeye amepata watoto wawil kwa sasa lakini mimi bado sina hata mmoja,piga mahesabu hadi sasa ni muda gani nimeishi bila kuona mwiko wa mwanamke?, najua utasema nimewezaje kwa muda wote huo ola nimeweza."


"Pole sana mr muran changamoto za ndoa ni nyingi sana je mliwahi kufanya vipimo vya uzazi mara kwa mara?."


"Ndio tulifanya hivyo kila baada ya miezi mitatu kwa miaka yote mitatu lakini hatukua na shida yoyote ile."


"Pole sana ,hata bwana nathan na mkewake namzungumzia reshma nao pia ndoa yao ina miaka miwili sasa lakini nao pia iko hivyo,miss reshma amekua akiniambia nimfatilie bwana nathan nikagundua kua anamchepuko japo mchepuko ni mke wa mtu lakini nilishindwa kumwambia sababu miss reshma ni mpole sana na anampenda sana mumewake sikutaka kuwa kikwazo kwenye ndoa yao,ila ndio hivyo,na kama unavyosema alibahatika kupata ujauzito na umetoka sijui reshma atafanya maamzi gani."


"Adam mdogo wangu sijui kwanini nimekuambia mapema ila nimetokea kumpenda sana reshma,sura yake ya upole,nimejikuta tu navutiwa nae,ila sijui kwa upande wake itakua vipi."


"Ooh usijari mr muran sidhani kama dada reshma atarudi kwa bwana nathan tena,japo sina uhakika sana ila nachojua anampenda sana."


"Sawa ila pia nataka ufikirie kua nataka kukupa ajira bandarini kama utahitaji,utanipa jibu."


"Mr muran,kufikiria?,kazi ya bodaboda nilikua nafanya tu mimi ila sikua naipenda kabisa ila nilikua nafanya kwaajiri ya kujikimu tu na maisha kama utanipa ajira nitafurahi sana."

"Sawa leo muda naona umeishia nakwenda kumuona reshma kisha nitarudi nyumbani kupumzika tukutane kesho basi huko bandarini."

"Sawa mr muran."

Mr muran alimuachia pesa tena adam kisha akapanda kwenye gari na kuondoka zake,adam akasema.

"Mungu hakupi unachotaka ila anakupa unachostahili kukipata,dada reshma tazama leo hii ametokea mtu wakukufuta machozi tena anaonekana bado kijana mdogo sana,siwezi kukufanya ukose furaha kamwe nitakupigania hadi tone la mwisho."

Adam alisema hivyo kisha aliondoka zake...


itaendelea....


 I MISS YOU 04

Ni asubuhi mapema, sana siku mpya imeanza,mr muran alifika bandarini mapema na alikutana na adam walisalimiana kisha mr muran alimchukua adam hadi ofisini kwake na kumwambia.


"Karibu sana hii ndio ofsi yangu kama unavyoiona,na nilikua na na wasaidizi ambao walikuwa wasumbufu sana hadi sasa nimeondoa wasaidizi wengi sana hadi nikaamua nibaki Mwenyew lakini kwakua upo nataka kukabidhi ofisi hii kwamaana hata mtu akinikosa mimi akukute wewe ukiniwakilisha."


"Mr muran lakini mimi sijasoma nawezaje kufanya kazi hapa ofisini.?"




Mr muran alitabasam kisha akamwambia


"Sawa,nifate.."


Adam alimfata mr muran hadi mapokezi kisha akamwambia secretary wake.


"Aah leo umechelewa sana hadi nimekuwahi mimi,haya karibu ukae tuzungumze nahitaji kutoka."


"Sawaa boss.."


Walikaa kikao kifupi watu watatu wakazungumza vizuri kisha mr muran akasimama na kusema.


"Adam chochote ambacho hujakielewa muulize tu hapo secretary wangu hawezi kukuangusha nimefanya nae kazi kwa muda mrefu sana tangu nihamie hapa sijawahi kubadirisha msaidizi,ni mpole mkarimu pia hivyo...,Amina,anaitwa Adam.."


"Sawaa boss usijari nitajitahidi saña kumuelekeza kila kitu hadi ataelewa kidogo kidogo."


Mr muran alitabasam kisha akawaaga na kuondoka zake.




Safari yake iliishia hospital ambapo alikua amelazwa reshma, aliingia wodini na kumkuta reshma anataka kwenda chooni mr muran alimsaidia alimshika mkono hadi alipoingia chooni ,na hata wakati anarudi alifanya hivyo pia,reshma akamuuliza.




"Mr muran nimekushukuru sana lakini huna sababu ya kufanya haya yote,inatosha mimi mke wa mtu unajua?."


"Ooh nisamehe sana kwa hilo huwenda nimezidisha ila ni kwasababu...!,ohk sawaa nimekuelewa usijari."


Mr muran nikama hakupenda kile alichozungumza reshma akaamua kutoka nje na kumwacha mwenyewe,mr muran alimtumia ujumbe adam,kisha akaelekea kwa daktar kutaka kujua hali ya reshma daktar alimwambia kua anaendelea vizuri hivyo anaweza kupata ruhusa muda wowote siku hiyo,mr muran aliondoka pale hospital,na kwenda kutafuta chumba kizuri sana,uswazi akaingiza fanicha mpya ndani kila kitu kinachohitajika kisha akarudi hospital na muda huo alimkuta reshma ameshapata ruhusa lakini hakua na hela ya kuripia matibabu, mr muran akamwambia kua ataripia reshma akamwambia.




"Sitaki kutumia pesa yako sijui umetafuta vipi lakini nitakuripa."


"Reshma lakini mimi ndio nimekugonga lazima gharama iwe juu yangu."


Reshma hakujibu chochote na kutoka nnje,akaingia kwenye gari ya mr muran, mr muran alitabasam na kusema.




"Kaikumbuka gari yangu haya ngoja nimuulize wapi anaelekea."


Mr muran aliingia kwenye gari na kutaka kuwasha gari reshma akamwambia.


"Niazime simu yako nataka kuongea na adam."


Mr muran alimpatia simu reshma na wakati tu anawasha akakutan na ujumbe ambao ulionesha kua mr muran alichat na adam muda mfupi nyuma,alimtazam mr muran,nae alimuuliza.


"Vipi mbona unanitazama unataka kunimeza au?."


"Hapana naona ujumbe wa adam huyu adam mdogo wangu au?."


Mr muran alichukua Simu mkononi mwa reshma na kujifanya alisahau kuujibu,aliamua kumpigia adam na kumwambia.


"Samahan adam nilishindwa kujibu ujumbe wako skuiskia."


"Usijari mr muran ila kama ulivopata ujumbe fanya hivyo."


Mr muran alimtazama reshma na kukata simu,mr muran aliwasha gari, reshma akamuuliza.


"Unafahamu anapoishi adam?."


"Ndio nafahamu sababu nilikutana nae sehem kadhaa tukajikuta tunakua marafiki ghafla."


"Sawa."


Mr muran aliendesha gari hadi kwenye hiyo nyumba aliichukua funguo kwenye kanyagio na kuingia ndani,reshma alishtuka Saña baada ya kuona vitu kama vipya na vya kisasa, alimsogelea mr muran na mr muran alikua kimya tu , reshma akamuuliza.




"Unahakika kama hapa anaishi adam?."


"Sasa kwanini unaniuliza?."


"Mh nakuuliza sababu adam namjua hadi anapoishi napajua pia na hawezi kumuacha mama yake aishi mwenyewe hata kwa usiku mmoja,mr muran hivi vitu umenunua wewe na kumpanga adam ili ionekane ni vyake sio?."


Mr muran jasho lilikua linamtoka kwa uoga wa kuhisi anaweza kumpoteza reshma, hakujibu chochote,reshma akataka kutoka nje mr muran alisema.


"Ndio kila kitu ni mpango wangu sababu adam aliniambia kila kitu ulichokua unapitia na sikutaka urudi tena kuishi kwa mumeo ukiwa anakuumiza,reshma nisamehe kwa hilo."


Reshma alimtazama mr muran na kumuuliza.


"Kwenye maisha yako umeshawahi kua na mpenzi wa siri wakati ukiwa na mwanamke mwingine?."


"Hapana,lakin kwanini unaniuliza?."


"Nakuuliza sababu nimeona hauuwezi uongo,huwezi kufanya uongo kuwa ukweli unajulikana mapema sana,ila kuna viumbe vilivyosoma cuba,anakuzungusha hadi unaamini kumbe zote ni porojo tu na niuongo uliokithili ila asante sana kwa ukarimu wako naondoka zangu.."


"Reshma,usiondoke tafadhaii."


Reshma hakugeuka nyuma akaamua kuondoka zake Kabisa pale mr muran hakua na chakufanya zaidi ya kujiona sio mwenye bahati kila siku yeye ni mtu wa kukosa tu,akaamua kujituliza kwa kunywa bia huku akiskiliza nyimbo za taratibu sana za kuumizwa.




Upande wa bwana nathan alikua haelewi moja wala mbili ikabidi aende nyumbani kwao na suzy na alipofika alimkuta suzy amependeza sana,suzy akamuuliza nathan.


"Hee wewe umekuaje?."


"Suzy mkewangu ameondoka nyumbani baada ya kunishutumu kua mimba yake imetoka kwasababu yangu."


"Hee mkeo alikua na mimba?,pole sana lakini,mimi natoka hebu toka nje nifunge mlango wangu."


"Suzy unaenda wapi?."


"Nathan unaniuliza naenda wapi?,nakwenda kumpokea Mumewangu mimi,, unadhani naenda wapi?."


"Haah!,Suzy si uliniambia kua huna mume wewe?."


"Haa..!, nathan mwanamke mzuri kama mie nakosaje mume sasa?,hebu kua na akili hata robo,mtoto mashallah nisiwe na Mumewangu hebu nenda bwana na nisikuone tena hapa."


"Suzy lakini nakupenda mwenzio,na umesema una mimba yangu nitawezaje kuwa mbali na wewe?."


"Hee..! we babu we unitue mtoto huyo una kizazi wewe cha kunipa mimi mimba tena unikome mbwa mkubwaa wewe.."


Suzy alimjibu vibaya sana nathan na kuondoka zake, nathan alijiskia vibaya sana na kumkumbuka mkewake reshma,kwanini alimsaliti,na huenda muda huo wangekua na furaha zaidi kama angejua kama ana ujauzito wake,mr nathan alilia kwa uchungu sana.




Lakini wakati reshma anapitia pita karibu na mitaa ya kuelekea nyumbani kwao,alikutana na adam,ambae muda huo alikua amevaa vizuri amependeza sana,reshma akamuita.


"Adam ni wewe?."


"Ndio dada vipi unaendeleaje?."


"Vizuri sana,adam umependeza sana."


"Asante sana,lakini dada kwanini uko huku,si nilimwambia mr muran akupeleke nyumbani kule?, ndiomaana nimekuja huku ili wewe ubaki kule."


Reshma alimsogelea adam na kumtazama kwa makini kisha akamwambia.


"Ni mr muran ndio alikushawishi munidanganye sio?."


"Dada re...!!"


"Kimya adam inamaana mlikua mnaniendesha kam mtoto kwa mipango yenu binafsi sio,?,sasa basi iwe mwanzo na mwisho kuniita dada na pia usije kunisalimia wala kuniita popote utakaponiona sababu nawachukia wewe na huyo mwenzio mpuuzi."


Reshma alizungumza kwa hasira sana na kupiga hatua kuondoka pale lakini adam alimuita.




"Reshma..!"


Reshma aligeuka na adam akazungumza.


"Nisawa unaweza ukawaza kuhusu chochote kibaya,sababu ni kawaida ya watu wenye maumivu wanaweza kuzungumza chochote ambacho kinakuja kwenye ulimi na kinywa chake sababu ukishaumwa na nyoka,hata ukiguswa na jani hushtuka ila Nataka kukwambia tu kwamba mr muran hakua na nia mbaya na wewe,ila upweke wake Ndio umemfanya ajenge ukaribu na wewe kwa haraka baada ya kusikia kile unachopitia,ila kwakua umesema niskuite dada kwaajir ya mipango yangu sawa ila nilifanya hivyo sababu sikutaka uende tena kukwazika na kuumia kwa mtu ambae hajali kuhusu wewe,wakati nikiumia kama mdogo wako wa tumbo moja juu ya mambo aliyokua anakufanyia na nikaomba sana Mungu uweze kukomboka ila leo nimekua m'baya,sababu ya mipango yangu,nenda reshma ila hutokaa unisahau kwa kukupambania kama mdogo wako siku zote kwaheri.."


Adam aligeuka na kuanza kupiga hatua kutoka pale alipokua amesimama,wakati huo reshma alikua amesimama tu akimtazama adam akipotelea kwenye kona ya ya nyumba yakaribu na walipokua wanazungumza....


itaendeleaaa usikose....


Previous Post Next Post

نموذج الاتصال