I MISS YOU 5 - 8

 I MISS YOU 05



Asubuhi ya simu iliyofata jay aliamka na kumtazama mkewake,suzy alionekana kua mchovu saña,jay alisikitika saña kuona hajamfanyia fea mkewake,alitoka kitandani,kuelekea jikoni,aliandaa kifungua kinywa kisha akampelekea suzy chumbani kwake,alimuasha suzy aliamka na kukuta jay amemletea kifungua kinywa,alitabasam kwanza kabla ya yote kisha akasema.


"Asante saña jay wangu,pia nisamehe saña kwa usiku wa jana." alizungumza suzy kichwa akiwa ameinamisha chini.

Jay alimsogelea pale akam'busu kisha akashika mkono wake na kumtazama suzy kwa sekunde kadhaa kisha akamwambia.


"Suzy wewe ni mkewangu ambae nakupenda sana,na kinachotokea ni kama bahati mbaya,ola nakushukuru kwa kubaki na mimi sababu niwengi walishindwa kuwa na mimi wakinisema mimi ni m'baya,sana pia uume wangu mkubwa lakini wewe hukuwahi kunizungumzia vibaya hata siku moja nakupenda sana."

Jay alizungumza na kum'busu tena suzy kwenye lipsi zake,kisha akavuta sahani ambayo ilikua na bakuli ya supu na mkate kisha akakamulia ndimu kidogo kisha akachota mchuzi wa supu kidogo kisha akasema.


"Sijaweka kiungo cha kukera kama utahitaji niongeze utanijulisha mamaa."

Suzy aliona huo ndio muda wa kudeka zaidi kwa jay, akaitikia kea kichwa,jay nae akaendelea kumchombeza suzy wake.


"Mamaa inamaana hadi kuzungumza unaona shida?,kama unahisi homa basi nikupeleke hospital." Jay alizungumza huku akiwa anamgusa gusta suzy kwenye shingo yake na sehemu kadhaa za mwili wake kujua kama mwili wake umepandisha homa,kisha akasema.


"Aah lakini naona mwili wakouko sawa labda ni....!" 

Kabla hajarudisha mkono kuna mahari alifanikiwa kugusa na kuhisi kama vile ameumwa na mdudu,jay alisema.

"Hebu subiri."


Aliweka sahani ya supu kwenye meza kisha akasogea karibu ya suzy na kumtazama kwenye shingo yake.


"Khaaaaah!." Jay alisema kwa mshtuko ambao ulimfanya hadi suzy ashtuke na kumuuliza.


"Jay nini tena?."


Jay alimtazama suzy kwa sekunde zaidi ya thelathini,bila kuzungumza chochote niwazi alikua anamtathimini vizuri suzy ni mwanamke wa aina gani kisha akasimama na kufungua kabati na akachukua shati lake na kuondoka zake,akimwacha suzy mwenye mshangao na kujiuliza maswali mengi sana,alisimama kutoka kitandani na kusogea kwenye kioo,akaona alama nyingi sana na kutokana na rangi yake hizo alama zilionekana vema sana bila hata viulizo,ulikua ni (love bite),na hapo sasa ndipo akagundua kwanini jay ameondoka bila kuweka chochote.


Nyumban kwa muran,adam aliamka mapema sana na kuelekea kwenye chumba cha mr muran akagonga mlango,lakin haukufunguliwa mlango wala kusikia sauti,adam alifungua mlango lakin hakuona mtu kitandani,aliingia huku akifuta kwa tahadhali sana.

"Mr muran,mr muran...mr."


Lakinj hakukua na majibu yoyote,adam alitoka chumbani kwa mr muran na kumpigia simu amina,simu ilipokelewa kwa haraka sana na amina.

"Hallow adam,unaaemaje?."

"Amina sijui,sijui nini kimetokea mr muran hayupo chumbani kwake."

"Adam mr muran hilo ofisini mbona,hata mwenyewe nilishtuka sana baada ya kuona simu yake na kuniambia kwanini nimechelewa kufikia ofisini,na alinipigia majira ya saa kumi."


Adam alishusha pumzi kisha akataka simu na kujiuliza,kuna nini kinaendelea Kati ya amina na boss muran huendà kuna siri ambayo wanayo kwanini aondoke na kuwaacha bila ya kusema chochote,adam aliamua kumuamsha reshma.

"Reshma..! resh..,amka kumepambazuka."


Reshma alijinyosha nyoosha baada ya kuamka kisha, akamsalimia adam huku akipiga hatua kuelekea kwenye chumba cha mr muran adam akamwambia.


"Hayupo tayari ameondoka mapema sana."

"Unasema??, inawezekanaje kuondoka mapema?."

"Reshma unategemea nitakua majibu gani ikiwa swali lako unajua majibu?,sikia navyoendelea kukaa hapa naona kama nazidi kupoteza muda nahitaji kwenda kazini,ukiboeka unaweza kwenda kule msasani,ola hakikisha hapa inafungwa mana mimi naondoka pia."


Adam aliondoka zake na kumuacha reshma,nikama alikua hajamuelewa adam,aliingia chumbani kwa mr muran,akakuta bahasha ya khaki kwenye kitanda chake,upande wa juu wa bahasha ulikua haijaandikwa chochote,lakini aliposhuka na kugeuza upande wapili aliona maandishi yaliyoandikwa kwa herufi kubwa,

(I miss you).


Reshma alishika moyo wake na kushindwa kuendelea kusimama,alikaa kwenye kitanda cha mr muran,bahasha huyo haikua imebanwa ilikua open hovyo reshma alichungulia ndani na kuona kuna karatasi nyingi sana nyeupe na picha pia, hakuridhika sababu hakua ameona vizuri,alizimwaga kitandani hapo na kuanza kuchambua moja baada ya nyingine.

Zilikua ni picha za mwanamke mzuti sana,reshma alikua makini sana kutazama hizo picha,na alipomaliza kutazama picha zite akaanza kupitia na barua ambazo zilikua hapo pia.


Moyo wake nikama ulikua unagoma sana kufungua hizo barua lakini bado yeye binafsi alitamani sana kujua kile kilichomo kwenye hizo barua.

Akafungua kikaratasi kidogo ambacho ni wazi kilikua na ujumbe mfupi kuliko karatasi nyingine.

Upweke.. Hili ni neno pekee ambalo lilikua limeandikwa kwenye hiko kikaratasi kidogo,reshma alitikisa kichwa chake na kuona hakina maana yoyote akamuweka pembeni na kuendelea na kufungua karatasi nyingine.


Adam alifika ofisini na kumkuta mr muran,alinisalimia na mr muran alijibu na kuendelea na kazi,adam alikua anatamani sana kuzungumza nae kwa kina lakini mr muran alijifanya tuko bize kuliko kawaida,adam akaona amuache kwanza kisha atarudi baadae akiwa hana kazi nyingi,alitoka ofsini akiwa hana amani kabisa,amina alimuona adam hana amani,adam aliingia kwenye ofisi yake ndogo kisha akatulia na muda mchache amina alimfata na kumuuliza.


"Upo sawaa adam?."

"Ndio nipo Sawa haina haja ya kuwa na wasiwasi."

Adam aliweza kumjibu kifupi tu amina Ili aweze kutoka na kumuacha mwenyewe,lakini alichokitegemea kilikua tofauti maana amina hakuondoka,alikàa kwenye kiti na kumtazama adam ambae alijifanya bize sana,amina aliendelea kumtazama amina hadi aliposikia simu ya mezani ikiita ndipo alitoka ofisini kwa adam na kurudi ofisini kwake na kupokea ile simu,na baada ya kukatwa kwa simu hiyo simu yake ya mkononi ikaita alipotazama akaona ni namba ya dada yake aliweka faili chini na kuzungumza na dada yake,amina alionekana kua na furaha sana isiyo kifani na uso wake ulionesha wazi shauku aliyokua nayo.


Mr muran alifungua mlango wa ofisini na kumshtua amina.

"Hey ni vipi unazungumza na simu muda wakazi amina..!"

Mr muran aliwaka kwa jazba sana amina alikata simu na kuweka mezani kisha akachukua faili na kumfata mr muran,nawakati hayo yote yanaendelea adam alikua anashuhudia kupitia upenyo mdogo wa mlango wake ambao amina alisahau kuufunga,na baada ya kuona amina amemfata mr muran nae alisimama na kwenda kuskiliza mazungumzo,amina alipofunga tu mlango cha kwanza mr muran alimuuliza alikua anaongea nanani?,kitu ambacho kilimfanya adam awe na mashaka saña kwanini amuulize hivyo....

usikose itaendelea...


 I MISS YOU 08

Asubuhi hii kea reshma alijikuta amelala sebleni na nathan,tena akiwa amelala juu yake,reshma aliamka haraka na kuanza kumtazama nathan,nathan hakua amelala ni vile tu alijifanya amelala reshma akamwamsha.


"Nathan..!,nathan!,nat....!"


Nathan alijifanya anaita Ili kuendeleza tu na maigizo yake kwa mtoto wakike reshma mwisho akajifanya ameshtuka sana na kujiangusha kutoka kwenye sofa hadi sakafuni na mara hii pia alijiuliza kwa maumivu zaidi hadi reshma nae akazidi kua na huruma nae,haraka alichukua simu yake na kutaka kupiga lakini nathan alimzuia na kumwambia


"Reshma sikati kuhudumiwa na yoyote zaidi yako mkewangu nakupenda sana"


"Nathan kumbuka mimi sio....!"


"Aaahhhh!,naumiaaa" Reshma alivyotaka kumjibu kua yeye sio mkewake nathan akajifanya anaumia ni wazi hakutaka kusikia yake maneno kutoka kwa reshma wake..




Baada ya wiki mbili kupita penzi lao likarudi upya ambapo nathaniel aliahidi kubadirika na kuwa kama zamani na reshma alimuamini na kuhisi nathan amejifunza kutokana na makosa yake ya nyuma,hivyo mara nyingi walikua pamoja pale tu nathan anaporudi kutoka kwenye mizunguko yake,reshma alijihisi kama amezaliwa upya maana aliona mapenzi yake ya mara hii yamekua bora zaidi ya mara ya kwanza.


Upande wa mr muran aliamua kuweka nguvu zaidi kwenye kazi yake,hata adam na amina tena kila mmoja alikua bize sababu wote Kati yao walihisi kupata tulizo mara tu baada ya kupata wapenzi ambao walikua wanawajali sana.




Ilikua siku ya jumatano mchana ambapo mr muran alifika ofsini na kuzungumza na amina


"Amina tafadhaii naomba mwambie adam nahitaji kupata chakula cha mchana na nyie"


"Sawa boss nimekuelewa"


"Sawa mtanikuta hapo nje nawasubiri" amina aliacha kile alichokua anakifanya kwa muda huo na kuingia kwenye ofisi ya adam na kumwambia.


"Boss anatuhitaji muda huu tafadhaii"


"Sawa nakuja."


Adam alisema hivyo na kuweka kila kitu sawaa kisha kutoka nje mr muran aliwaambia waingie kwenye gari na kuondoka pamoja. Walifika kwenye hotel nzuri iliyo karibu kisha wakashuka kwenye gari na kuingia ndani ya hotel hiyo kisha mr muran akawaambia.


"Agizeni chochote nitaripa."


"Mimi sitaki vitu vikubwa nahitaji tu ugali." adam alisema baada ya kuja mhudumu


"Aah mimi nataka chipsi kuku." amina aliagiza mr muran alitabasam na kusema.


"Ndio mambo yenu hayo watoto wakike haya bwana me nahitaji tu kahawa" mhudumu aliondoka baada ya kupewa oda kisha mr muran akazungumza.


"Aah!,ndugu zangu,amina na adam nafikiri kila kitu kipo sawaa na hakuna jambo lolote linalohitaji utatuzi sindio?"


"Ndio mr muran,nilikua mgumu sana kwenye kuelewa lakini amina mashallah amefanikisha kunielekeza kea vizuri hadi sasa niko vizuri"


"Napenda vijana wenye nidhamu na wanaopenda kujituma kama wewe adam"


"Asante sana mr muran"


"Sawa vipi lakini amina,huoni ni nafasi pekee ya ku...!" Kabla mr muran hajamaliza kuzungumza simu yake ikaita,alisimama na kutoka nje kuzungumza na simu na kuwaacha wakiwa wenyewe pale,amina alimtazama adam kea muda kisha akasema.


"Naona unafuraha sana sikuizi huna tena hasira na mimi hunichukii tena?."


"Amina sikuwahi kukuchukia kabla ila nilikua nawasiwasi sana kuhusu wewe na mr muran,baada ya kuona ukaribu wenu ile siku."


"Anha pole sana lakini hukusema kabla,ola mimi na mr muran ni mashemeji tu,yaani dada yangu aliolewa na mr muran na kushindwa kupata watoto akamuacha na kuondoka zake,mr muran alijitolea kunisomesha na nilipomfata dada huko anapoishi mumewake alikua ananichukia sana nikaona bora nirudi huku na bado mr muran alinipokea na kunipa kazi hapa hivyo muda wote nasimamia kama ndugu kwake hata matatizo yake mengi nayajua ndiomaan sikua na shaka na hilo"


"Anha nilihisi hivyo kabla ola nikataka kujipa uhakika"


"Inamaana ulikua una wivu kwaajiri yangu adam?,ulkua unanipenda?"


"Aah amina unajua..!",kabla hajazungumza simu yake ikaanza kuita na baada ya kutazama mpigaji alikua humaira, alitabasam na kuifunika ile simu. Amina alichukua simu ya adam na kutazama nani alikua anapiga aliona ni kina lililoseviwa my love,moyo wa amina uliripukwa kwa wivu na kuamua kuipokea.


"Hallo wifi mambo!"


"Mmh wewe nani?"


"Mimi naitwa amina nafanya kazi na adam,hivyo ni wifi yako"


"Anha haya sawa naomba niongee na adam tafadhli" adam mwenyewe alikua anamtazama tu amina alikua anazungumza lakini alionekana kua hana furaha kabisa, alimkabidhi simu kisha adam aliipokea na kuzungumza,akiwa amesimama.


"Niambie mkwe wa mama adam"


"Baby nilishtuka sana baada ya kusikia sauti ya mwanamke nikahisi nishaibiwa."


"Aah naanzaje kukuacha wewe?,sikia wewe Ndio namba moja,mbili na tatu wengine Ndio wanafata"


"Sawa mpenzi basi naomba leo tukutane tafadhali nimekumiss sana."


"Humaira unataka tushikwe?, tafadhali mpenzi,ujue naogopa yaani kuwa na wewe nikama tayari màisha yangu yapo mikononi mwa wazazi wako."


"Tafadhaii adam wangu kuna jambo nataka kukwambia."


"Sawa mpenzi nitajitahidi kufanya kila kitu Ili niwahi kuonana na wewe."


Simu ilikatwa kisha adam alirudi kukaa kwenye kiti lakini mr muran nae alikua anaaga kutaka kuondoka zake adam akajiuliza kwanini anaondoka ikiwa bado chakula hakijaletwa,mr muran alitoa hela na kumpa adam aweze kuripa chakula adam akajifanya kukata lakini mr muran aliwekwa mezani na kuondoka zake.Waliletewa chakula walikula na kuripa kisha kurudi ofsini na siku ile ikawa ngumu kwao adam kuweza kuonana na humaira.




Miezi mitatu baadae humaira na adam waliweza kukutana na kuzungumza, mwanzo kabisa walipokutana walikua wenye furaha sana maana walikaribisha kwa makumbato ya mahaba na mabusu kisha walikaa na kuanza kuzungumza.


"Adam baba yangu aliniambia kua mtoto wa shangazi amesharudi masomoni hivyo anataka kunioa, nilitaka kuzungumza nawewe kwa muda mrefu sana lakini ulikua bize, nilitaka kukwambia hivi tu"


"Ooh kumbe sass humaira unadhani itakuaje,au tunafanyaje sasa?"


"Adam nataka wewe uke nyumbani kwetu ili niweze kukutambulisha kwa mama yangu na baba pia sababu mimi kwenu mama yako ananijua"


"Humaira, unahisi wazazi wako watakua radhi na wewe kuhusu mimi?"


"Sijari kuhusu hilo kama hawatokukubari bàsi nitakua upande wako siku zote."


"Humaira,wale ni wazazi wako unapaswa kuwaheshimu na kutii kile wanachohitaji kwanini ukose nidhamu kwasababu yangu?"


Humaira alimtazama adam kwa sekunde kadhaa kisha alisimama na kuchukua pochi yake na kumwambia.


"Nasubiri simu yako kujua lini utakuja kwetu kama nikiona kimya bàsi nitajua kua hunipendi." Humaira alisema hivyo na kutaka kuondoka zake lakini adam alishindwa kumuacha mrembo huyo sababu alikua anampenda sana akamshika mkono wake na kumvuta kwake. walikumbatiana kwa dakika kadhaa kisha adam akazungumza.


"Sawa nitakuja kwenu ila naomba unirinde naogopa sana kuhusu hili jambo."


"Nitakua na wewe adam kwa hali yoyote ile."


Humaira alim'busu adam na kumkumbatia tena kisha wakaondoka zao.




Upande wa nathan na reshma,reshma alimuaga nathan kua anaelekea kwa rafiki yake lakini hatochelewa kurudi, nathan alimuomba sana amsindikize reshma lakini reshma alimzuia,reshma alielekea kwenye chumba ambacho akitaka kupewa na mr muran lakini akakataa. Aligonga mlango na kuhisi huenda aliyekua ndani alikua adam sababu ni muda mrefu hawajaonana, alishtuka sana baada ya mlango kufunguliwa na aliyemuona alikua mr muran,wote waliimarisha nyuso zao chini,wakati mr muran anamkaribusha ndani reshma,reshma akakataa na kusema.


"Samahani nilikua nahitaji kuzungumza na adam kama yupo"


"Adam hayupo nipo mwenyewe karibu."


"Asant sana kwaheri."


Reshma aliondoka zake na kumuacha mr muran akiwa na mawazo sana maana tayari alishaanza kumsahau lakini baada ya kumuona tena tayari alianza kuumia tena kwaajiri yake.




Nathan alivyoachwa ndani pekeake akachukua laini yake ya zamani na kuiweka na ilikua kama bahati tu simu yake ikaanza kuita alipotazama namba ilikua ngeni maana bado majina yalikua hayajasoma nathan alipokea.


"hallo habari?"


"nzuri, nathan uko wapi mpenzi wangu?, nimekukumbuka sana,mwenzio tafadhali nakuomba uje unione mwenzio nina halo mbaya"


"unamaanisha nini kusema una halo mbaya?"


"Nathan nina mimba yako, tafadhali nakuomba uje nyumbani nakuomba."


Nathan kuhusu mtoto ni jambo ambalo linamfanya awe na shauku kubwa sana,muda huo huo alisimama na kuingia chumbani alivaa surual yake na tisheti kisha akatoka nje,na hapo nje akikutana na reshma ambae alionekana kushangazwa sana kuona amependeza kiasi hiko maana alisema siku hiyo hatoenda popote wanashinda wote nyumbani lakini alishangaa kuona anatoka, alipomuuliza kua anaenda wapi nathan alijifanya anaharaka sana na kumfanya rashma akose cha kusema na kumtazama tu nathan akipotelea kwenye kona ya nyumba yao...


usikose itaendelea....

Previous Post Next Post

نموذج الاتصال