I MISS YOU 13 - 15 * MWISHO *

 I MISS YOU 13




Baada ya kupewa taarifa kua suzy amefariki nathan aliumia sana,sababu alikua anampenda na alitegemea mara baada ya kujifungua basi familia yao itakua yenye furaha na wangeweza kufunga ndoa lakini mambo yalikua tofauti.


 Mama yake pia alishtuka sana na kuanza kulia sababu alimkumbuka sana binti yake lakini hakumuona tena na siku ambayo alikua na shauku ya kutaka kumuona alijiahidi kua atamsamehe binti yake na kuanza upya lakini mategemeo pia yalikua tofauti.


Walikuwa wenye majonzi sana,nathan akiitwa na daktari na baada ya kuingia ofsini akaambiwa.

"Bwana nathan kama tulivowapa taarifa kua mtoto yupo hai,lakini afya yake haijaimarika vizuri pia amezaliwa akiwa na kifua,hahitajiki kua mbali na uangalizi wa madaktari, nachotaka kusema ni kwamba ikiwa taratibu zote za kuchukua maiti zimekamilika basi nenda kafanyeni taratibu za mazishi kisha utarudi na utamkuta kijana wako."


"Asante sana daktari, nakushukuru sana kwa msaada wako naomba umrinde sana mwanangu sitaki tena kumpoteza mtoto wangu."

"Kua na amani kila kitu kitakua sawaa."

Nathan alitoka ofsini kwa daktari na kumpa taarifa zile mama yake suzy,na kwakua tayari taratibu za kuchukua maiti zilikamilika na mama suzy alibeba jukumu la kuchukua mwili wa binti yake.


Walipofika nyumbani kwao mama adam alishuka kwenye gari Nathan na marafiki zake walisaidiana kutaka kuingiza mwili wa suzy ndani lakini adam akazuia na kuuliza.

"Enhe imekuaje,mama inamaana umemleta suzy hapa nyumbani na umesahau tote aliyotufanyia?."

"Adam mwanangu tafadhali waache wapite,dada yako ni marehemu tayari tafadhali naomba usifanye ajiskie vibaya mwanangu."

"Adam baada ya kusikia hivyo alishtuka sana,amina alimtuliza adam,na alikubali mwili wa suzy ukaingizwa ndani. Adam alikua anamtazama vibaya sana bwana nathan maana alihisi huebda yeye ndio chanzo cha dada yake kufariki kama aliweza kusababisha mimba ya reshma kutoka basi hakuwahi kumuamini tena,mara nyingi alikua anamtazama kwa chuki na hasira sana.


Hatimae mazishi yalifanyika jioni ya siku hiyo na baada ya kurudi makaburini nathan alimuuliza mama yake adam.

"Mama samahan sana sitaki kukukumbusha maumivu uliyopitia lakini Nataka kujua suzy alifanya kitu gani ambacho kilikutenga nae."

Mama huyo alishusha pumzi kisha akamjibu.

"Nathan,kwanza sikuwahi kufikiria kwamba wewe unaweza kumsaliti yule binti mpole na mrembo kwasababu ya suzy,simsemi vibaya binti yangu na wala sitaki kukufanya ukumbuke yaliyopita lakini suzy aliniumiza sana,alinisemea maneno mengi mabaya sana kipindi naumwa,na kunitamkia kua nitakufa sitapona,wakati huo adam anapambana niweze kupata dawa,na siku hiyo akamkuta dada yake ananisemea hivyo ukweli aliumia sana na kutamani hata kumpiga lakini hakuweza sababu sikupenda wawape watu faida huko nje nilimzuia na kumuaga aende moyo wangu uliumia lakini sikutaka kumtamkia neno baya lolote japo nilitamani siku moja aje amuombe msamaha niweze kumgusa tena kwenye uso wake lakini imeshindikana,naumia sana kumpoteza binti yangu kwa wakati ambao nilikua natamani kumuona."


Nathan pia aliumia kuhusu hilo na alitamani hata kusema kua suzy akimwambia wazazi wake wamefariki lakini hakutaka kufanya hivyo sababu alihisi atamuumiza zaidi hivyo ikabidi aendelee kumbembeleza mama mkwe wake kisha akamwambia.

"Mama mtoto yupo chini ya uwangalizi wa daktari,ukipata nafasi unaweza kwenda kumtazama,mimi nakwenda kazini kuimba nipewe pesa kwaajiri ya kuripia matibabu ya mtoto kisha kesho nitarejea."


Mama huyo alikubari lakini wakati anataka kuondoka adam na amina walifika nyumbani hapo wakitokea makaburini,adam alimshika nathan na kumpa ngumi mzito za kifua hadi bwana nathan,alianza kukohoa mfurulizo,na alivyotaka kumrukia teke amina akamzuia na kumwambia.

"Adam unafanya nini kila kitu kilichotokea kimepangwa tafadhali usiwe na hasira nakuomba sana mpenzi wangu."

"Amina hujui tu jinsi gani namchukia huyu mbwa,huyu alifanya maisha ya reshma kua magumu,na yenye maumivu leo hii tena amesababisha kifo cha dada yangu nawezaje kumuacha, hapanaa niacheni nimuoneshe."

Adam alimsogelea kwa kasi bwana nathan na alipotaka kumtandika ngumi nyingine mama yake akasema kwa sauti."

"Achaaa.!!"

 Adam aliganda kwa sekunde kadhaa kumtazama nathan ambae alikua amepoa sana ,hulu akitazama ngumi iliyokunjwa na adam kisawasawa,adam alimtazama nathan kisha akamsukuma na kumsogelea mama yake na kumwambia.

"Mama najua siwezi ku...!"

"Ndio najua huwezi kubadirisha chochote na huyo unaempiga tayari alikua chaguo la dada yako,na wamepata mtoto ambae bado anatuunganisha kama familia adam sitaki tena kuona ukimfanyia ubaya nathan."

Adam hakusema chochote alimsogelea nathan na kumuuliza.

"Mjomba wangu yuko wapi?."

"Mtoto yupo hospital,hali yake sio nzuri sana hivyo yupo chini ya uangalizi wa daktari."

"Tazama mtoto ambae hana hatia anaripia kwa dhambi zako nathan wewe unalaana na umefanya mtoto wako ambae ni mjomba wangu aripie kwa laana yako,mpumbavu mmoja wewe."


Adam aliingia ndani kwao hasira sana,na amina alimfata,lakini alipoingia ndani ghafla simu ya amina nayo ikaanza kuita,alipomtazama namba ilikua ngeni,alipokea na sauti aliyoisikia ilikua sio ngeni kwakwe,aliamua kukata lakini iliita tena aliitazama kwa sekunde kadhaa hadi adam akasogea karibu yake na kumuuliza.

"Mbona hupokei simu?."

"Adam aliyekua,aliye...alikua ni mpenzi wangu aanipigia mimi sitaki kurudi kwake sababu aliondoka na kuniacha kwa muda mrefu."

"Ooh Sawa pokea simu na umsikilize anataka nini."

Amina alipokea simu na kuweka sauti ya juu na kuzungumza.

"Hallow,unataka nini jay?."

"Amina,nataka kuongea na wewe, nimeskia mengi kuhusu wewe nataka kuzungumza na wewe nakuomba uje nyumbani."

"Ha.!!!" kabla hajazungumza adam alimwambia atulie Ili wapate kujua nini anataka kumwambia hivyo akamsihi akubali, mazungumzo yalimalizika na amina alikubali kwenda kuonàna na jay,lakini mara baada ya simu kukatwa amina akazungumza.


"Adam lakini nina wasiwasi kuhusu jay anaweza kufanya kitu kibaya wewe humfahamu vizuri nahofia kuhusu mahusiano yangu na yako kua yatakua hatarini."

"Mpenzi usiwe na wasiwasi kabisa nitakua nakufata nyuma sababu hatuwezi kwenda pamoja,ola nitakua nyuma yako wala usiwe na wasiwasi kabisa."

Amina alikubali lakini bado hakutaka kuamiani kwa asilimia zote kua atakua Sawa.


Baada ya kupitia siku mbili,siku ya tatu ilikua mahira ya sa10 jioni adam na amina walijiandaa na kupelekwa kituo cha tax amina alikua anamuomba adam abadirishe mawazo lakini adam alimuahidi kua asihofu,alimpandisha kwenye tax,kisha yeye akapanda kwenye tax nyingine Ili waweze kufatilia ile tax aliyokua amepanda amina.


Baada ya dakika karibia ishirini na saba waliweza kufika kwenye nyumba ambayo alikua anaishi amina ambayo alinunuliwa na jay,akamshika kwenye raxyna alipogeuka alimuona tayari adam amefika ola alijificha mbali kidogo napalee,tax iliondoka na amina aligonga mlango,na picha linaanza baada ya jay kufungua mlango alimkumbatia amina na kum'busu,kitu ambacho adam kilimuumiza na kumfanya awe nahasira na wivu lakini alijizuia,hakutaka kuwa na haraka.

Waliingia ndani akiwa amemshika kiuno ,amina alikua hataki kabisa lakini hakua na namna.

Baada ya kufika ndani jay alimkarisha amina kwenye kiti kisha akamuuliza.

"Za masiku mengi,naona nawe ukaamua kunisahau, ukanisaliti na kupoteza ahadi zote tulizokua tumepanga."

"Jay niache,uliamua kuondoka zako,yangu umeondoka hukuwahi kupatikana kwenye simu wala kunitafuta kwa bahaiti mbaya hivi unahisi mimi roboti?,nimeshindwa jay ninahisia pia niliweza kukusubiri mwanzo sababu ulikua unanitafuta japo kwa mwezi mara moja ola safari hii umeenda miezi mingapi mpaka sasa nimechoka sana sasa niache niwe na maisha yangu mengine sitaki kuishi na mtu ambae sijui anafanya kazi gani,sitaki kuishi na mwanaume ambae sijui lini atanitelekeza sitaki tena kuishi kwa mawazo na mashaka siwezi."

Amina alizungumza kwa ujasiri sana tena kwa sauti ya juu,jay alimtazama kisha akatabasam na kusema.

"Inamaana unataka kujua kazi ninayofanya? na je kama ukijua utafanya nini ikiwa tayari umepayuka kwaajiri yangu niwazi kua hunihitaji tena na mimi sina sababu ya kukuficha jazi ninayofanya,amina mpenzi ambae ulikua unanipa mapenzi hadi najihisi dunia nzima tupo mimi na wewe tu,leo mapenzi hayo anapata mtu mwingine?,ohk by the way mimi ni jambazi...!"

"Niniii!!"

"Enhe ndio hivyo...!"

Amina alishtuka sana na taarifa hizo zilimshtua sana na kugusa moyo wake na tumbo lake pia maana alihisi kama kamtetemo pale kwenye kitu alichokua amekaa...

usikose itaendelea....


 I MISS YOU 14

Wakati jay amemwambia hivyo amina ndani,hulu nje na adam alishasikia na kawaida ya jambazi hua anahisia fulani kua kama kuna mtu anawaina au kusikia kile anachozungumza na kwakua alishajua kua amina hawezi kuja pekeake hivyo hakua na mashaka kabisa akaendelea kuzungumza.


"Naona umeshtuka sana ila hiyo ndio kazi ambayo nimekua nafanya,na ndiomaan nilikua sipatikani kwa muda mrefu nilikua nafanya misheni nyingi sana na nilikua napata pesa pia na nilishajiahidi kua narudi kukuoa na sitafanya tena hiyo kazi kwasababu nilitaka kutengeneza familia na wewe baada ya kuona mwanzo ulinivumilia kumbe sikujua na wewe ni wale wale tu,lakini sawa tu ila...!,nahitaji na wewe uliokua nje uingie ndani sababu unahitaji kuona mengi sana tofauti na hayo uliyoyasikia."




Amina alishtuka sana maana alishaona wote wametiwa nguvuni hivyo hakuna ambae anaweza kuchomoka kwa jay,maana jay alikua mtu mmoja serious sana japo wanasema kwenye mapenzi hakuna komando,ila kwa huyu hata mapenzi yake yalikua ya kikomando.


Adam hakua na chakufanya alifungua mlango na kuingia ndani,nae alipewa kiti amina akamwambia.


"Adam nilikuambia ona sasa kilichotokea unafikiri tunaweza kutoka salama hapa?,adam tumekwisha tayari."


"Amina tulia, brother najua unauchungua wa kusalitiwa ndio lakini naomba msamehe sana amina,tazama na hali aliyokua nayo tafadhali."


"Anha kumbe unamuombea msamaha inamaana wakati anakupa show ukiwa unakatika na kusikiliza sauti zake za mahaba ulikua unaona raha sana hadi ukapandikiza mbegu kwenye kizazi chake afu sahivi unanibania pua eti msamehe hakunaga msamaha mrahisi hivyo."


Jay alichomoa bastora akawa anaifuta kea kitambaa huku akipiga mluzi kupitia mdomo wake amina alikua anamtazama adam aweze kufanya chochote waweze kutoka salama,adam hakua na nguvu za kushindana na jay sababu jay anamwili mkubwa uliojengeka kwa mazoezi magumu na nguvu pia alikua nazo lakini adam alikua mtoto wa mama tu hivyo hakuweza kabisa kumkabiri jay lakini alijipa moyo wa ujasiri na kumrukia jay shingoni alipokua amegeuka,kea asilimia kadhaa aliweza kumshika vema shingoni lakini hakuweza kudumu kwa muda mrefu,na aliweza kurushwa mbali na kujipigiza ukutani,adam alishuka mbavu zake kwa maumivu sana,na jay aliruka sarakasi na kuokota bastora yake kisha akacheka sana na kusema.


"Naona wapenzi wanajaribu kutaka kuniua ila hamtafanikiwa kwakua mko kwenye mikono yangu,ila wewe dogo una machaguo mawili tu kama unahitaji kubaki hai,lakwanza ni kumuuwa amina kukuacha wewe huru,au nimuache amina awe hai na wewe ila nitakuingilia kinyume Ili niweze kupoza nafsi yangu."


Adam alimtazama amina kwa maumivu sana maana mambo yote yalikua machaguzi magumu na hata amina alikataa kabisa adam asikubali ni bora yeye afe,adam alijikokota hadi alipokua amina na alipotaka kumshika jay tayari alifyatua risasi,na kuanza kucheka kwa dharau,adam alilia kwa sauti ya juu sana huku akimuomba amina asimuache mwenyewe,amina alikua akigalagala pale chini kwao maumivu makali na damu zikiwa zinamwagika kwa wingi sana hata jay pia alijipiga risasi nyingi sana na kuanguka chini.


adam alipiga simu kuomba msaada wa gari la wagonjwa na hata kituo cha polisi pia walipata taarifa hizo.




na baada ya kufika eneo la tukio adam alikua amelia sana hadi machozi yamekauka hata Sauti haikua ikitoka tena,walimkimbiza hospital amina maana alikua anapumua lakini alifariki ghafla wakiwa njiani,upande wa askari walipomuona jay walishtuka sana na kusema.


"Hili ni jambazi hatari ambalo limekua likisumbua sana na limeua watu wengi sana lakini ni wazi kua kilichomuua ni mapenzi."


Mwili wa jay ulichukuliwa pia na kwenda kupimwa yeye alikua amekufa pia.




BAADA YA MWAKA MMOJA.


Mr muran, na reshma walifanikiwa kupata mtoto wa kike,na kwa bahati nzuri reshma alijifungulia zanzibar hivyo ndugu zake wengi walifika nyumbani kwao mama yake kwaajiri ya kumpongeza.


Hata wazazi wa humaira pia,na humaira na hashim pia,walijumuika pamoja kama familia hadi muda wa chakula ulipowadia,na wakati wanaanza kula hashim simu yake iliita, aliomba kuzungumza na simu sababu hakutaka kuwasumbua hivyo alitoka nje na kuzungumza.


"Hallow,ndio kuna tatizo?."


"Ndio tena kubwa sana zaidi ya tulivyotegemea unaweza kuja ofisini?."


"Sawa nakuja."


Hashim alirudi ndani na kuwaaga kua atakwenda hospital mara moja kisha atarejea ,humaira alimfata nje maana alikua tayari ameshamzoea hashim hivyo hakutaka kabisa kumuacha mwenyewe,hivyo nae alisema.


"Naweza kukupeleka mumewangu?."


"Hapana mkewangu,baki hapa cheza na anti yako nitarudi sio muda mrefu."


"Sawa kua makini mumewangu, nakupenda sana."


Walikumbatiana kisha hashim akaondoka zake,na humaira alirudi ndani,na kuendelea na mambo mengine kama unavyojua mkikutana familia moja nasi mtaongea mambo mengi ya zamani na mautani mengi.




Hashim alifika hospital na moja kwa moja kwa daktari ambaye alikua amempigia simu alikua ni rafiki yake omari, walisalimiana kisha hashim akamuuliza.


"Vipi kaka mbona umenishtua sana?."


"Najua kaka lakini kama ulivyotaka nimefanya vipimo tena lakini naona haki yako inazidi kuwa mbaya zaidi ya tulivyotegemea,hashim nilishtuka nikahisi vipimo vinasema uongo nikamwambia rafiki yangu aliyekua hospital kubwa ya dar es salaam lakini nae ametoa majibu hayo hayo,hashim una hali mbaya sana tafadhali tunatakiwa kuwambia wapendwa wako waweze kujua. hali uliyokua nayo."


"Kaka najua unamaanisha nini lakini naogopa sana ikiwa mama yangu atasikia taarifa kama hizi na vipi kuhusu humaira sitaki kuwaumiza."


"Kaka najua lakini huna jinsi nakuomba sana usipuuzie juu ya kuwambia ukweli."




Hashim alitoka chumba hiko akavua na miwani kabisa maana alihisi kama inamuwekea uzito usoni kwake,alipanda kwenye gari na kwenda maeneo ya beach, alitulia kwa muda mrefu sana hadi majira ya usiku simu yake ikaanza kuita alitazama na kuona ni rafiki yake ambae alikua anampigia hakupokea simu.


Humaira alikaa kwa muda kusubiri simu ya hashim lakini hakupigiwa simu mama yake akamuuliza.


"Binti hebu utupishe wewe nyumbani kwako ni karibu mwambie mumeo akufate."


"Ndio mama wala hata sibaki hapa namsubiri yeye alisema atanipigia naona kimya hadi sasa."


"Mpigie simu sasa."Humaira alitoa simu yake kwenye mkoba na kutafuta namba ya omar akampigia na kumuuliza kuhusu hashim,omar alishajua kama simu hiyo ni kwaajir ya kumuulizia hashim akamwambia kua tayari ameondoka, humaira alimtafuta hashim lakini hakua akipatikana lakini muda mchache tu alisikia honi ya gari nje,aliwaaga na kutaka kuondoka akamuuliza wifi,binamu reshma shemeji huko wapi akasema kua alimfata mgeni bàsi hajarejea lakini wakati anatoka nje alikutana na shemeji yake na adam pia wakiwa wanaingia ndani, lakini akajifanya kama hajamuon alipanda kwenye gari nakuondoka zao.




Humaira kila alipokua anamtazama hashim hakuonekana kama yupo sawa akamshika mkono wake ambao alikua ameegesha kwenye paja lakini hashim alitoa mkono wake na kujifanya ameshika usukani wa gari,humaira alishagundua kua kunatatizo akasubiri wafike nyumbani Ili amuulize, walitumia dakika kadhaa tu hai kufika nyumbani kwao na walipokua wanateremka kwenye gari,hashim alibamiza mlango na kutaka kuingia ndani humaira akamuita.


"Mpenzi.!!" Hashim alisimama,humaira alimsogelea na kumkumbatia kwa nyuma lakini hashim hakujari kuhusu kumbato hilo aliingia ndani na moja kwa moja hadi chumbani,akajilaza kitandani,humaira alipoingia chumbani akaweka pochi kwenye sehemu husika kisha akavua nguo na kwenda kuoga kisha akajifuta maji na kuvaa nguo za kulalia na kukaa kitandani, akamuuliza hashim.




"Mumewangu hujawahi kua hivi kabla tafadhaii unaweza kuniambia nini kinakusumbua hadi unakua hivyo?."


Hakupata majibu yoyote hashim na alikua macho lakini niwazi alikua anawaza,baada kujiskia vibaya kukaa kimya kea muda mrefu aliamka na kukaa kitako, alishindwa kujizuia na kuanza kulia,humaira alizidi kushangazwa kwanini inakua hivyo maana haijawahi kutokea hali hiyo, alimsogelea na kumkumbatia kwa nyuma tena huku akisema.


"Mpenzi wangu,mimi ndio mwandani wako,najua unatatizo niambie mimi ni mkewako tafadhali nakuomba mpenzi unavyokua kimya sana naumia."


Hashim alijisikia faraja sana kisha akamshika mkono na kumvuta mbele yake na kumwambia.


"Humaira nisamehe sana,naomba nisamehe sana lakini sina namna ya kufanya lazima ni...ah!"


Hashim alikua anashindwa kàbisa kuzungumza alisimama na kwenda kusimama dirishani akiwa bado analia kwa maumivu sana, humaira nae alimfata na kumkumbatia kwa mbele sasa huku nae akilia pia..


je unadhani nini kinachomfanya hashim ashindwe kusema ukweli?, usikose itaendelea..

"Hapana mkewangu nitakukuta."


 I MISS YOU 15

Mr muran alimkaribisha adam ndani,reshma alifurahi sana kumuona alimkumbatia na kumwambia.




"Mdogo wangu nimuda mrefu sana hatujaonana karibu sana jamani."




"Asante sana dada, nikweli muda mrefu umepita bila kuonana ila nilikua Tabora huko ndani ndani maana kabla kuna mambo ambayo yalikua yametokea hivyo nikaamua kujitenga mbali sana na mama pia alihitaji tufanye tambiko hivyo baada ya hapo nikaamua kupumzika huko huko nimerudi hivi Karibuni nikaambiwa kua umekuja kujifungua."




"Ndio,ila mpaka kufanya tambiko lazima kutakua na jambo kubwa sana ola kwakua ni usiku bàsi uoge upate chakula kusha upumzike kesho nayo ni siku hivyo tutazungumza karibu sana jisikie uko nyumbani."




"Asante sana dada."




 Mr muran alimleta mtoto maana alikua analia na hivyo aliwakatisha mazungumzo yao na adam kisha mr muran akamuelekeza sehemu ambayo atapumzika baada ya kupata chakula.




Nyumban kwa hashim baada ya vilio na kubembelezana kwa muda mrefu ikabidi hashimu amwambie ukweli humaira.




"Mkewangu humaira nataka kukwambia kinachokusumbua ila sijui utalipokea vipi lakini siwezi tena kulificha,ila nina kansa,ambayo imekua ikinisumbua kwa muda mrefu sana,kwa mara ya kwanza nilipogundua sikumwambia mama sababu nilihisi huenda nitalitatua lakini nimeshindwa zaidi halo imefikia hatua ya mwisho kabisa hadi sasa."




"Hashim una kansa kwanini hukumwambia mama mapema lakini eeh,familia yetu ni kubwa na ina upendo huenda tungechangisha na na ungeweza kupona kwanini umekua hivi mumewangu moyo wangu unauma sana kwanini umeamua kuniambia muda huu hashim kwanini."




Safari hii majonzi yalihamia kwa humaira alijisikia vibaya sana,hashim kila alivyotaka kujitetea humaira alikua hataki kumsikiliza lakini kwa kumuhurumia tu Ili asijiskie vibaya akamkumbatia kwa nguvu sana na kumwambia.




"Hashim nakupenda sana,hata iweje siwezi kukuacha,nitakua mstari wa mbele kabisa kuhusu suala lako hili najua Mungu atakusaidia utapona nakupenda sana hashimu wangu."




Hashim alichokitarajia haikua alihisi huenda akimwambia hivyo humaira ataondoka sababu hakua anaamini kama atampenda kupitiliza hivyo,lakini mbali na hayo yote humaira alikua amebadirika sana,bàsi usiku huo ulikua wa majonzi kwao lakini walifarijiana mpaka asubuhi.




Waliamka na kusaidiana kila kitu humaira hakutaka kumuacha hashim mwenyewe walifanya usafi wa nyumba pamoja kisha wakaoga na kupata kifungua kinywa kisha humaira akasema.


"Huwenda ningejua unatatizo hilo mapema nisingekua naumiza moyo wako, nimekuumiza sana hashim nisamehe sana."


"Usijari hata hivyo nafurahi kua na wewe mkewangu nakupenda sana."




Bàsi walimaliza kula kisha wakajiandaa kuelekea nyumbani kwa mama yake hashim ambapo alikuwapo reshma,lakini asubuhi hiyo mr muran,adam na reshma walikua uwani wakizungumza,adam alikua anawasimulia juu ya kila kilichotokea kwa Nathan na suzy na yeye na amina pia,wote walishtushwa na taarifa hizo lakini walimoa mpole sana adam kwa kumpoteza dada yake na mwanamke ambae alikua anampenda sana ambae alikua na ujauzito wake,na wakati wanapeana pole,humaira na hashim walikua ndani tayari humaira alipomuuliza mama wa mtoto akaambiwa yupo uwani hivyo alipoenda alikutana na adam,adam alipomuona alianza kulengwa na machozi sana mr muran alimzuia na kumwambia kua sio wakati wake ajitulize, walisalimiana kisha wakarudi ndani na mambo mengin yakaendelea, ukweli hashim alizungumza kuhusu tatizo lake,familia ilipata taharuki kwa haraka lakini mama yake na baba yake humaira walisema kua watagharamia kiasi chochote tmcha pesa Ili aweze kufanyiwa matibabu ya haraka sana aweze kupona.




Baada ya wiki moja kupita zilibaki siku tatu ambazo hashim angeweza kufanyiwa upasuaji kuhusu ugonjwa wake wa kansa ya utumbo,mara nyingi humaira alikua anamfariji Ili asiwe na mawazo sana,awe mtu wa kawaida kila kitu kitakua sawa hashim nae alijitahidi saña kuwa mwenye furaha Ili asiwafanye watu wake wakaribu wajiskie vibaya,na walibaki pale nyumbani kwao mama yake siku hizo zote wakati wanazungumza na kufurahia mama yake alikua anamtazama huku alisikitika sana na kusema mtoto wake bado mdogo hajatimiza hata robo ya ndoto zake lakini amekuja kupata ugonjwa mkubwa sana,mama yake alikua anaumia sana moyoni mwake lakini hakua na namna yoyote zaidi ya kumuomba Mungu amsaidie kijana wake.




Hatimae siku ya upasuaji iliwadia ilikua asubuhi yenye shamra shamra za hapa na pale, familia yote ilikua hospital hapo kutaka kusubiri majibu kutoka kwa madaktari,na kama mjuavyo madaktari,mara wameingia kwenye chumba cha upasuaji mara wametoka hivyo hivyo hadi inafika majira ya sa7 mchana mr muran alimfata daktari na kumuuliza.


"Doctor mbona hamtupi majibu yoyote, tazama hapo nje kuna mama wa yule kijana ambae ni mzee na hajatia hata maji kwenye kinywa chake, kuna dada yake pia ambae nae ni mzazi hajala chochote pia na mkewake pia lakini bado na hamsemi kinachoendelea kuwapa matumaini kwanini?."




"Tunajua hilo lakini bado hajafanyiwa upasuaji presha yake imepanda sana anaogopa, unadhani tunaweza vipi kumfanyia upasuaji akiwa hivyo?."


"Dah, bàsi tunaomba nafasi walau ya mwisho tu mkewake na mama yake waweze kuzungumza nae najua ni kosa na haziruhusiwi lakini fanya kama mimi ndugu yako nakuomba"




Daktari aliwaruhusu, humaira na mama yake waliingia kwenye chumba cha upasuaji walizungumza na hashimu sana kumuomba aondoe hofu Ili madaktari wafanye upasuaji aweze kuwa sawa, madaktari waliwatoa baada ya kuona muda unaenda sana lakini humaira hakutaka kabisa kumuacha hashim hapo ndani maana alihisi amebeba uhai wa hashim alikua analia sana kea maumivu na kujuta kwanini alimuumiza sana lakini hakua na jinsi madaktari walimtoa nje lakini mara tu baada ya humaira kutolewa na hashim nae alizidi kupandwa na uoga na presha akapoteza maisha akiwa kwenye chumba cha upasuaji.




Hii iliwatia simanzi hata wale madaktari pia waliumizwa sana na maisha ya bwana mdogo hashim,na kea sura walizotoka nazo mle ndani ziliwarisha sana ndugu wa hashimu,mr muran aliitwa tena ofsini na kupewa taarifa ya msiba aliumia sana maana hakutegemea kama ingekua haraka kiasi hiko lakini hakua na chakufanya,aliwapa taarifa zile ndugu wote,waliumia sana walilia kwa uchungu sana ,humaira,mama yake hashim na dada yake pia walilia kwa uchungu sana lakini hakukua na jinsi ilishatokea.




Baada ya miezi mitatu,reshma na mr muran walirudi dar es salaam wakiwa na mama yake reshma maana hakuweza Kabisa kuishi zanzibar mwenyewe na mr muran hakua na tatzo alipenda sana familia hivyo walikua wanaishi pamoja hata na humaira pia waliishi nae pamoja.




Ikapita tena miezi mitatu bado humaira alikua anaonekana mwenye msongo wa mawazo sana mama hashim alikaa na ena kuzungumza nae kuwa yeye msichana lazima aolewe na maisha mengine yaendelee lakini humaira hakutaka kabisa kufanya hivyo sababu alihisi ataendelea kumuumiza hashim hatakama amekufa maana kifo chake anahisi yeye ndio amesababisha hivyo hakutaka kabisa,reshma pia alijitahid sana kumsihi aweze kurudiana na adam maana yeye pia alipitia matatizo kama yake, alikataa sana siku za mwanzo lakini baada ya kufikiria kwa muda mrefu aliweza kukutana na adam na kuzungumza juu ya hisia zao na wote tayari mioyo yao ilikua imefunguka upya hivyo hata wazazi wake humaira walikua radhi kumuozesha binti yao.




Maisha yaliendelea,nahatimae miaka mitano ilipita.


Siku moja reshma akiwa kwenye biashara zake ni kama bahati alimuona nathan alikua amefatana na mtoto wake alikua amekua sana reshma alimuona kwa mbali akamuita..


"Nathaniel..!!" Aligeuka maana sauti haikua ngeni,alisogea hadi alipohisi inatokea sauti iliyomuita,na kuhulizia.


"Samahani naona nimeitwa ni wewe umeniita?."


"Ndio,ni mimi inamaana hunikumbuki?."


"Ndio japo sauti kama singeni kwangu."


"Mimi ni reshma mpenzi wako wa zamani."


Nathan alishtuka sana na kumtazama mwanae akajikuta tu anashindwa kujizuia mwanzo aliona aibu lakini aliweka aibu kando kisha kumkumbatiana kisha waliweza kupiga story mbili tatu,nathan akamsimulia maisha yake yalivyokua magumu kumlea mtoto huyo hadi hapo alipofika,reshma nae akasema pia anamtoto ana miaka minne na ni wakike nathan alifurahi na kumpongeza na kumtakia heri zaidi japo alikua anamtazama kwa matamanio sana,na kusema kua amemkumbuka lakini tayari alishachelewa maana jimbo lina mtu tena linarindwa kama dhahabu.




Adam na humaira walikua na furaha sana japo hawaku barikiwa mtoto lakini upendo wao ulikua mkubwa sana,na kujaliana pia.


Na undugu wao uliendelea kukua zaidi kila siku na maisha yao yakawa na mafanikio sana kwakua walikua wanashirikiana kwenye biashara zao...




Nathan alikua akipita mara kwa mara kwa reshma kutaka kujenga urafiki lakini mwenye jimbo alikua anarinda wakati wote, nathan alilala na kushtuka ndotoni usiku kisha akasema.


"NILIMPENDA SANA LAKINI NILISHINDWA KUMTUNZA NA KUWA MVUMILIVU,SASA AMEPATA MTU SAHIHI,ANAEMJALI NA KUMTHAMINI, NIMEBAKI KUMKUMBUKA TU KWA MAZURI YAKE YOTE,SURA YAKE YA UPOLE, HURUMA YAKE, UPENDO WAKE DAAAH!!! I MISS YOU RESHMA."


"Baba unaongea pekee yako usiku wote huu?"


"Mtoto hebu lala,huijui kesho yako."


Yalikua maneno ya nathan kwa mtoto wake baada ya kuingilia mazungumzo yake..




                        ***MWISHO***


Previous Post Next Post

نموذج الاتصال