MSALA Sehemu Ya Sita-06

 

MSALA Sehemu Ya Sita-06
MSALA Sehemu Ya Sita-06

MSALA Sehemu Ya Sita-06

MSALA

Ilipoishia “Masaa manne umeyamaliza kwa kukoroma, Mwanaume halali Benjamin. Bado tupo Msitu wa Umauti” alinikumbusha Elizabeth akiwa ananitoa dripu ambayo ilikua imeshamaliza kazi ya kuniongezea damu. Kwa kiasi kikubwa nilijisikia vizuri


Nilikuta tayari ameniandalia Gongo la Mti kwa ajili ya kutembelea, nilitabasamu japo tulikua shidani lakini sikuacha kuusifu moyo wa Msichana yule nisiye mjua. Kabla hatujaanza kutoka tulisikia mlio wa Helkopta, macho yalimtoka pima Elizabeth, akasimama na kuanza kuifwatisha ile sauti huku akitazama juu


Akarudi mbio hadi mahali alipokua ameniacha


Endelea 


SEHEMU YA SITA


“Twende Benjamin” alisema kwa haraka haraka huku akinipanganisha, nami sikua Mbishi wala sikuuliza chochote nililishika gongo na kuanza kuchapa mwendo wa kuchechemea, harufu ya hatari niliivuta ikanipa ujasiri wa kuikimbia hatari. Tulikata nyika kwa haraka haraka, nilipoanguka nilijikusanya na kuendelea na safari bila ya kuhimizwa na Elizabeth


Tulifika mahali ambapo tulianza kuiyona kwa uzuri ile Helkopta ambayo muda wote nilikua nikisikia mlio wake, walishushwa Wanajeshi zaidi ya tisa kwa kutumia kamba Maalum, nilijikuta nikiwa nimeduwaa


“Hii ni ndoto si ndiyo?” nilimuuliza Elizabeth Aliyekua ameitolea macho ile Helkopta, jua la kuelekea Mchana lilikua likigonga utosi.


“Benjamin, kama unafikiria unaota simama hapo hapo ili uamke sawa, kile ni kikosi maalum kutoka Ikulu, kimetumwa kwa ajili yetu. Kwa ufupi hatuwezi kuchomoka hapa kirahisi” alisema, maneno yake mazito yaliibadili akili yangu


“Lakini Mimi sihusiki na chochote, sikujui, hatujuani. Siko tayari kuingizwa kwenye Msala nisioujua” nilisema huku nikilitupa lile gongo alilonipatia, moyo wangu uliamini kujisalimisha mbele ya kikosi kile ulikua ndiyo uamuzi sahihi zaidi. Niliona ni bora nifanye hivyo kuliko kunaswa na kuuawa kikatili, istoshe Mimi ni rubani wa shirika la ndege la Tanzania, niliona sikupaswa kuambatana na Elizabeth.


 


“Usijidanganye kua watakuacha Benjamin, wanachojua kwasasa ni kua wewe unajua ninachokijua, ngoja nikwambie kitu. Rais ananitafuta kwasababu nina taarifa zake nyeti, usikate tamaa tufike Kijijini msaada utatukuta huko” alinishawishi Elizabeth lakini tayari akili yangu ilishafanya Maamuzi ya kujisalimisha


“Sijui chochote kuhusu wewe, sijui Msala wako uneanzia wapi. Wakinikamata nitasema ukweli wangu, hakuna kitakachonifika” nilisema huku nikigeuka kurudi nyuma, Elizabeth alikuja mbele yangu, macho yake yalilengwa na chozi akaniambia


“Watakumaliza Benjamin, ulinisaidia sina budi kukusaidia pia, usijaribu kufanya hilo unalokusudia” alisema lakini maneno yake yalitokea huku yakaingilia kule, sikutaka kumpa hata chembe ya kumsikiliza na kumwelewa, nilitimbagila Mguu wangu wenye Bandeji.


Nilijitokeza eneo la wazi nikimwacha Elizabeth akiwa eneo la maficho zaidi, mara ghafla niliona miale ikigusa mwili wangu, ilikua zaidi ya miale sita, tayari kikosi maalum kilichoshuka kwenye Helkopta kilikua kimetufikia, Elizabeth alizama zaidi Msituni akikimbia. Nilinaswa, taratibu Askari walianza kujitokeza wakiwa wananielekeza Bunduki zao.


Namna nilivyowatazama kwa haraka haraka nikiwa na wenge zito niligundua mambo kadhaa kuhusu askari wale, kwanza sale zao sikupata kuziona popote hata katika filamu za mapigano, sura zao zilifichwa kwa Mask maalum, walikua na silaha nzito nzito. Maneno ya Elizabeth yakazunguka kichwani pangu huku nikiwa nazungusha shingo huku na kule nikiwa nimepiga goti na kunyoosha mikono yangu juu, jasho jingi lilikua likinitiririka


“Don’t move!” alisema Askari Mmoja, wenge likazidi kunijaa nikawa natetemeka huku nikizungukwa na wale Askari, ndani ya sekunde chache nilikua nineloa jasho mwili mzima kama nimemwagiwa maji, jua lilikua likinichoma, jasho lilivuja usoni , funda zito la mate lilinisindikiza


“Yuko wapi Elizabeth?” aliniuliza mmoja wa wale Askari, yeye alikua hajashika Bunduki mkononi, alikua na sauti nzito. Sauti na maneno yao vilinifanya nithibitishe kua yule Msichana alikua akiitwa Elizabeth. Nilitikisa kichwa changu kuashiria kua nilikua sijui mahali alipo Elizabeth, akanitolea picha ya Elizabeth.


Msichana yule alikua ndani ya hiyo picha akiwa amevalia mavazi mafupi akiwa anatabasamu


“Sijui alipo, naapa sijui, sijafanya chochote Mimi” nilisema nikizidi kutetemeka, yuke askari alisimama na kutoa agizo


“Achukuliwe huyu atasema alipo Elizabeth, epelekwa ‘Black site’….. Msako uendelee hapa Msituni” alisema yule kiongozi kisha haraka ilikuja Helkopta tayari kunichukua kunipeleka Black Site, hili ni eneo la siri la Serikali litumikalo kwa ajili ya Mahojiano kwa Watu wenye masuala mazito ambayo hata Polisi hawawezi kukabidhiwa.


NDANI YA BLACK SITE ‘SEHEMU NYETI’


Hii ndiyo sehemu hatari zaidi Duniani, kila Nchi ina hili eneo maalum kwa ajili ya uchunguzi wa masuala mazito, eneo hili halijulikani mahali lilipo lakini lipo hapahapa Tanzania. Sauti ya pangaboi ya chopa ‘Helkopta’ ilikua ndiyo sauti pekee niliyoisikia


Macho yangu yalizibwa na mfuko mweusi niliovalishwa usoni, nilijua nipo angani lakini sijui ni anga gani, Ningeachiwa macho yangu yatarai angani ningeweza kutambua kwa haraka maana Mimi ni Rubani, kirahisi ningewaambia Black Site ipo wapi lakini waliyaficha macho yangu makubwa yenye umbo la duara ili nisijuwe napelekwa wapi.


Niliona napelekwa mahali ambapo hakuna Mtu atakayejua mwisho wangu, kifo kilizidi kunisogelea lakini nilijipa tumaini sababu Mimi nilikua sina Hatia yoyote ile, kidevu changu kilijaa ndevu zilizo niwasha kutokana na ule uchafu wa tope, kwa muda akili yangu ilisahau kuhusu maumivu yangu ya Mguu.


Nusu ya akili yangu iliitamani safari ya Elizabeth, na nusu ya Akili yangu iliona kujisalimisha lilikua ni wazo sahihi zaidi kuwahi kulifikiria. Mara Chopa ilianza kushuka kwa ajili ya kutua, bado palikua kimya sana, dakika tano zilitosha sisi kushuka ndani ya Chopa, nikasukumwa kusonga mbele nikiwa sioni chochote kile


Niliamza kuhisi Ubaridi, sauti ya Chopa iliyakimbia masikio yangu, nilihisi tulikua tukiingia sehemu tulivu sana yenye kiyoyozi, milango ya chuma ilifunguka tukazama ndani zaidi, mwendo wa dakika moja nilitupwa ndani ya chumba kimoja kilicho tupu kisha niliondolewa ule mfuko.


Nikayalazimisha macho yangu kupambana na mwanga mkali wa taa ulio ndani ya chumba kile, masikio yangu yalikua yakipiga filimbi kutokana na kua kwenye kelele kwa muda mrefu


“Aaaggghh” niligugumia nikiwa najituliza sakafuni, hapakua na yeyote ndani ya kile chumba, kilikua chumba kikubwa ambacho hata basi tatu zinaweza kusimama bila shida yoyote ile.


“Aaahh” nilishusha pumzi baada ya mwili wangu kukubali uhalisia kua nilikua kikaangoni mahali pa siri sana. Baada ya muda kidogo kupita nilipata hisia kali ya joto, mwili ulichemka. Halikua joto la kawaida ni kama lilipulizwa ndani ya kile chumba tupu


Joto lile liliniumiza vya kutosha kwa zaidi ya dakika tano, mwili ulikosa nguvu


“Msaaada, nani yupo karibu anisaidie nakufaa” nilipaza sauti yangu nikiwa nina randaranda ndani ya kile chumba, jasho kali lilikua likinimwagika. Nilikaribia kuanguka chini sababu sikua na hewa nzuri ya kutosha, mara hali ya Ubaridi ya ghafla ilikuja na hapo nikaanza kupumua vyema


“Kwanini mnanitesa?” nilipaza sauti nikiwauliza walionileta pale, mara mlango wa chuma ulifunguliwa kisha nilichukuliwa na kupelekwa shemu moja, kilikua chumba kingine. Bado sikupata nafasi ya kuziona sura za watesi


Nilifungwa na kuning’inizwa kama mzigo kwenye kapani, miguu yangu ilikua imegusa chini kwa kiasi kidogo sana tena kwa kutumia vidole tu.


“Kwanini mnanitesa?” niliwauliza Watu wawili walio nihamisha kutoka kwenye chumba cha awali, wao hawakuonekana kama Askari sababu hawakua na sale zozote, walivalia suti nyeusi na Mashati meupe kwa ndani, mmoja alikua Mwanaume na mwingine alikua Mwanamke.


Walikua kimya hakuna hata aliyekohoa hata kwa Bahati mbaya, sauti za viatu vyao nilizisikia wakiwa wanaondoka na kufunga mlango, waliniacha peke yangu.


HEKAHEKA MSITUNI


Kikosi maalum kilizidi kumsaka Elizabeth Mlacha kule Msituni, muda huo alikua ameshafika Kijiji kimoja kinachoitwa Mwambisi, alijificha hapo ndani ya kijumba kidogo cha nyasi, tayari kikosi maalum kikisaidiana na Polisi kilifika Kijijini hapo na kuzingira Kijiji kizima.


“Nani ana simu?” aliuliza Elizabeth Mlacha akiwa amewaelekezea Bastola wakazi wa kijumba hicho, Baba mwenye kile kijumba alikua na simu, akampatia Elizabeth, akawataka kukaa kimya na kama watafanya mchezo wowote basi atawamaliza wote. Haraka Elizabeth aliingiza mkono kwenye chupi yake akafungua zipu na kutoa laini ya simu


Haraka haraka akaiondoa ile Laini iliyo ndani ya simu, kisha akaiweka ya kwake. Bila kuchelewa alipiga simu ambayo ilipokelewa kwa haraka sana kutoka upande wa pili, sauti ikasikika ikisema


“Upo hai?”


“Yes! Nipo Mwambisi, hali ni tete Muhonzi, nahitaji msaada kuchomoka hapa salama. Vikosi vimenizingira, sina silaha yoyote ile” alisema Elizabeth, upande wa pili ukamjibu kwa haraka


“Msaada upo njiani, jiandae kuchomoka kijijini kwanza. Pambana utoke hapo kisha tutakutana Picha ya ndege” ulisema upande wa pili


“Over!!” akasema Elizabeth kisha ile simu akaipasusa pasua baada ya kua ameshaitoa laini yake, haikutosha aliitia kwenye jiko la kuni na kuiwasha moto kabisa.


Naaam!!


Huko nje vikosi viliwasili ili kumnasa Elizabeth, Rais aliagiza ni lazima anaswe au auawe. Namna vikosi vilivyojikusanya kwa ajili ya Msichana mdogo ilileta taswira halisi ya mambo mazito ambayo Elizabeth alikua nayo. Mkuu wa Majeshi ya Polisi IGP Hassan Kitulo aliwasili Kijjini Mwambisi kwa maagizo maalum ya Rais wa Tanzania Lucas Mbelwa.


IGP Hassan Kitulo akawatangazia Wanakijiji waliokimbilia majumbani mwao baada ya kuona Vikosi vya Polisi vikifika hapo. 


Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya Saba ya MSALA hapa KIJIWENI

Previous Post Next Post

نموذج الاتصال